JamiiForums @jamiiforums Channel on Telegram

JamiiForums

@jamiiforums


Official JamiiForums Telegram Channel | Be Informed, Engaged & Entertained

JamiiForums (English)

JamiiForums is the go-to destination for staying informed, engaged, and entertained. With their official Telegram channel, @jamiiforums, users can access a wealth of valuable information and engaging content. Whether you're looking to stay updated on the latest news, participate in thought-provoking discussions, or simply enjoy entertaining posts, JamiiForums has got you covered

Who is JamiiForums? JamiiForums is a popular online platform that provides a space for Tanzanians to connect, share information, and engage in meaningful conversations. Known for their commitment to promoting freedom of expression and fostering an inclusive online community, JamiiForums has become a trusted source of information and a hub for social interaction

What is JamiiForums? The JamiiForums Telegram channel, @jamiiforums, is an extension of the main platform, offering users a convenient way to access curated content, updates, and discussions. By joining the channel, users can stay informed about important news, engage with like-minded individuals, and enjoy a wide range of entertaining content

Whether you're interested in politics, current events, entertainment, or simply connecting with others, the JamiiForums Telegram channel has something for everyone. Join today to be part of a vibrant community that values knowledge sharing, active engagement, and fun-filled interactions. Be informed, engaged, and entertained with JamiiForums!

JamiiForums

14 Nov, 13:13


Mdau, ulikutana na kero au Masharti yapi yaliyokufanya ughairi kupanga au kuhamia nyumba?

Soma https://jamii.app/KeroNyumbaZaKupanga

#JamiiForums #JFMaisha

JamiiForums

14 Nov, 12:16


DAR: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Mamlaka husika kushughulikia ukusanyaji wa Taka maeneo ya Msasani kwani imekuwa kero kwa Wakazi wa eneo hilo

Pia, anasema Mamlaka inatakiwa ishughulikie suala la ukusanyaji taka jijini Dar es Salaam kwa ujumla kwani imekuwa kawaida kwa Taka kuzagaa bila Gari la taka kupita kuzikusanya

Soma https://jamii.app/TakaKeroMsasani

#JamiiForums #JFUwajibikaji #Accountability #ServiceDelivery

JamiiForums

14 Nov, 11:32


Opportunity Alert: Consultant for Technical Development of an E-learning Course

JamiiForums, through the “Mwananchi Makini” project, supported by the U.S. Embassy Dar es Salaam, is seeking a consultant to work on the technical development of an e-learning course about information fact-checking.

Key Deliverables

• Submission and presentation of a concept after the first two weeks of the assignment period
• Perfectly working and user-friendly E-learning course that is ready to be used and go public one week before the end of the assignment period
• End of Activity Report explaining the procedure and all lessons learned

Submit Your Proposal with cover letter, company portfolio, samples of previous relevant work and references by 18th November 2024.

For more info visit https://jamii.app/TechnicalDevelopmentConsultant

Apply at: [email protected]
Inquiries: +255 743 440 000

#JamiiForums #JFOpportunities

JamiiForums

14 Nov, 10:24


#JFWomen #WanawakeNaTabianchi #Accountability #ClimateChange #ClimateIssues

JamiiForums

14 Nov, 09:45


Kisukari ni Ugonjwa Sugu unaoathiri Mtu 1 kati ya 10 Duniani kote. Ugonjwa huu husababisha kiwango cha Sukari Mwilini kuzidi kiasi kutokana na Mwili kutozalisha au kushindwa kutumia Insulini kama unavyopaswa.

Baadhi ya Dalili za Kisukari ni pamoja na Kuhisi Kiu kupita Kiasi, Kupata haja ndogo mara kwa mara kuliko kawaida, Uoni Hafifu, Kuhisi uchovu kila wakati, Kupungua uzito bila kukusudia n.k

Kisukari cha aina ya 1 hakiwezi kuzuilika kwakuwa hutokana na Mfumo wa Kinga za Mwili kujishambulia zenyewe na kuzuia Mwili kuzalisha Insulini. Kisukari aina ya Pili kinaweza kuzuilika hasa kwa kuzingatia Mtindo bora wa Maisha.

Soma https://jamii.app/SukariDay

#JamiiForums #PublicHealth #DiabetesAwareness #WDD2024

JamiiForums

14 Nov, 09:16


Opportunity Alert: Consultant for Content Development of an E-learning Course

JamiiForums, through the “Mwananchi Makini” project, supported by the U.S. Embassy Dar es Salaam, is seeking a consultant to create learning materials for an e-learning course about information fact-checking.

Key Deliverables
• Submission of a draft plan for an e-learning course within the first two weeks of the assignments period
• User-friendly and relevant learning materials about mis/disinformation and strategies for information fact-checking
• End of Activity Report explaining the procedure and all lessons learned

Submit Your Proposal with cover letter, company portfolio, Samples of previous relevant work and references by 18th November 2024.

For more info visit https://jamii.app/ContentDeveloperConsultant

Apply at: [email protected]
Inquiries: +255 743 440 000

#JamiiForums #JFOpportunities

JamiiForums

14 Nov, 08:39


MWANZA: Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) imesema japokuwa 'Crane Machine' ya kwenye Meli ya MV. Victoria imetengenezwa na kuanza kutoa Huduma

Soma https://jamii.app/CraneImetengenezwa

#JamiiForums #JFHuduma #ServiceDelivery #Accountability #Uwajibikaji #Governance

JamiiForums

14 Nov, 07:35


UINGEREZA: Kampuni ya Apple inayozalisha Vifaa vya Kidigitali zikiwemo Simu za #iPhone, iPads na Laptop, imefunguliwa Kesi ya Madai ya takriban Tsh. Trilioni 10.19 ikidaiwa kulazimisha Wateja kutumia huduma za iCloud

Kesi hiyo iliyofunguliwa na Kundi la Watumiaji Huduma liitwalo 'Which?' inaituhumu Apple kukiuka Sheria ya Ushindani kwa kuwataka Wateja kuhifadhi Data zao kama Picha au Video kwenye #iCloud na kulipia gharama wanapohitaji kuongeza nafasi ya uhifadhi au kupata data zao

Apple imekuwa ikitoa Hifadhi ya Mtandaoni (Cloud Storage Space) yenye ukubwa wa Gigabytes 5 (5GB) kwa wateja wa Vifaa vyake, lakini imeweka sharti la malipo ya takriban Tsh. 40,416 kwa nyongeza ya Gigabaiti 50 na Tsh. 2,245,308 kwa Terabaiti 12 kwa mwaka

Soma https://jamii.app/iCloudSued

#JamiiForums #DigitalRights #JFDigitali #TechWorld #SocialJustice

JamiiForums

14 Nov, 07:21


DAR: Mdau anadai Watu kuanza kutupa taka katika Shimo lililopo eneo la Mkwajuni-Vijibweni imeongeza hatari za kiafya, hasa kutokana na kuongezeka kwa mbu wanaoeneza malaria, hali inayowalazimu wakazi kwenda Hospitali mara kwa mara kwaajili ya kupima na kutibu Malaria

Mdau ametoa wito kwa uongozi wa Wilaya ya Kigamboni kuchukua hatua za haraka kushughulikia tatizo hili, ili kulinda maisha yao dhidi ya madhara yanayoendelea kutokana na shimo hilo

Soma https://jamii.app/ShimoVijibweni

#JamiiForums #ServiceDelivery #JFHuduma #Uwajibikaji #Accountability

JamiiForums

13 Nov, 12:03


Mabadiliko ya Tabianchi yamekuwa na athari kubwa kwenye ndoa za Utotoni hasa katika nchi za Kiafrika, ikiwa ni pamoja na Tanzania

Ripoti ya #UNICEF ya Mei 2023 imebainisha kuwa Majanga ya Asili kama Ukame na mafuriko yanachochea ndoa za utotoni kwa familia ambazo zinakabiliwa na changamoto za Kiuchumi hasa zile za Kijijini

Ripoti imeeleza wakati wa ukame, baadhi ya familia huwaozesha Watoto wao wa kike kwa kubadilishana na fedha, vyakula au mifugo jambo linalosababisha kuongeza idadi ya ndoa za utotoni

Soma https://jamii.app/MajangaAsiliVsWomen

#JFWomen #WanawakeNaTabianchi #Accountability #ClimateChange #ClimateIssues

JamiiForums

13 Nov, 11:28


TABORA: Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mkoani humo kushughulikia kero ya upatikanaji wa Maji safi na salama Kata ya Uyui inayopatikana kwenye Manispaa Tabora

Anadai kuwa kero hiyo ni ya muda mrefu licha ya Bomba kubwa linalosambaza maji Tabora kupitia Mradi mkubwa wa maji ya Ziwa Victoria kupita kwenye kijiji hicho.

Anasema wawakilishi wa Kijiji hicho wamewatafuta wahusika wa Mamlaka ya Maji mara kwa mara lakini kumekuwa hakuna ushirikiano

Soma https://jamii.app/MajiSafiUyui

#JamiiForums #JFUwajibikaji #Accountability #ServiceDelivery

JamiiForums

13 Nov, 10:21


DAR: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa Mamlaka zinazohusika kushughulikia mashauri yanayowakabili Watumishi wa Shule ya Msingi ya Green Acres wenye tuhuma za Ulawiti na Shambulio la Aibu dhidi ya Wanafunzi kufikisha suala hilo Mahakamani

Mama wa Mtoto alipozungumza na JamiiForums amesema “Mwanangu ameharibika sana nyuma, Watuhumiwa wapo nje kwa dhamana. Nilipeleka kesi Kituo cha Polisi Oysterbay, ni zaidi ya Mwezi sasa, kila nikienda naambiwa Jalada langu bado, Mtoto hawezi kuzuia haja kubwa, inatoka tu yenyewe, anaendelea na matibabu.”

