CHA TATU, Alisema inabidi wajifanye kama watu wa manispaa ambao wako eneo hilo kwa ajili ya urekebishaji wa jengo na mandhari zima, genius aliona hii njia ni nzuri kwasababu itawalazimu wavae mask ambayo itawsaidi katika kuficha uhalisia wako.
CHA NNE, Alisema baada ya tukio tutasafirisha mali zetu kupitia madastibini ya taka ili kuwapoteza maboya mapolisi na walinzi wasiwashtukie wakiwa wanasepa zao na tutaweka haya madastibini upande ambao tutatorokea ili iwe rahisi kwetu.
CHA TANO, Alisema kuwa ni lazima tukodishe magari na tusitumie magari yetu binafsi kwani itakuja baade kutugharimu uchunguzi ukianza kufanyika na akasema pia kuwa READER kwakuwa yeye ndo alikuwa mzee kupita wote [alikuwa na miaka 76] basi atatumia usafiri wa jumuiya kufika eneo la tukio [nchini uingereza kuna kibali maalumu kinachowaruhusu wazee sana kama READER kutumia usafiri wa jumuiya bure kufikishwa mpaka aendapo kutokana na umri wake ndo maana MR. BASIL akataka READER atumie faida ya uzee wake]. CHA SITA, Alisema kuwa njia ya kupitia itakuwa lifti kwa mantiki ya kuwa yeye MR. BASIL alikuwaga katika kampuni moja nchini RUSSIA ya kuweka na kutengeneza lifti kwenye majengo makubwa, kwahiyo suala la namna ya kupenya ndani wamwachie yeye kwani bado hajamalizia vizuri kuandaa namana bora ya kupenya ila hatobadilisha njia penedekezwa ya lifti.
CHA SABA, Alisema kuwa njia ya kutokea itakuwa ni ule mlango wa tahadhari ambao unakuwepo kwa ajili ya tahadhari kama kutatokea maafa kama moto na hapo ndipo walipohifadhi yale madastibini ya uchafu kwa ajili ya kuhifadhia mali zao ili wakitoka waziingize humo na kuondoka zao.
CHA NANE, Alisema kuwa faida ya uzee wetu itatusaidia sana kuwaharibu kisaikolojia walinzi na mapolisi kwani huwezi kutegemea wazee wafanye uwizi na sisi indo tutawaonyesha kuwa tunaweza kushangaza dunia nzima, na hapo ndo MR. BASIL akawa amemaliza kufungua mpango wake wote kwa wenzake na kusikiliza maoni yao wao wanasemaje.
Wazee wote waliipitisha bila kipingamizi na kuona mpango unajitosheleza na hakuna haja ya kuongeza chochote zaidi ya kujiandaa na kazi inayowakabili mbele yao...!!! INAENDELEA...!!!