Últimas Postagens de Chakushangaza (@chakushangaza) no Telegram

Postagens do Canal Chakushangaza

Chakushangaza
Njoo▶tukujuze ▶tukushangaze ▶tukuelimishe ▶tuulishe ubongo wako madini

CHANNEL ILIANZISHWA RASMI MNAMO 11/06/2019
4,721 Inscritos
4,984 Fotos
168 Vídeos
Última Atualização 28.02.2025 22:03

Canais Semelhantes

Msomi Bora
11,552 Inscritos
NEW BONGO FLEVA MUSIC
5,728 Inscritos

O conteúdo mais recente compartilhado por Chakushangaza no Telegram


#CHAKUSHANGAZA
🤔Kutana na Balaz 75710 ambalo ndio Tipa kubwa kuliko yote duniani * lipo kwenye mgodi wa makaa ya mawe kule Belorussia, lina uwezo wa kubeba mchanga tan 450 kwa wakati mmoja na tairi lake moja lina uzito mkubwa kuliko uzito wa Tembo mkubwa

🤯Lina diesel tank lenye uwezo wa kujaza wese lita 5,600 na pia gari inatumia oil lita 548 na hydraulic fluid lita 1800

👆Bei ya hii giant tipper moja tu sokoni au kiwandani ni $ 6 million

Channel name @Chakushangaza
Channel link t.me/chakushangaza


SAMBAZA MARA NYINGI UWEZAVYO

#CHAKUSHANGAZA
BABA WA TAIFA
Alienda kucheki afya akalihutubia taifa kwamba Hali yake sio mbaya sana Kaenda anarudi kwenye jeneza kafariki

Channel name @Chakushangaza
Channel link t.me/Chakushangaza

#CHAKUSHANGAZA
Siku moja Mwalimu Nyerere alipita Nairobi akitokea Addis Ababa. Akaongea na waandishi wa habari.

Mmoja akamwuliza 'Mwalimu ni kweli unasaidia wanaotaka kumpindua Rais Moi?".

Mwalimu akamtazama yule mwandishi, kisha akamwuliza-: Ni kweli watu wanavyosema kuwa mimi natembea na mama yako?

Ile press conference iliishia hapo

#CHAKUSHANGAZA
Patrice Lumumba: Shujaa Asiye na Kaburi

Hofu iliyosababishwa na ukoloni bado inatesa akili na maisha yetu mpaka leo. Baada ya Mkutano wa Berlin wa mwaka 1884-1885, ardhi tajiri zaidi duniani, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DR Congo), ilitolewa kama mali binafsi kwa Mfalme Leopold II wa Ubelgiji. Umiliki huu haukuhusisha tu ardhi na rasilimali zake, bali pia watu waliokuwepo ndani yake, wakihesabiwa kama mali ya kifalme.

Wakati wa utawala wa Leopold II, ukandamizaji na ukatili vilifikia kiwango cha kutisha. Takribani nusu ya idadi ya watu wa Kongo, milioni 15, waliuawa kwa amri ya Leopold. Mauaji haya yalifanywa kwa lengo la kudhibiti idadi ya watu ili kuhakikisha upatikanaji wa faida kubwa zaidi kutoka kwa rasilimali za Kongo bila kulazimika kutumia kazi ya watu wengi ambao walionekana kama "mali binafsi."

Uhuru wa Kongo na Changamoto Zake

Baada ya zaidi ya karne moja ya ukoloni wa Ubelgiji, Kongo ilipata uhuru wake mwaka 1960. Hata hivyo, ukosefu wa elimu ulikuwa ni tatizo kubwa. Kufikia wakati wa uhuru, ni watu 11 tu kati ya milioni 15 waliokuwa wamehitimu shahada ya chuo kikuu. Utawala wa Ubelgiji ulizuia kwa makusudi upatikanaji wa elimu kwa wakazi wa Kongo, ili kuwahakikisha kuwa hawatakuwa na maarifa wala ujuzi wa kujinasua kutoka kwenye minyororo ya ukandamizaji.

Kwa hiyo, serikali mpya ya Kongo chini ya Waziri Mkuu wake wa kwanza, Patrice Lumumba, ililazimika kutegemea mfumo huo huo wa kikoloni kusimamia mambo muhimu ya kitaifa. Hali hii ilipelekea utegemezi mkubwa kwa wafanyakazi wa Kibelgiji katika sekta nyeti kama mawasiliano na ulinzi wa kijeshi, hali iliyohatarisha uhuru wa kweli wa nchi hiyo.

Patrice Lumumba: Mkombozi Aliyekandamizwa

Patrice Lumumba, kiongozi shupavu na mzalendo wa Kongo, alikuwa na maono makubwa ya kujenga taifa lenye haki na usawa. Hata hivyo, nia yake njema haikuwa siri kwa wakoloni wa Ubelgiji na washirika wao wa kimataifa waliopinga vikali juhudi zake za kuimarisha uhuru wa kweli wa Kongo.

Kwa sababu hiyo, Lumumba alikamatwa, kuteswa, na hatimaye kuuawa kinyama mwaka 1961. Mwili wake ulitoweshwa kabisa kwa kumwagwa katika tindikali, hatua iliyochukuliwa kuhakikisha kuwa hakuna kumbukumbu ya kiongozi huyo mkubwa. Hadi leo, Patrice Lumumba hana kaburi, lakini historia na urithi wake unaendelea kuishi.

Mnamo mwaka 2020, jino moja la Lumumba, lililookolewa na mmoja wa wauaji wake wa Kibelgiji, lilirudishwa rasmi kwa Kongo. Jino hilo linaendelea kuwa alama ya unyama aliokabiliana nao na ushahidi wa mapambano yake ya kudai uhuru wa watu wake.

Hitimisho

Urithi wa Patrice Lumumba ni ukumbusho wa maumivu ya ukoloni na changamoto za kujenga Afrika huru. Shujaa huyu asiyekuwa na kaburi anawakilisha ndoto za Waafrika wengi za kujikomboa kutokana na ukandamizaji na kujenga jamii huru yenye haki na usawa. Hata kama mwili wake ulitoweshwa, mawazo yake yataendelea kuishi mioyoni mwa wapigania haki kote barani Afrika.

Channel name @Chakushangaza
Channel link t.me/chakushangaza

SAMBAZA MARA NYINGI UWEZAVYO

Vitabu vipo hivi
Kwa Tsh 3000 tuu
Ni soft copy tuu, unatumiwa kwa telegram au WhatsApp

Buy ads: https://telega.io/c/chakushangaza

Enjoy our content? Advertise on this channel and reach a highly engaged audience! 👉🏻

It's easy with Telega.io. As the leading platform for native ads and integrations on Telegram, it provides user-friendly and efficient tools for quick and automated ad launches.

⚡️ Place your ad here in three simple steps:

1 Sign up

2 Top up the balance in a convenient way

3 Create your advertising post

If your ad aligns with our content, we’ll gladly publish it.

Start your promotion journey now!

https://t.me/sdgdgegsgbot?start=_tgr_5ioZpTs2ZTY0

Vitabu vipo hivi
Kwa Tsh 3000 tuu
Ni soft copy tuu, unatumiwa kwa telegram au WhatsApp

Vitabu vipo hivi
Kwa Tsh 3000 tuu
Ni soft copy tuu, unatumiwa kwa telegram au WhatsApp