Alipolizwa Afisa wa Ustawi wa Jamii, Joyce Mtesigwa amesema “Tumeshafanya upande wetu, Mtoto ametoa maelezo yake, tunasubiri shauri litakapofika Mahakamani.”

Mpelelezi wa Kesi, Christowelu Mkumbo alipoulizwa amesema “Ahh! Kuhusu kesi ya… (Anataja jina la Mtoto) wa Green Acres, sina Mamlaka ya kujibu chochote, mimi ni mpelelezi tu nipo chini ya Mtu.”

Soma https://jamii.app/WalimuGreenAcres

#JamiiForums #HumanRights #ChildRights #HakiZaBinadamu #SocialJustice

JamiiForums

13 Nov, 09:41


DAR: Mdau wa JamiiForums.com anasema Mazingira na Miundombinu ya Soko la Mwanga lililopo Keko (Temeke) ni mibovu, kwasababu halijafanyiwa ukarabati kwa miaka mingi

Anadai Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na Diwani wamekuwa wakiwaahidi Wananchi kila wakati wa Uchaguzi kuwa watakarabati Soko hilo, lakini ni ahadi ambazo hazijawahi kukamilishwa na hata kufika eneo hilo hawafiki

Amedai hali hii hufanya Wananchi kuchanga mara kwa mara ili kukarabati baadhi ya sehemu ambazo ni korofi zaidi, lakini kawaida hazidumu

Soma https://jamii.app/SokoKekoMwanga

#JamiiForums #Uwajibikaji #ServiceDelivery #JFHuduma #Accountability #Governance

JamiiForums

13 Nov, 09:03


Opportunity Alert: Consultant for Technical Development of an E-learning Course

JamiiForums, through the “Mwananchi Makini” project, supported by the U.S. Embassy Dar es Salaam, is seeking a consultant to work on the Technical Development of an E-Learning Course about Information Fact-Checking.

Key Deliverables

• Submission and presentation of a concept after the first two weeks of the assignment period
• Perfectly working and user-friendly E-learning course that is ready to be used and go public one week before the end of the assignment period
• End of Activity Report explaining the procedure and all lessons learned

Submit Your Proposal with Cover Letter, CVs of lead and key personnel, Samples of previous relevant work and references by 18th November 2024.

For more info visit https://jamii.app/TechnicalDevelopmentConsultant

Apply at: [email protected]
Inquiries: +255 743 440 000

#JamiiForums #JFOpportunities

JamiiForums

13 Nov, 08:27


Kwa mujibu wa Ripoti ya Usimamizi wa Deni ya Hazina ya Taifa ya 2023/24, mkopo huo wa SGR, ambao ulitarajiwa kulipwa kupitia mapato ya reli hiyo tangu Mwaka 2020, sasa mzigo wake umeangukia Serikali Kuu kwa sababu mapato ya #SGR hayatoshi

Mikopo ya reli ya SGR inayodaiwa Kenya Railways Corporation imefikia Ksh. Bilioni 737.5, huku Jumla ya deni la SGR likiongezeka kwa Asilimia 36.8, kutoka Ksh. Bilioni 539 hadi Ksh. Bilioni 737.5 kutokana na faini hiyo pamoja na ongezeko la thamani ya Dola ya Marekani

Zaidi https://jamii.app/RejeshoSGRKe

#JamiiForums #KenyaSGR #Governance #Uchumi

JamiiForums

13 Nov, 07:39


Opportunity Alert: Consultant for Content Development of an E-learning Course

JamiiForums, through the “Mwananchi Makini” project, supported by the U.S. Embassy Dar es Salaam, is seeking a consultant to create learning materials for an e-learning course about information fact-checking.

Key Deliverables
• Submission of a draft plan for an e-learning course within the first two weeks of the assignments period
• User-friendly and relevant learning materials about mis/disinformation and strategies for information fact-checking
• End of Activity Report explaining the procedure and all lessons learned

Submit Your Proposal with cover letter, CVs of lead and key personnel, Samples of previous relevant work and references by 18th November 2024.

For more info visit https://jamii.app/ContentDeveloperConsultant

Apply at: [email protected]
Inquiries: +255 743 440 000

#JamiiForums #JFOpportunities

JamiiForums

13 Nov, 06:53


MAREKANI: Rais Mteule, Donald Trump, amemteua Mfanyabiashara Bilionea, #ElonMusk, kusimamia Idara Mpya ya Kuhakiki Ufanisi katika Utendaji wa Serikali (DOGE), ambapo jukumu hilo atasaidiana na mteule mwingine, Vivek Ramaswamy, Mtaalamu wa masuala ya Bioteknolojia

Taarifa ya #Trump imesema baadhi ya majukumu ya idara hiyo yatakuwa ni Kuondoa Urasimu, Kupunguza Masuala ya Udhibiti, Kuunda upya Idara za Serikali, kitu ambacho Elon Musk ameahidi kuwa kitasababisha mtikisiko kwenye Mfumo na yeyote ambaye hana msaada kwa Serikali

Trump ameongeza kuwa Uteuzi huo utaisha Julai 4, 2026 ukitarajiwa kuondoa matumizi ya Serikali yasiyo na msingi ya takriban Dola Trilioni 6.5 kwa Mwaka, kuweka sawa Uchumi na kufanya Serikali iwajibike kwa Watu huku ikiwa na idadi ndogo ya Watendaji.

Soma https://jamii.app/MuskDOGE

#JamiiForums #Governance #Accountability

JamiiForums

11 Nov, 18:44


UTEUZI: Rais #SamiaSuluhuHassan, amemteua Mhandisi Peter R. Ulanga kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) akichukua nafasi ya Mhandisi Ladislaus Matindi ambaye amestaafu
-
Pia, Rais amemteua Prof. Harun J. Mapesa kuwa Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere akichukua nafasi ya Prof. Shadrack Mwakalia aliyemaliza muda wake, kabla ya uteuzi huu Prof. Mapesa alikuwa Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Mzumbe
-
Soma https://jamii.app/UteuziATCL
-
#JamiiForums #Governance #Accountability

JamiiForums

11 Nov, 18:39


UTEUZI: Rais #SamiaSuluhuHassan, amemteua Mhandisi Peter R. Ulanga kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) akichukua nafasi ya Mhandisi Ladislaus Matindi ambaye amestaafu

Pia, Rais amemteua Prof. Harun J. Mapesa kuwa Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere akichukua nafasi ya Prof. Shadrack Mwakalia aliyemaliza muda wake, kabla ya uteuzi huu Prof. Mapesa alikuwa Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Mzumbe

Soma https://jamii.app/UteuziATCL

#JamiiForums #Governance #Accountability

JamiiForums

11 Nov, 17:35


UCHAGUZI: Chama cha #ACTWazalendo kimetoa taarifa kuwa Wagombea wake 51,423 wameenguliwa katika Wilaya za Temeke, Mkuranga, Kibiti, Rufiji, Majimbo mengi ya Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha kwa kigezo cha kudhaminiwa na Ngazi ya Kata

Taarifa iliyotolewa na chama hicho Novemba 11, 2024 imedai Oktoba 14, 2024, Waziri wa Tawala za Mikoa ya Serikali za Mitaa kupitia barua alielekeza kuwa Vyama vya Siasa vitaamua vyenyewe ngazi za udhamini za Wagombea lakini wanashangaa Wagombea wao kuenguliwa kwa kudhaminiwa na Kata

ACT imetoa wito kwa Waziri wa #TAMISEMI kutoka hadharani na kuwataka Wasimamizi wa Uchaguzi kuwarejesha Wagombea wote wa chamba hicho walioenguliwa

Soma https://jamii.app/WagombeaKuenguliwaACT

#JamiiForums #Democracy #Demokrasia #Governance #Kuelekea2025

JamiiForums

11 Nov, 14:41


#JFWomen #WanawakeNaTabianchi #Accountability #ClimateChange #ClimateIssues

JamiiForums

11 Nov, 13:43


Mdau wa JamiiForums.com anadai mara kwa mara ameshuhudia Watu wakikatwa Tsh. 500 badala ya Tsh. 300, huku wengine wakisimamishwa pembeni kwa muda mrefu na kuambiwa wangojee chenji hata kama Wahudumu wanayo, hii ikiwa ni mbinu ya kuwakatisha tamaa Wateja waache Chenji

Mdau ametoa wito kwa Mamlaka zinazosimamia Stendi ya Mabasi ya Magufuli kufuatilia na kuwachukulia hatua Wahudumu wanaobainika kukosa uadilifu na kama kuna upungufu wa cheji, suala hilo lishughuliwe ipasavyo ili kuondoa kero na usumbufu

Soma https://jamii.app/WahudumuKukosaChange

#JamiiForums #JFHuduma #ServiceDelivery #Accountability

JamiiForums

11 Nov, 12:11


MAZINGIRA: Mdau wa JamiiForums.com kutoka Dar ameomba Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kufuatilia Maji machafu yanayotiririka kutoka kwenye Mabwawa ya Mabibo

Amedai Maji hayo yamekuwa yakisababisha harufu kali inayosemekana kutokana na Kemikali zinazokuwa kwenye Maji hayo yanayotoka kwenye Viwanda vilivyopo eneo la Urafiki na kuwapa usumbufu wakazi wa jirani na maeneo hayo

Soma https://jamii.app/MajitakaMabibo

#JamiiForums #JFHuduma #Accountability #SociallJustice

JamiiForums

11 Nov, 10:50


DIGITALI: Mzazi/Mlezi una jukumu la kumfundisha na kumkumbusha mwanao kuepuka kuchapisha taarifa zake binafsi kama vile namba za Simu, Vitambulisho, Tarehe ya kuzaliwa, Anuani, Nywila zake na namba za akaunti zake za Benki Mtandaoni

