Swahili Times @swahilitimes Channel on Telegram

Swahili Times

@swahilitimes


Swahili Times (English)

Are you looking for a reliable source of news and information in Swahili? Look no further than Swahili Times! This Telegram channel is dedicated to providing the latest updates, news, and stories in the Swahili language. Whether you are a native Swahili speaker or simply interested in learning more about Swahili culture, Swahili Times has something for everyone. From breaking news to cultural events, this channel covers a wide range of topics to keep you informed and engaged. Join us today and stay connected with the Swahili-speaking community around the world. Swahili Times - your go-to source for all things Swahili!

Swahili Times

17 Jul, 07:37


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ameomba radhi kufuatia kauli ya ‘goli la mkono’ aliyoitoa wakati akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Kashai, mjini Bukoba ambayo imezua mjadala kwenye mitandao ya kijamii.

Swahili Times

17 Jul, 07:37


“Siwezi kuelewa mahakama inafanya kazi gani, kwa sababu mimi ndio mstahili wa kupewa hukumu. Hizi ni propaganda. Mimi bado Eng. Hersi ni kiongozi wangu pamoja na bodi yake. Lakini kama itatokea jambo lingine lolote kupitia kwangu, mimi mwenyewe nitaita vyombo vya habari nitaongea navyo. Lakini haya yaliyotokea jana [kushinda kesi dhidi ya uongozi Yanga] hazina ukweli.” – Juma Magoma, Mwanachama Yanga

Swahili Times

10 Jul, 16:12


NCCR Mageuzi yadai Mbatia ameuza mali za chama https://swahilitimes.co.tz/2024/07/nccr-mageuzi-yadai-mbatia-ameuza-mali-za-chama/

Swahili Times

28 Jun, 19:34


Tabora United hatarini kufungiwa uwanja wa nyumbani kwa kuvunja kanuni za ligi https://swahilitimes.co.tz/2024/06/tabora-united-hatarini-kufungiwa-uwanja-wa-nyumbani-kwa-kuvunja-kanuni-za-ligi/

Swahili Times

26 Jun, 17:37


Ruto akataa kusaini Muswada wa Fedha 2024 https://swahilitimes.co.tz/2024/06/ruto-akataa-kusaini-muswada-wa-fedha-2024/

Swahili Times

26 Jun, 17:37


PDPC: Wanaofunga CCTV kamera maeneo ya faragha wanakiuka sheria https://swahilitimes.co.tz/2024/06/pdpc-wanaofunga-cctv-kamera-maeneo-ya-faragha-wanakiuka-sheria/

Swahili Times

26 Jun, 07:25


"Mchezaji yeyote ambaye ataondoka Simba kwenda nyuma mwiko FC [Yanga SC] fahamu kwamba huyo mchezaji hatakiwi Simba. Kwa ufupi ni kwamba hakuna timu yoyote Tanzania hii inayoweza kumchukua mchezaji ambaye anatakiwa na Simba SC." - Ahmed Ally, Afisa Habari Simba SC

Swahili Times

10 Jun, 05:09


#NenolaSiku

Swahili Times

03 Jun, 10:09


“Tunayo idadi ya safari za ndege za moja kwa moja za kimataifa zinazokuja Tanzania, zikiwemo zile za mashirika ya ndege kama Air France, FlySafair, na Jambojet. Hivi sasa tuko kwenye mazungumzo ya kupata mashirika zaidi ya ndege yatakayokuja moja kwa moja Tanzania.” – Rais Samia Suluhu katika hafla ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa nchini Korea

Swahili Times

03 Jun, 10:08


Kiungo wa Klabu ya Azam FC, Adolf Bitegeko ameongezwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kwa ajili ya mechi za kufuzu Kombe la Dunia.

Stars itacheza ugenini Juni 11 mwaka huu nchini Zambia katika mechi ya kundi E.

Swahili Times

03 Jun, 10:08


“Ninajivunia kutambua kuwa mchango wa sekta ya usafiri wa anga nchini Tanzania umeongezeka kutoka asilimia 0.9 mwaka 2018 hadi asilimia 2.5 ya Pato la Taifa mwaka 2023.” – Rais Samia Suluhu katika hafla ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa nchini Korea

Swahili Times

03 Jun, 10:01


Ndege ya mizigo ya ATCL yachangia ongezeko la asilimia 87.78 kwenye usafirishaji https://swahilitimes.co.tz/2024/06/ndege-ya-mizigo-ya-atcl-yachangia-ongezeko-la-asilimia-87-78-kwenye-usafirishaji/

Swahili Times

28 May, 09:09


Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) inatafuta hati ya kuwakamata Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu (kulia) na kiongozi wa Hamas, Yahya Sinwar (kushoto) kwa makosa ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu kufuatia shambulio la Oktoba 7, 2023 na vita katika ukanda wa Gaza.

Wengine inaotaka wakamatwe ni Waziri wa Ulinzi wa Israel pamoja na viongozi wawili waandamizi wa Hamas.

Swahili Times

08 May, 15:20


“Nimeitwa kila aina ya jina baya. Kuna ushirika wa ajabu unaonishambulia, wapo wanaojiita wanachama wenzangu wanasema haya mambo yanazungumziwa ndani usiyaseme hadharani, ukisema hadharani unachafua chama, hapana ukizungumza hadharani kukemea rushwa unasafisha chama.” – Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA

Swahili Times

08 May, 15:19


Miji 5 Afrika yenye watu wenye uwezo mkubwa kifedha https://swahilitimes.co.tz/2024/05/miji-5-afrika-yenye-watu-wenye-uwezo-mkubwa-kifedha/

Swahili Times

08 May, 15:18


Rais Samia: Matumizi ya gesi ni lazima sio anasa https://swahilitimes.co.tz/2024/05/rais-samia-matumizi-ya-gesi-ni-lazima-sio-anasa/

Swahili Times

08 May, 09:58


TikTok imefungua kesi kuzuia sheria ya Marekani ambayo itazuia mtandao huo wa China kutumika nchini humo ikisema kitendo hicho ni ukiukaji wa haki ya uhuru wa kujieleza.

Marekani imesema mtandao huo unaweka hatarini taarifa za raia wake kwani zinaweza kuangukia mikononi mwa serikali ya China au kutumika kwa propaganda.

Swahili Times

08 May, 09:57


Rais wa Kenya, William Ruto ameagiza kufunguliwa kwa shule zote nchini humo Mei 13, mwaka huu ambazo zilifungwa kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa.

Utabiri wa hali ya hewa nchini humo umeonesha kupungua kwa mvua kubwa ambayo ililazimu ufunguzi wa shule kuahirishwa tangu Aprili 29, 2024.

Swahili Times

01 May, 11:47


Mwaka 1886 wafanyakazi katika Jimbo la Chicago nchini Marekani waliandamana wakitaka saa za kazi zipunguzwe toka saa 12 hadi saa 8, ambapo siku ya nne ya maandamano mtu asiyejulikana aliwarushia askari bomu na polisi walifyatua risasi na kupelekea vifo vya wafanyakazi wanne.

Baada ya tukio hilo, Mei Mosi husherehekewa kama Siku ya Wafanyakazi Duniani ambapo wafanyakazi hupata fursa ya kuwasilisha changamoto zao kwa waajiri.