Taarifa hizi zikiangukia kwenye Mikono isiyo salama zinaweza kutumika vibaya kufanyia uhalifu, anaweza kuibiwa Fedha zake hata utambulisho wake na hivyo kuhatarisha Usalama wake mtandaoni

Soma https://jamii.app/MzaziMlindeMwanaoMtandaoni

#JamiiForums #DigitalSecurity #ChildOnlineSafety #MtotoSalamaMtandaoni

JamiiForums

11 Nov, 10:02


#JAPAN: Wabunge wamepiga Kura na Kumchagua tena Waziri Mkuu, Shigeru Ishiba kuendelea na nafasi hiyo licha ya Muungano wake kupoteza wingi wa Wabunge katika Uchaguzi wa Baraza la chini Mwezi uliopita

Ishiba ameshinda kwa Kura 221 dhidi ya Kura 160 za Yoshihiko ikiwa ni marudio ya Uchaguzi ya Kihistoria ambayo hayajashuhudiwa Nchini humo kwa takriban Miaka 30

Imeelezwa kuwa kufanya vibaya kwa Chama cha LDP kunatokana na Kashfa za Rushwa ambazo zilimlazimu Waziri Mkuu aliyepita, Fumio Kishida, kutakiwa kuomba radhi Bungeni Januari 2024.

Soma https://jamii.app/IshibaJPPM

#JamiiForums #Governance #Democracy #Accountability

JamiiForums

11 Nov, 09:37


JF CHITCHAT: Mdau, kumbukumbu za Matukio gani zinakujia ukisikia habari za Mtihani wa Kidato cha 4?

Soma https://jamii.app/PepaIV

#JamiiForums #JFChitChat #JFMatukio

JamiiForums

11 Nov, 09:01


Maji yanapopungua kutokana na Ukame au Uharibifu wa Mazingira, husababisha Wanawake na Wasichana hutumia muda mwingi zaidi kwenda kuyafuata/kutafuta. Hali hii inawanyima Wasichana muda wa kuhudhuria Masomo na kufanya Kazi za Shule

Zaidi https://jamii.app/EffectsOfClimateChangeOnWomen

#JFWomen #WanawakeNaTabianchi #Accountability #ClimateChange #ClimateIsssues

JamiiForums

11 Nov, 08:27


MAWASILIANO: Mdau wa JamiiForums.com kutoka Singida ametoa wito kwa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kuangalia hali ya kusuasua kwa Mawasiliano katika Kata za Kikio na Misughaa

Mdau ameomba Mamlaka husika iwajibike kuchukua hatua ikiwemo kuhakikisha eneo hilo linapata Nishati ya uhakika ili huduma za Mawasiliano ziwe bora.

Soma https://jamii.app/TTCLSingida

#JamiiForums #JFHuduma #Governance #DigitalRights

JamiiForums

11 Nov, 07:53


KENYA: Naibu Rais aliyeondolewa Madarakani, #RigathiGachagua amedaiwa kukutana kwa siri na Viongozi wa Upinzani akiwemo #KalonzoMusyoka ikielezwa wanajadili mipango ya Uchaguzi wa Mwaka 2027

Mtandao wa The Star umeripoti kuwa Gachagua ameanza ushawishi kwa Vijana wa Gen Z kuhakikisha wanajiandikisha ili washiriki Uchaguzi huo akiamini wao ndio silaha ya eneo la ukanda wa Mlima Kenya ambalo linatajwa kumpa ushindi Rais Ruto katika Uchaguzi uliopita

Taarifa zaidi zinadai Chama cha United Democratic Alliance (UDA) kinatarajia kumfuta uanachama Gachagua ambaye amekuwa akipinga Sera za Rais Ruto hadharani

Soma https://jamii.app/Riggy2027

#JamiiForums #AfricanPolitics #Democracy #CivilRights

JamiiForums

09 Nov, 17:40


MARA: Mkurugenzi wa Wilaya ya Serengeti, Dkt. Maulid Madeni amesema moja ya sababu ya Wagombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuenguliwa ni kutokidhi vigezo, ikiwemo Wagombea kujidhamini wenyewe, kutochukua fomu za kugombea na baadhi kutojiandikisha kwenye Daftari la Wapiga Kura wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Amesema “Nawaasa viongozi wa Vyama vyote wawafundishe Wanachama wao au Viongozi wao kuhusu taratibu za Uchaguzi, wana nafasi ya kukata rufaa kwa kuwa bado CHADEMA wanatakiwa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.”

Awali, CHADEMA kilitoa taarifa ya Wagombea wao wengi kutotendewa haki ikiwemo wa Serengeti na kueleza kuwa wameenguliwa pasipokuwa na sababu za msingi

Soma https://jamii.app/SerengetiDED

#JamiiForums #Democracy #Kuelekea2025

JamiiForums

09 Nov, 15:46


ARUSHA: Mdau wa JamiiForums.com amelalamikia kero ya Wizi wa Mita za Maji, unaosababisha Changamoto kwa Wananchi kupata Huduma ya Maji

Anahoji, wanaoiba Mita hizo huwa wanazipeleka wapi? Mamlaka za Maji zinashughulikia vipi tatizo hilo ambalo linaongezeka?

Soma https://jamii.app/WiziMitaMaji

#JamiiForums #Uwajibikaji #Accountability #SeriviceDelivery #HudumaZaKijamii

JamiiForums

09 Nov, 14:29


UCHAGUZI: Chama cha ACT Wazalendo kimesema kimeendelea kupokea taarifa za Kutoteuliwa kwa Wagombea wake wa nafasi mbalimbali kwa sababu zisizo na mashiko, kinyume na Kanuni za Uchaguzi pamoja na misingi ya Haki, Uwazi na usawa wa Kidemokrasia

Msemaji wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa ACT, Rahma Mwita amesema Wagombea wameondolewa kwa madai ya Kutokujaza fomu kwa ukamilifu, bila kuelezea kwa undani. Madai mengine ni Wagombea kutokuwa wakazi wa maeneo husika na kukosa shughuli halali, madai yasiyo na ushahidi wa Kisheria

ACT imeeleza kuwa imeelekeza Wagombea wake wote walioenguliwa kukata rufaa kwa mujibu wa Kanuni na Muongozo wa Uchaguzi dhidi ya maamuzi mabovu yaliyofanywa na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi nchini

Soma https://jamii.app/ACTNov9

#JamiiForums #Democracy #Demokrasia #Governance #Kuelekea2025

JamiiForums

09 Nov, 13:42


DEMOKRASIA: Madiwani 10 wa Vyama vya Upinzani kutoka Halmashauri ya Mtwara, wamesusia kikao cha Baraza la Madiwani wakidai kutokubaliana na maamuzi ya msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri hiyo, ya kuwaengua baadhi ya Wagombea wa nafasi mbalimbali za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa madai ya kujaza vibaya fomu za uteuzi

Alipoulizwa Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mtwara, Abeid Kafunda amesema hajapokea malalamiko rasmi ya kimaandishi. Amewataka Viongozi wa Upinzani wanapokuwa na malalamiko, wawasiliane na Maafisa wa Uchaguzi ili kuhakikisha mchakato unafanyika kwa amani na haki

Soma https://jamii.app/MtwaraUchaguzi

#JamiiForums #Governance #Kuelekea2025 #Democracy

JamiiForums

09 Nov, 13:02


Siku chache baada ya Mtumishi wa Serikali ya Equatorial Guinea, Baltasar Engonga kukutwa na Video za Ngono takriban 400 akiwa na Wanawake tofauti, mtumishi huyo amefukuzwa kazi

Pia, tayari anakabiliwa na tuhuma nyingine za Ubadhirifu na kuhatarisha Afya ya Umma ambapo atapimwa ili kubaini kama ana magonjwa ya zinaa

Soma https://jamii.app/SakataEquatorialGuinea

#JamiiForums #JFMatukio

JamiiForums

09 Nov, 11:42


DAR: Mdau wa JamiiForums.com kutoka Mtaa wa Mwananyamala Kisiwani Kwa Kidile, anasema kuna Takataka zimekusanywa sehemu za Makazi kwa takriban Wiki, hadi funza na Wadudu wengine wameanza kusambaa

Anasema, kwa hali ilivyo Maambukizi ya Magonjwa mbalimbali ikiwemo Kipindupindu yanaweza kutokea endapo Mamlaka zinazohusika zitaendelea kufumbia Macho hali hiyo

Soma https://jamii.app/UchafuMwananyamala

#JamiiForums #HudumaZaKijamii #SeriviceDelivery #Accountability #Uwajibikaji

JamiiForums

09 Nov, 10:30


DEMOKRASIA: Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema baada ya Waziri wa TAMISEMI kuwataka Wagombea walioenguliwa wakate rufaa, leo Novemba 09, 2024 kimepokea taarifa kuwa Ofisi za Watendaji wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji zimefungwa kuanzia Bukoba Vijijini, Dar, Simiyu, Solwa, Bariadi na maeneo mengine Nchini

CHADEMA imeeleza kuwa kuna Wasimamizi wa Uchaguzi ambao wameondolewa kwenye nafasi zao baada ya kufanya teuzi Novemba 8, 2024 huku wa Buhigwe na Kigoma wakishushwa Vyeo na kuteuliwa wasimamizi wapya

CHADEMA kimewataka Wanachama, Wagombea na Viongozi walioenguliwa, wakate rufaa na kwenda kuziwasilisha kwenye Ofisi za Watendaji na kama zimefungwa, wakae hapo mpaka zitakapofunguliwa na Watendaji kupokea mapingamizi yao

Soma https://jamii.app/CDMRufaaKufungwa

#Uwajibikaji #Accountability #JamiiForums #UchaguziSerikaliMtaa #Democracy

JamiiForums

09 Nov, 09:49


TANZIA: Lawrence Nyasebwa Mafuru, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango amefariki leo Novemba 9, 2024 katika Hospitali ya Apollo Nchini India, alipokuwa akipatiwa matibabu

Akiwa Mtaalamu wa masuala ya Fedha kwa zaidi ya Miaka 20, amewahi kuwa Msajili wa Hazina, Mkuu wa Hazina katika Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, na Mwenyekiti wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA)

Soma https://jamii.app/RIPMafuru

#JamiiForums #JFMatukio

JamiiForums

09 Nov, 08:32


DEMOKRASIA: Jeshi la Polisi limesema baada ya uteuzi wa Wagombea wa nafasi za Serikali za Mitaa, kuna Chama cha Siasa kimepanga na kinahamasisha wafuasi wake kudhuru Watu na kuharibu Ofisi za Serikali

Taarifa ya Polisi imesema uhamasishaji unafanyika kwa njia mbalimbali ikiwemo kukutana, kupigiana Simu, kutumiana ujumbe na kwa kutumia makundi sogozi (WhatsApp)

Aidha, imeeleza kuwa Viongozi wa Vyama vya Siasa na Wafuasi wanaoona kuna kasoro katika mchakato wa uteuzi wa Wagombea wao, wafuate Sheria na Kanuni zinavyoelekeza

Soma https://jamii.app/OnyoPolisiVurugu

#JamiiForums #Governance #Democracy #UchaguziSerikaliMtaa #Kuelekea2025

JamiiForums

09 Nov, 07:01


MBEYA: Mahakama ya Wilaya ya Kyela imemhukumu kifungo cha nje cha Mwaka mmoja, Mwanafunzi wa Kidato cha 4 mwenye Umri wa Miaka 17 wa Shule ya Sekondari Ikimba na kumuamuru kumlipa fidia mwathirika ya kiasi cha Tsh. 200,000 baada ya kukutwa na hatia ya kubaka na kumpa mimba Mwanafunzi

Kamanda wa Polisi Mkoa, SACP Benjamin Kuzaga amesema Kijana huyo Mkazi wa Kijiji cha Kilambo, alitenda makosa hayo dhidi ya binti mwenye Umri wa Miaka 17, Mwanafunzi wa Kidato cha 3, aliyekuwa akisoma Shule moja na Mshtakiwa

Hukumu imetolewa na Hakimu Paul Barnabas - SRM kwa mujibu wa Kifungu cha 130 kifungu kidogo cha Kwanza na cha Pili (e) na Kifungu cha 131 kifungu kidogo Cha pili (a) vyote vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu na Kifungu cha 60A kifungu kidogo cha Tatu cha Sheria ya Elimu

Soma https://jamii.app/MiakaMahakamani

#JFMatukio #JamiiForums

JamiiForums

09 Nov, 04:59


Maneno ya Heshima na Motisha humfundisha Mtoto thamani yake, kumjenga Kisaikolojia, na kumwezesha kukua kwa kujiamini na kujiheshimu

#JamiiForums #ParentingJourney #Malezi #AmkaNaJF #GoodMorning #ChildRights #SafariMaleziBora #Maisha

JamiiForums

08 Nov, 18:58


DIGITALI: Programu za "Parental Control" husaidia kulinda usalama wa Mwanao mtandaoni kwa kuzuia upatikanaji wa maudhui hatarishi, kudhibiti muda anaotumia mtandaoni na kudhibiti watu anaowasiliana nao

Aidha, programu hii inakuwa na ufanisi pale kunapokuwa na uangalizi na ufuatiliaji wa karibu kutoka kwa Mzazi/Mlezi

Soma https://jamii.app/MzaziMlindeMwanaoMtandaoni

#JamiiForums #DigitalSecurity #ChildOnlineSafety #MtotoSalamaMtandaoni

JamiiForums

05 Nov, 10:20


TABORA: Siku chache baada ya baadhi ya Wanachama wa JamiiForums.com kulalamika kuhusu changamoto ya kukatika kwa Umeme mara kwa mara, JamiiForums imezungumza na Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja TANESCO - Tabora, Mwanahamisi Hussein ili kupata ufafanuzi zaidi

Mwanahamisi amesema kulikuwa na hitilafu iliyotokea katika Transfoma mbili kwenye Kituo cha kupooza Umeme cha Kiloleni na kusababisha mgawo wa Umeme kwa nyakati tofauti kwa Wateja wa Mjini Kati

Kuhusu Uyui, amesema "Kuna siku ambazo kunakuwa na 'plant shutdown' kwaajili ya matengenezo ya kawaida, tumekuwa tukitangaza katika Vyombo vya Habari vya huku".

Soma https://jamii.app/TanescoUyuiTabora

#JamiiForums #Accountability #HudumaZaKijamii #Uwajibikaji

JamiiForums

05 Nov, 09:49


Ripoti ya Benki ya Dunia (2019) - “Tanzania - Country Environmental Analysis” inaonesha maeneo ya Vijijini Tanzania yanaathirika kwa kiwango kikubwa na mabadiliko ya TabiaNchi, hivyo kusababisha changamoto za shughuli za Kilimo na upatikanaji wa maji

Ukame, Mafuriko, mabadiliko ya misimu, upepo mkali, joto kali au vimbunga vinaweza kupunguza upatikanaji wa maji na rutuba ya ardhi, jambo linalowaathiri moja kwa moja Wanawake wa Vijijini katika maisha yao ya kila siku kutokana na utegemezi wao mkubwa kwa rasilimali hizo

Pia, ripoti inaonesha Wanawake wa Vijijini ndio wanaobeba mzigo mkubwa zaidi wa Mabadiliko ya TabiaNchi kwakuwa wao hujihusisha zaidi na shughuli za kilimo na kuteka maji.

Soma https://jamii.app/WanawakeWaVijijini

#JamiiForums #ClimateIsssues #ClimateChange #WanawakeNaTabianchi #JFWomen

JamiiForums

05 Nov, 09:29


DAR: Mdau wa JamiiForums.com anasema kuna hatari ya kuibuka kwa Magonjwa ya Mlipuko kutokana na Utiririshaji wa Maji machafu katika eneo la Ubungo Riverside

Anaziomba Mamlaka za Mazingira, Afya, Serikali ya Mtaa na Wananchi zichukue hatua za haraka kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.

Soma https://jamii.app/MajiTakaUbungoRiverside

#JamiiForums #Accountability #Afya #Uwajibikaji

JamiiForums

05 Nov, 08:47


MBEYA: Mdau wa JamiiForums.com ametoa wito kwa mamlaka kushughulikia suala la usafi kwa kuwajengea Wachimbaji Migodi vyoo ili kuepusha magonjwa ya mlipuko kama Kipindupindu

Aidha, ametoa wito kwa mamlaka kutoa taarifa kuhusu madai ya uwepo wa Ugonjwa wa Kipindupindu Jijini hapo ili Wananchi wachukue tahadhari

Soma https://jamii.app/UwepoKipindupinduMbeya

#JamiiForums #Accountability #ServiceDelivery

JamiiForums

05 Nov, 07:40


Opportunity Alert: Consultant needed for Citizenship and Leadership Academy Content Development

JamiiForums, in partnership with WiLDAF via the USAID's Wanawake Sasa Project, is seeking a Content Development Consultant to create engaging, inclusive training modules and promotional materials for our Citizenship and Leadership Academy. This consultancy aims to empower Tanzanian women and girls in civic and political engagement.

Key Deliverables:
• Inception Report on project objectives, methodology, and planned outputs
• User-friendly, relevant content to enhance women and girls’ civic and leadership skills
• Designed Promotional Materials

Submit Your Proposal with detailed proposal, methodology, budget, CVs of team members, samples of past work, and references by 5th November 2024.

For more info visit https://jamii.app/ContentDeveloperCLA

Apply at: [email protected]
Inquiries: +255743440000

#JamiiForums #JFOpportunities

JamiiForums

05 Nov, 07:16


USAFIRISHAJI: Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imewaomba radhi abiria waliokuwa na ratiba ya kusafiri kutoka Mumbai kwenda Dar es Salaam Novemba 4, 2024, kuwa watarejea Dar leo Novemba 5, 2024

ATCL imesema mabadiliko hayo yametokana na hitilafu ya kiufundi iliyotokea kwenye Ndege yake (Air Tanzania) na kuongeza "Kwa kuzingatia kipaumbele chetu cha usalama, abiria wote waliokumbwa na mabadiliko haya wameshapatiwa huduma stahiki na wanatarajiwa kurejea nchini Novemba 5, 2024)"

Aidha, taarifa imesema Ndege hiyo inatarajia kuendelea na ratiba zake za #Mumbai kwenda Dar es Salaam kuanzia Novemba 6, 2024.

Soma https://jamii.app/ATCLMumbai

#JamiiForums #JFHuduma #Accountability #ServiceDelivery

JamiiForums

05 Nov, 06:56


Opportunity Alert: Consultant Needed for Software Development of Citizenship and Leadership Academy

JamiiForums, in partnership with WiLDAF and Her Initiative, are looking for a highly skilled Software Developer for USAID-supported Wanawake Sasa Project. This consultancy aims to create an interactive, competence-based learning platform to empower Tanzanian women and girls with civic knowledge and leadership skills.

Key Deliverables:
• Needs Assessment Report of platform requirements
• Platform Design & Architecture
• Fully Functional Online Platform
• Training & Documentation of user manuals
• Technical Support Plan

Submit Your Proposal including your methodology, work plan, budget, relevant past projects, and CVs of key team members by November 5, 2024.

For more info visit https://jamii.app/SoftwareDeveloperCLA

Send to: [email protected]
Inquiries: +255743440000

#JamiiForums #JFOpportunities

JamiiForums

05 Nov, 06:44


Baada ya Mdau JamiiForums.com kutoka Geita kulalamikia kero ya Huduma ya Maji, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema Hali ya upatikanaji wa Maji kwa sasa kwa Mji wa Geita ni asilimia 75 kwa Wakazi wasiopungua 360,000.

Aidha, amesema Serikali inaendelea na Mradi wa utanuzi wa Chujio la Maji Safi eneo la Nyankaga kwa gharama ya Tsh. Bilioni 1.17 ambao umefikia asilimia 95. Kukamilika kwa Mradi huo Mwezi Novemba 2024 kutaongeza Lita milioni 11 kwa Siku kutoka Lita milioni 8 kwa za sasa.

Mdau wa JamiiForums.com alisema Rais Samia alipofanya Ziara Mwezi Oktoba karibu maeneo mengi yalipata Maji ila alivyoondoka shida imerudi pale pale ambapo maeneo mengi ya Geita yanapata Maji ya bomba mara moja kwa wiki

Soma https://jamii.app/AwesoMajiGeita

#JamiiForums #Accountability #ServiceDelivery #Uwajibikaji #HudumaZaKijamii

JamiiForums

05 Nov, 05:43


Mdau wa JamiiForums.com aliyejitambulisha kuwa mtumiaji mzuri wa Mfumo wa #NeST anadai mfumo huo umekuwa na changamoto ya Mtandao kiasi kwamba Inaonekana kama unaelemewa na hivyo anatoa wito kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kuchukua hatua kwa kuwa hali hiyo imekuwa kero

Akifafanua, Afisa Uhusiano wa Umma wa PPRA, Joseph Muhozi anasema “Inapotokea hali hiyo tumekuwa tukitoa taarifa kwa Wadau wetu kwa kuwatumia barua pepe, tunafanya jitihada za kutosha ili kuwa na mtandao imara, pamoja na hivyo kuna muda Mdau anaweza kuwa na shida ya Mtandao yeye mwenyewe na sio mfumo.”

Soma https://jamii.app/MfumoWaNeST

#JamiiForums #ServiceDelivery #Accountability #Governance #Uwajibikaji #DigitalRights

JamiiForums

05 Nov, 04:09


Kila Mtoto ana uwezo na kasi yake ya kujifunza vitu. Kumlinganisha na wengine kunaweza kumfanya ajihisi hafai au kushindwa

Badala yake, mtie Moyo kwa kuzingatia juhudi na Maendeleo yake binafsi.

#JamiiForums #ParentingJourney #Malezi #Maisha #AmkaNaJF #GoodMorning #ChildRights #SafariMaleziBora

JamiiForums

30 Oct, 16:47


MWANZA: Mdau wa JamiiForums.com anatoa wito kwa mamlaka husika kukarabati Barabara ya Mtaa wa Green View uliopo Kata ya Nyamanoro, Manispaa ya Ilemela akidai imechakaa na inasababisha usumbufu kwa Watumiaji

Soma https://jamii.app/BarabaraNyamanoroKero

#JFHuduma #JamiiForums #ServiceDelivery #Accountability

JamiiForums

30 Oct, 15:57


Mdau wa JamiiForums.com kutoka Mkoani Singida amelalamikia kero ya Mamlaka ya Maji Singida (SUWASA) kwa kuwabambikia bili za Maji ambayo hawajatumia

Amedai, kuna jirani yake hana Maji tokea Mwezi Septemba lakini ameletewa bili ya Tsh. 10,500 na hivyo anatoa wito kwa Mamlaka hiyo kuwaelewesha namna wanavyopiga hesabu za matumizi ya Maji na kuandaa Bili za Wateja.

Soma https://jamii.app/BiliZaMajiSingida

#JamiiForums #ServiceDelivery #JFHuduma #Governance #Accountability

JamiiForums

30 Oct, 15:10


DIGITALI: Kutokana na ukuaji wa teknolojia ni muhimu kwa Watoto kuwa na Elimu ya Matumizi Sahihi na Salama ya Mtandao ili kuepuka athari za matukio ya uhalifu mtandaoni

Endapo Watoto watatumia mitandao bila usimamizi wa Wazazi au Walezi wanaweza kukutana na changamoto mbalimbali wakiwa mitandaoni kama vile maudhui yasiyofaa pamoja na habari potofu

Aidha, kuwapatia muongozo na elimu sahihi Watoto kutasaidia kutumia vifaa kwa uangalifu na kuepuka kuingia katika tovuti zisizo salama au kupakua 'apps' hatarishi

Soma https://jamii.app/MtotoSalamaMtandaoni

#CybersecurityAwarenessMonth #JamiiForums #DigitalSecurity #DigitalSafety #DigitalRights #JFDigitali #CyberCrime #StaySafeOnline

JamiiForums

30 Oct, 14:23


ARUSHA: Mdau wa JamiiForums.com anadai eneo la Mti Mmoja - Monduli Wananchi wanatumia Maji ya Bwawa yaliyotuama ambayo ni hatari kwa #Afya na wanaiomba Serikali kufanya juhudi za haraka kuwapatia Maji safi kwa kuwa kinachoendelea kwa sasa ni kero kubwa kwao

Wale wanaohitaji Maji safi wanayapata eneo linaitwa Duka Bovu ambapo ni umbali wa zaidi ya Kilometa 20, wananunua kwa Tsh. 50,000 Lita 1,000 jambo ambalo ni gumu kwa Wananchi kumudu gharama

Soma https://jamii.app/MajiMonduli

#JFHuduma #JamiiForums #ServiceDelivery #Accountability

JamiiForums

30 Oct, 13:51


PWANI: Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) imesema huduma ya Kivuko cha MV. Kilindoni imerejea na huduma katika njia ya Nyamisati kuelekea Mafia imeanza baada ya majaribio ya takriban saa nne

Meneja wa Vivuko Kanda ya Mashariki na Kusini, Mhandisi Abdulrahman Ameir amewaomba radhi wakazi wa maeneo hayo kwa kipindi chote ambacho kivuko hicho hakikuweza kutoa huduma tangu kilipopata hitilafu Oktoba 10, 2024, hali iliyochangia Wananchi wengi kutumia Vyombo vya Usafiri visivyo salama na vya uhakika

Soma https://jamii.app/MVKilindoni

#JFMatukio #Accountability #Governance #ServiceDelivery #JFHuduma

JamiiForums

30 Oct, 13:33


Mjadala zaidi https://jamii.app/KutembeaUmbaliMrefu

#JamiiForums #JFStories #JFChitChats #LifeLessons

JamiiForums

30 Oct, 12:27


MAWASILIANO: Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa amekiri uwepo wa changamoto ya mitandao ya mawasiliano ya Simu Nchini na kuwa wamepokea malalamiko kuhusu Mtandao wa Vodacom ambao umeeleza unafanya maboresho ya Mifumo yake

Kutokana na changamoto hiyo, Waziri Silaa ametoa maagizo kwa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kufanya tathmini ya suala hilo ili kubaini kama ni tatizo la Kiufundi au kuna uzembe ambao unapaswa kuchukuliwa hatua

Kauli ya Waziri Silaa inakuja ikiwa ni baaada ya uwepo wa malalamiko ya Watumiaji wa mitandao mbalimbali wakiwemo wa JamiiForums.com kuhusu kusuasua kwa huduma za Mtandao ambapo Vodacom imesema kwa upande wake ipo katika kipindi cha maboresho ya mifumo yake ya #TEHAMA na tatizo litamalizika katikati ya Novemba 2024

Soma https://jamii.app/TCRAIfanyeTathminiMitandao

#JamiiForums #DigitalWorld #Governance

JamiiForums

27 Oct, 18:39


Kusoma kwa undani habari hizi na mengine yaliyojiri wiki hii bofya https://jamii.app/YaliyojiriWikiHii

#JamiiForums #YaliyojiriWikiHii #JFToons

JamiiForums

27 Oct, 15:36


ZANZIBAR: Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Riziki Pembe Juma, amesema ukatili na unyanyasaji kwa Mama na Watoto ni janga kubwa linaloharibu familia nyingi na kusisitiza kuwa inawezekana kuiondoa hali hiyo

Amesema ili kupambana na hali hiyo imezinduliwa Kampeni ya "MTOTO NI MBONI YANGU" iliyoandaliwa na Wizara ya Maendeleo kwa kushirikiana na Taasisi ya “Ndoto Ajira” ya Dar es Salaam, itakayofanyika Novemba 2024 katika Mikoa mitano ya #Zanzibar (Unguja na Pemba), lengo likiwa ni kutokomeza matukio yote ya unyanyasaji

Amesema Kampeni hiyo itaendana na Marathon itakayoshirikisha Washiriki 20,000 kutoka Bara na Visiwani, ikiwa na mpango wa kukusanya Tsh. Milioni 650 zitakazotumika katika utekelezaji wa kampeni hiyo

Soma https://jamii.app/KupingaUkatili

#JFMatukio #ChildRights #HumanRights #JamiiForums #HakiZaBinadamu #SocialJustice #Accountability #Governance

JamiiForums

27 Oct, 12:25


PWANI: Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Uchukuzi na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa zimesema zitaunda Timu Maalum kusimamia urejeshaji wa huduma ya usafiri wa Vivuko vya MV Kilindoni na Meli ya TNS Songosongo, vinavyofanya safari kati ya Kituo cha Mafia - Nyamisati (Kibiti) vilivyosimamisha huduma tangu Oktoba 10, 2024

Wakati huohuo, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Eng. Aisha Amour na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Ufundi na Umeme (TEMESA), Lazaro Kilahala kufika Mafia na kupiga kambi mpaka huduma ya usafiri wa Kiivuko itakaporejea na kutoa huduma

Ikumbukwe, Februari 2024 baadhi ya Wadau wa JamiiForums.com walitoa maoni kuwa baadhi ya Watendaji wa Serikali wawe na uchungu na kodi za Wananchi katika matumizi ya fedha za Umma katika masuala ya matengenezo ya Vivuko mbalimbali Nchini wakidai kuna matumizi yasio sahihi

Soma https://jamii.app/VivukoMaboresho

#JFMatukio #Accountability #Governance #ServiceDelivery #JFHuduma

JamiiForums

27 Oct, 11:04


DAR: Mdau wa JamiiForums.com kutoka Soko la Tandika, Temeke ameziomba Mamlaka husika kurekebisha hali ya Miundombinu ya Soko hilo ikiwemo Mitaro ya Maji Machafu kwa kuwa imekuwa ikisababisha Uchafu na Nzi

Anadai, licha ya Halmashauri ya Temeke kukusanya Ushuru wa Vibanda kila siku na kuahidi kufanya ukarabati lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika na hali inazidi kuwa mbaya

Soma https://jamii.app/MdauTandika

#JamiiForums #SocialJustice #JFHuduma #Governance

JamiiForums

27 Oct, 08:22


MAZINGIRA: Mdau wa JamiiForums.com kutoka Ubungo Kisiwani, Dar es Salaam, ameomba Mamlaka ziwasaidie kujenga Kuta za Mitaro katika Mto Gide kwakuwa umekuwa ukichimbika kila wakati na kubomoa nyumba za jirani

Anadai hadi sasa zaidi ya nyumba 40 zimebomoka kutokana na athari za Mto huo huku makazi ya watu wengine zaidi ya 500 yakiwa hatarini kutokana na Mto huo kutojengwa Kuta za kuzuia Maji

Soma https://jamii.app/MitaroUbungo

#JamiiForums #SocialJustice #JFHuduma #Governance

JamiiForums

27 Oct, 06:15


#AfyaYaAkiliKazini #MentalHealthAwareness #PublicHealth #AmkaNaJF #JFMotivations #GoodMorning

JamiiForums

26 Oct, 15:33


Umesoma mara ngapi kugundua kosa? 😂

#JamiiForums #JFChitChats #ChemshaBongo

JamiiForums

26 Oct, 14:46


Yafahamu makosa 11 yaliyosababisha #RigathiGachagua kuondolewa Madarakani akiwa Naibu Rais wa Kwanza kung’olewa Nchini Kenya tangu kutambulishwa kwa Mfumo huko katika Katiba Mwaka 2010

#JamiiForums #Democracy #Governance

JamiiForums

25 Oct, 15:40


LIGI KUU BARA: Magoli ya Shomari Kapombe dakika ya 5 na Jean Charles Ahous (34) pamoja na Debora Fernandes (84) yanaiwezesha Timu ya Simba kupata ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Namungo FC kwenye Uwanja wa KMC, Dar es Salaam

Ushindi huo unaiwezesha Simba kufikisha alama 19 katika michezo Nane, ikiwa nyuma ya Singida Big Stars ambayo ina pointi 22 katika michezo Nane pia ambapo katika mchezo wa mapema leo, Oktoba 25, 2024 timu hiyo ilishinda Magoli 2-0 dhidi ya Fountain Gate

Soma https://jamii.app/Simba3Namungo

#JFSports #JFLigiKuu24 #JamiiForums

JamiiForums

25 Oct, 14:55


Zoezi la Uandikishaji Wananchi watakaoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024 limekamilika, ambapo kwa mujibu wa TAMISEMI, takriban Watu Milioni 32.9 (94%) wamejiandikisha

Mdau, ulijiandikisha? Unazungumziaje uendeshaji wa zoezi hilo ikiwa ni takriban Mwezi Mmoja umesalia kufikia siku ya Kupiga Kura?

Ungana na Wananchi wengine Oktoba 31, 2024 Saa 12:00 Jioni kutoa maoni kupitia #XSpaces ya JamiiForums katika Mjadala utakaoangazia Mchakato Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024

Kushiriki bofya https://jamii.app/MitaaElectionSpaces

#JamiiForums #JFDemokrasia #Governance #CivilRights #MitaaElection24 #JFSpaces #MitaaSpaces2024 #MitaaSpaces

JamiiForums

25 Oct, 13:02


Mdau, jambo gani Muhimu huwa lazima ulifanye kila Mwisho wa Mwezi unapofika?

Mjadala zaidi https://jamii.app/EndOfMonth

#LifeLessons #JFStories #Maisha #JFChitChats #JamiiForums

JamiiForums

25 Oct, 10:49


SIMIYU: Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoani humo kimedai kuwa baadhi ya Mitaa imeongezewa majina ya Wapiga Kura kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mtaa, kinyume na utaratibu uliokuwa ukitumiwa wakati wa uandikishaji na kuwa hakitakuwa tayari kuona majina yaliyoongezwa yakihusishwa katika upigaji wa Kura

Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Simiyu, Mussa Onesmo ametaja baadhi vituo anavyodai vimeongezewa majina Mtaa wa Nyakabindi, Gagabali, Muungano, Mwahnunda, Guya, Nghesha (Bariadi Mjini na Vijijini)

Akijibu madai hayo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Adrian Jungu amesema “Kanuni inaruhusu kuweka pingamizi kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Ngazi ya Kata kama Mwananchi hajaridhishwa, Shauri litafanyiwa kazi ndani ya Siku Mbili, wasiishie kulalamika pembeni.”

Soma https://jamii.app/UchaguziSimiyu

#Kuelekea2025 #Democracy #Governance #JamiiForums

JamiiForums

25 Oct, 10:01


Mdau ndani ya Jukwaa la JF Chit- Chat and Jokes ameelezea jinsi alivyojibana Kiuchumi akiwa Chuo kuweza kununua Simu ila baadaye ikaja kuibiwa na jinsi ilivyomuathiri

Kwako mdau, Simu yako uliyonunua kwa gharama kubwa bado unayo?

Mjadala zaidi https://jamii.app/SimuYagharamaKuimiliki

#JamiiForums #JFChitChats

JamiiForums

25 Oct, 08:53


Position: Consultant Citizenship and Leadership Academy (CLA) Software Developer

Organization: JamiiForums

RESPONSIBILITIES:
1). Platform Development
2). Integration of Learning Tools
3). Ensuring Data Security
4). Testing and Quality Assurance
5). Training and Documentation
6). Support and Maintenance

REQUIREMENTS:
1). Proven experience in software development for e-learning platforms
2). Strong expertise in developing user-friendly and accessible platforms.
3). Experience with Learning Management Systems (LMS) and Content Management Systems (CMS).
4). Expertise in UI/UX design with a focus on interactive, mobile-friendly platforms.
5). Strong understanding of security and data privacy

Send your Portfolio, CVs of Key team players Technical and financial proposals to: [email protected] before 29th October, 2024

For any inquiries please call (or WhatsApp) +255 743 440 000.

More details https://jamii.app/SoftwareDeveloperCLA

#JamiiForums #JFOpportunities

JamiiForums

25 Oct, 08:40


MAWASILIANO: Takwimu za Mawasiliano ya Huduma za Simu kwa Robo Mwaka (Juni - Septemba 2024) zinaonesha kulikuwa na ongezeko la Laini 4,137,981 za Mawasiliano ya Mtu kwa Mtu (P2P) na Laini Milioni 1.02 za Mawasiliano ya Mashine (M2M) hivyo kuwa na jumla ya Laini Milioni 80.7

Kwa mujibu wa Ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Mtandao wa tiGO uliongeza usajili wa Laini 1,940,468 ukifuatiwa na Haloteli Laini 1,249,745, Vodacom ilisajili Laini 1,047,768, Airtel ilipoteza Wateja 15,159, na TTCL ilipoteza Wateja 64,607

Aidha, Mtandao wa Vodacom umeendelea kuongoza kwa kuwa na laini nyingi zaidi nchini ikiwa na Laini 24,136,856, ikifuatiwa na tiGo 23,458,325, Airtel 19,492,734, Halotel 10,971,582 na TTCL 1,586,724.

Soma https://jamii.app/SimCardsQ3

#JamiiForums #DigitalRights #JFHuduma #ServiceDelivery #JFDATA

JamiiForums

25 Oct, 07:34


USAFIRISHAJI: Mdau wa JamiiForums.com kutoka Mbweni, Dar amelalamikia kero ya Usafiri aliyodai inasababishwa na Daladala zisizofuata utaratibu wa safari ambapo zimekuwa zikitumia njia ambazo hazipo kwenye maelekezo ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Ameshauri Mamlaka hiyo kuingilia kati na kuweka sawa utaratibu wa safari hizo kwa mujibu wa maelekezo ili kutowapa usumbufu na gharama zaidi Abiria wanatumia usafiri huo katika maeneo husika.

Soma https://jamii.app/KeroMbweni

#JamiiForums #JFHuduma #Accountability #Governance

JamiiForums

25 Oct, 06:24


Position: Consultant Citizenship and Leadership Academy Content Developer

Organization: JamiiForums

RESPONSIBILITIES:
1). Develop audio and written training modules
2). Design promotional materials
3). Collaborate with project implementing partners
4). Conduct desk review
5). Conduct needs assessment

REQUIREMENTS:
1). Legally recognized in Tanzania to perform consultancy tasks.
2). Competence in both Kiswahili and English language
3). Master's degree in related field
10 years experience in undertaking gender and politics analysis

Send CVs of key personnel in the assignment, Samples of previous work and Contact information from 3 previous clients to: [email protected] before 29th October, 2024

For any inquiries please call (or WhatsApp) +255 743 440 000.

More details https://jamii.app/ContentDeveloperCLA

#JamiiForums #JFOpportunities

JamiiForums

25 Oct, 04:18


#AfyaYaAkiliKazini #MentalHealthAwareness #PublicHealth #AmkaNaJF #JFMotivations #GoodMorning

JamiiForums

24 Oct, 18:27


AFYA: Ugonjwa wa Polio husababishwa na Virusi vya Polio ambavyo hushambulia Mishipa ya Fahamu na kusababisha Kupooza kwa Misuli, Homa, Mafua, Ulemavu wa Kudumu na hata Kifo

Chanjo 4 zinazotolewa pindi Mtoto anapozaliwa na akifikisha Umri wa Wiki 6, 10 na 14 husaidia kutoa Kinga ya Kudumu ya Ugonjwa huu

Soma https://jamii.app/PolioVaccine

#PolioDay #PolioFreeWorld #PublicHealth #VaccinesWork #Afya

JamiiForums

23 Oct, 08:57


MSUMBIJI: Umoja wa Ulaya umesema umebaini ukiukwaji wa taratibu wakati wa Kuhesabu Kura na hivyo baadhi ya matokeo ya Uchaguzi Mkuu yanayotangazwa hayaendani na uhalisia wa Kura zilizopigwa kwenye ngazi za Wilaya

Taarifa ya Waangalizi wa Uchaguzi wa EU imesisitiza Mamlaka za Uchaguzi kufanya mchakato wa kujumlisha Matokeo kwa njia za Uwazi, za Kuaminika na Kuhakikisha kuna ufuatiliaji wa kina wa matokeo kutoka kwenye vituo vya kupigia kura

Aidha, vurugu na maandamano vimeripotiwa kwa wanaopinga mchakato wa Uchaguzi huo ulivyoendeshwa, huku Polisi wakidaiwa kutumia nguvu iliyopitiliza, ikiwemo risasi za moto na kusababisha Vifo vya makada Wawili wa Upinzani

Soma https://jamii.app/EUMsumbiji

#JamiiForums #Democracy #AfricanPolitics #Governance #Diplomacy #MozambiqueDecides

JamiiForums

23 Oct, 08:01


Kitu cha Kumbuka: Si kila kurudia au kukwama kwa maneno kunaashiria Kigugumizi. Watoto wengi wanapokuwa wanajifunza kuongea hurudia maneno au silabi na hili linaweza kuwa sehemu ya Maendeleo ya kawaida

Kama Kigugumizi kinaendelea kwa muda mrefu au kinaathiri uwezo wa Mtoto kuwasiliana kwa ufanisi, ni muhimu kumtafuta Mtaalamu wa matamshi kwa Uchunguzi na msaada zaidi

Ikiwa unahisi Mtoto wako ana Kigugumizi, ni muhimu kumpa msaada wa kihisia na kumtia moyo. Usimkatishe tamaa au kumkosoa, badala yake msikilize kwa Utulivu na Uvumilivu (Mpe muda wa kumaliza kusema Sentensi anayoitamka bila kumkatisha)

Soma zaidi https://jamii.app/StutteringAwarenessDay24

#StutteringAwarenessDay #Stuttering #Stammering #ISAD2024 #JamiiForums

JamiiForums

23 Oct, 07:23


TAKWIMU: Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetangaza Wapiga Kura 31,282,331 wamejiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura wa Serikali za Mitaa 2024

Waziri Mohamed Mchengerwa amesema uchukuaji wa fomu unatarajiwa kuanza Oktoba 26 hadi Novemba 1, 2024 kuelekea Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024

Mdau zoezi la uandikishaji lilikuwaje Mtaani kwako?

Soma https://jamii.app/MchengerwaOkt21

#JamiiForums #Democracy #Governance #CivilRights #JFData

JamiiForums

23 Oct, 06:46


SIASA: Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, Amos Makalla amesema CCM ipo tayari kupokea aina yoyote ya matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024

Akizungumza Oktoba 22, 2024 wakati wa hafla ya kupokea taarifa ya zoezi la Uandikishaji wa Daftari la Wakazi kwa Mkoa wa Dar es Salaam, amesema “Tunaamini Uchaguzi huu utakuwa Huru na Haki, CCM itakuwa chama kiongozi cha kuheshimu matokeo yoyote"

Soma https://jamii.app/MakallaMitaa

#JamiiForums #JFDemokrasia #Governance #CivilRights #SocialJustice

JamiiForums

23 Oct, 04:47


#AfyaYaAkiliKazini #MentalHealthAwareness #PublicHealth #AmkaNaJF #JFMotivations #GoodMorning

JamiiForums

22 Oct, 18:59


Mshiriki wa Msimu wa 4 wa Shindano la Stories Of Change ameshauri kuwepo kwa Taasisi ambayo itakakusanya maoni ya Wananchi na kuyafikisha Serikalini ili kuongeza Ushirikishwaji wa Wananchi katika maamuzi mbalimbali yanayowahusu

Mshiriki huyu alisema ushirikishwaji wa Wananchi huboresha uhusiano kati ya Serikali na Wananchi, pia huongeza Uwajibikaji wa Viongozi na kudhibiti #Rushwa na ubadhirifu kwenye taifa

Una maoni gani juu ya hoja hii ya Mdau?

Kusoma andiko lote https://jamii.app/KushirikishaWananchiSoC

#JamiiForums #Governance #ServiceDelivery #JFHuduma #Accountability #KemeaRushwa #StoriesOfChange #Democracy

JamiiForums

22 Oct, 18:28


TEKNOLOJIA: Taasisi ya Kitaifa ya Afya na Ubora wa Huduma (NICE) ya Uingereza imesema teknolojia ya Akili Mnemba (AI), itasaidia kuongeza Uhakika wa Majibu ya Vipimo vya X-Ray kwakuwa ina uwezo wa kuona Uvunjikaji wa Mifupa zaidi ya inavyoonekana kwenye X-Ray

Kwa mujibu wa NICE, kwa sasa, uwezekano wa X-Ray kutoona Mivunjiko mingine zaidi kwa Mgonjwa huwa ni kati ya asilimia 3 hadi 10 kwenye vipimo vya sasa na hivyo kuongeza muda wa uchunguzi au kutopatikana kwa tiba stahili kwenye majeraha

Imeelezwa kuwa, teknolojia ya AI kwenye Vipimo vya X-Ray itapunguza muda wa kusubiri majibu kutoka kwa wataalamu wa Maabara, pamoja na kuondoa makosa ya kibinadamu yanayojitokeza wakati wa kusoma vipimo

Soma https://jamii.app/AIonXRays

#JamiiForums #TechWorld #DigitalWorld #Innovations #EmbracingTechnology

JamiiForums

22 Oct, 17:34


DAR: Siku chache baada ya Mdau wa JamiiForums.com kueleza kuwa Barabara inayopita katika Daraja la Mto Mzinga na Daraja lenyewe ni changamoto kutokana na uchakavu na kutoboreshwa kwa muda mrefu, hali inayochangia foleni, Serikali imeeleza mipango ya kuboresha miundombinu hiyo

Waziri wa Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema Barabara hiyo imekuwa na kero ya foleni, hivyo Serikali imeanza kwa ujenzi wa Daraja la Mzinga, pia ameelekeza ifanyike kama ilivyofanyika Kimara kwenda Kibaha ili kupunguza foleni

Soma https://jamii.app/MiundombinuMbagalaDar

#JamiiForums #Accountability #JamiiForums #ServiceDelivery

JamiiForums

22 Oct, 17:12


Position: Citizenship and Leadership Academy Content Developer

Organization: JamiiForums

RESPONSIBILITIES:
1). Develop audio and written training modules
2). Design promotional materials
3). Collaborate with project implementing partners
4). Conduct desk review
5). Conduct needs assessment

REQUIREMENTS:
1). Legally recognized in Tanzania to perform consultancy tasks.
2). Competence in both Kiswahili and English language
3). Master's degree in related field
10 years experience in undertaking gender and politics analysis

Send CVs of key personnel in the assignment, Samples of previous work and Contact information from 3 previous clients to: [email protected] before 29th October, 2024

For any inquiries please call (or WhatsApp) +255 743 440 000.

More details https://jamii.app/ContentDeveloperCLA

#JamiiForums #JFOpportunities

JamiiForums

22 Oct, 16:34


Position: Consultant Citizenship and Leadership Academy (CLA) Software Developer

Organization: JamiiForums

RESPONSIBILITIES:
1). Platform Development
2). Integration of Learning Tools
3). Ensuring Data Security
4). Testing and Quality Assurance
5). Training and Documentation
6). Support and Maintenance

REQUIREMENTS:
1). Proven experience in software development for e-learning platforms
2). Strong expertise in developing user-friendly and accessible platforms.
3). Experience with Learning Management Systems (LMS) and Content Management Systems (CMS).
4). Expertise in UI/UX design with a focus on interactive, mobile-friendly platforms.
5). Strong understanding of security and data privacy

Send your Portfolio, CVs of Key team players Technical and financial proposals to: [email protected] before 29th October, 2024

For any inquiries please call (or WhatsApp) +255 743 440 000.

More details https://jamii.app/SoftwareDeveloperCLA

#JamiiForums #JFOpportunities

JamiiForums

22 Oct, 16:07


Ban Ki-moon alitoa kauli hii wakati wa juhudi zake za kuhimiza usawa wa kijinsia na Haki za Wanawake alipokuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (2007-2016)

Kauli hii ilikuwa ni kusisitiza umuhimu wa kuleta usawa wa kijinsia kama sehemu ya msingi ya kufikia Amani na Maendeleo Endelevu, ikiwa ni sehemu ya kampeni za Umoja wa Mataifa za kukuza nafasi za Wanawake katika Uongozi na ushiriki katika Siasa

Umoja wa Mataifa umeendelea kuhimiza Serikali na Jamii kote duniani kuhakikisha Wanawake wanapata haki sawa na Wanaume katika nyanja zote za maisha, ikiwemo Siasa, Uchumi, na Kijamii

#JamiiForums #WomenInPolitics #WanawakeNaSiasa #WomenRights #JFWomen #Governance

JamiiForums

20 Oct, 16:53


KENYA: Aliyekuwa Naibu Rais, #RigathiGachagua, amedai alikutana na majaribio mawili ya kuuawa kwa njia ya sumu kabla ya kuondolewa katika nafasi ya Naibu Rais na kusema kuwa Rais #WilliamRuto amemsaliti

Akizungumza baada ya kutoka Hospitali ya Karen alipokuwa amelazwa amesema “Sihisi kama nipo salama, Agosti 30, kuna askari aliingia kwenye chumba changu akataka kukiwekea sumu Chakula changu, tuligundua hilo na kulikwepa."

Anaongeza "Septemba 3, nikiwa Nyeri, Maafisa wa NIS (Idara ya Kitaifa ya Ujasusi) walitaka kuweka sumu katika chakula, nikatoa taarifa hizo kwa NIS na kuelekeza Afisa aliyetumwa aondolewe. Baada ya majaribio ya kuniua kushindikana ndipo ikaja hoja ya kunivua cheo."

Soma https://jamii.app/GachaguaSpeech

#Governance #KenyanPolitics #JamiiForums

JamiiForums

20 Oct, 15:56


PWANI: Katibu Mwenezi wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA), Aisha Machano amesema alitekwa na kuteswa na baadaye kutupwa katika Pori la Kibiti na Watu wasiojulikana ambao pia wamempa vitisho mbalimbali

Aisha amezungumza na Wanahabari, leo Oktoba 20, 2024 na kueleza kuwa Watu hao walimvua nguo zote na kisha kumrekodi na kumwambia akijitokeza hadharani na kuelezea kilichotokea kwa Umma watasambaza picha hizo Mtandaoni pamoja na kumalizana naye

Jeshi la Polisi kupitia Msemaji wa Jeshi hilo, David Misime limesema uchunguzi wa tukio hilo unafanyika na kuwa watatoa majibu ya nini kilitokea dhidi ya Aisha na kina nani walihusika na tukio hilo na sababu zake ni zipi

Soma https://jamii.app/AishaMachano

#JFMatukio #JamiiForums

JamiiForums

20 Oct, 15:30


TANZIA: Msanii mkongwe wa Vichekesho Nchini Tanzania, Yusuph Kaimu maarufu kwa jina la #Pembe amefariki Dunia Mchana wa leo Oktoba 20, 2024 Jijini Dar es Salaam

Taarifa iliyotolewa na Msanii wa Filamu, Vincent Kigosi “Ray” imesema taratibu za msiba zitatolewa baadaye

Soma https://jamii.app/PembeRIP

#JamiiForums #JFMatukio

JamiiForums

20 Oct, 14:47


Tovuti ya #Businessinsider imetoa orodha ya Nchi 10 ambazo Serikali zake zina kiwango kidogo cha Madeni hadi kufikia katikati ya Mwaka 2024 na kueleza kuwa Wawekezaji wa Kigeni wanapendelea kuwekeza katika Nchi ambazo zina wastani wa chini wa madeni kulingana na Kiwango cha Pato la Taifa (GDP)

Soma https://jamii.app/Debt2024

#Economy #JFUchumi #Governance #Diplomacy #JamiiForums

JamiiForums

20 Oct, 13:47


MSUMBIJI: Watu wenye silaha wamesababisha vifo vya Wanasiasa wawili wa Chama cha Upinzani cha Podemos ambao ni Wakili Elvino Dias aliyekuwa Wakili wa Venâncio Mondlane aliyegombea Urais Wiki mbili zilizopita na Afisa mwingine wa upinzani, Paulo Guambe

Video zilizosambaa katika Mitandao ya Kijamii zinaonesha Gari aina ya BMW SUV likiwa na mashimo ya risasi katikati ya Barabara, nyingine inaonesha miili ya Watu wawili, mmoja ukiwa na Damu kwenye kifua

Tukio hilo limetokea wakati Wananchi wanasubiri matokeo ya Uchaguzi uliofanyika Oktoba 9, 2024 huku kukiwa na tuhuma nyingi za udanganyifu wa kura na kukandamiza upinzani

Soma https://jamii.app/MozambiquePolitics

#JamiiForums #Democracy #Governance

JamiiForums

20 Oct, 11:29


Wakili Boniface Mwabukusi ambaye ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) ameandika ujumbe kuhusu Utendaji wa Chama hicho kuwa hakiendeshwi kwa mihemko na chuki binafsi kupitia Ukurasa wake wa X (Twitter)

Soma https://jamii.app/NukuuMwambukusi

#JFNukuu #JamiiForums

JamiiForums

20 Oct, 10:43


MWANZA: Mdau wa JamiiForums.com anashauri Mamlaka zinazohusika na Maegesho ya Magari zitafute Mfumo tofauti wa kulipia maegesho, ikiwezekana Mtu awe ananunua kifurushi kisha akiegesha awe anakatwa kwa njia ya ‘ku-scan’ namba ya Gari husika

Anadai kuna Mazingira ya wenye Magari kutozwa kiasi ambacho hakiendani na uhalisia na mhusika anapotaka kufuatilia mlolongo ni mrefu, hivyo wengi wanaamua kuacha na kulipa madeni ambayo inawezekana wanakuwa wamebambikiwa

Soma https://jamii.app/MaegeshoKero

#JamiiForums #Accountability #JFHuduma #DigitalWorld #ServiceDelivery

JamiiForums

20 Oct, 09:04


Ushirikishwaji wa Jinsia zote (Wanawake na Wanaume) kwenye masuala ya Siasa na Uongozi unahakikisha Sera zinaundwa kwa mtazamo unaozingatia Jinsia

Masuala kama Haki za Uzazi, malipo sawa, Ukatili dhidi ya Wanawake, na malezi ya Familia yana uwezekano mkubwa wa kushughulikiwa panapokuwa na maoni ya uwiano kutoka kwenye mitazamo mbalimbali.

Soma https://jamii.app/GenderCollaboPolitics

#JamiiForums #WomenInPolitics #WanawakeNaSiasa #WomenRights #JFWomen #Governance

JamiiForums

20 Oct, 07:44


Mdau anadai amekuwa akikutana na changamoto ya kushindwa kubadilisha vyeti ili kuweka vilivyohakikiwa na Mwanasheria katika Tovuti ya Ajira Portal, hali ambayo inamfanya kukosa sifa ya kuchaguliwa kila anapoomba Ajira

Anadai amekuwa akipiga simu ya Huduma kwa Wateja lakini haipokelewi na mara nyingine anajulishwa Simu inatumika, amejaribu kuuliza kwa wenzake kadhaa nao wamekutana na changamoto hiyo pia

Anatoa wito Idara husika iangalie namna ya kusaidia Wateja, kama wanazidiwa basi watafute njia mbadala badala ya kuwa kero kama ilivyo sasa, anadai ni zaidi ya Mwezi Simu hazipokelewi

Soma https://jamii.app/AjiraPortal

#JamiiForums #Accountability #JFHuduma #DigitalWorld

JamiiForums

20 Oct, 06:09


PWANI: Katibu Mwenezi wa Baraza la Wanawake CHADEMA Taifa (BAWACHA), Aisha Machano anadaiwa kutekwa, kupigwa na kisha kutupwa porini akiwa Wilayani Kibiti

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na CHADEMA, kwasasa Aisha anapatiwa Matibabu akiwa kwenye Chumba cha Upasuaji huku tukio hilo likihusishwa na uchomaji wa vitenge katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2023 Mkoani Kilimanjaro.

Soma https://jamii.app/AishaAtekwaKibiti

#Democracy #WanawakeNaSiasa #JamiiForums #WomenInPolitics #Siasa #HumanRights

JamiiForums

20 Oct, 05:24


AFYA YA AKILI KAZINI: Inawezekana bado upo kazini muda huu, ni jambo zuri lakini kumbuka kuchukua mapumziko ya mara kwa mara ili Mwili na Akili yako visipate athari za Kiafya

Unaweza kupumzika kwa Kutembea kidogo, Kunyoosha Viungo vya Mwili (Stretching), Kusikiliza muziki na kunywa Maji ya kutosha.

#JamiiForums #AfyaYaAkiliKazini #MentalHealthAwareness #PublicHealth

JamiiForums

19 Oct, 17:37


Mdau wa Jukwaa la Urembo, Mitindo na Utanashati (Lifestyle) anasema katika suala la muonekano na urembo ni muhimu kuzingatia matumizi ya manukato au marashi kwa kiasi kwasababu kuna wakati huwa kero kwa wengine

Anadai baadhi ya Manukato au Marashi huweza kuwasababishia wengine madhara ikiwemo kupata mzio (allergy), Mafua Makali, Kupiga Chafya au maumivu ya Kichwa hivyo ni vema kupaka kwa kiasi manukato hayo

Una maoni gani hapa Mdau?

Soma https://jamii.app/MatumiziManukatoKero

#JamiiForums #JFLifeStyle