Canal Chakushangaza @chakushangaza en Telegram

Chakushangaza

Chakushangaza
Njoo▶tukujuze ▶tukushangaze ▶tukuelimishe ▶tuulishe ubongo wako madini

CHANNEL ILIANZISHWA RASMI MNAMO 11/06/2019
4,753 Suscriptores
4,941 Fotos
168 Videos
Última Actualización 20.02.2025 22:40

Canales Similares

Vinei TV
7,800 Suscriptores
Kilimo Biashara
3,952 Suscriptores
E-PLUS MEDIA
1,341 Suscriptores

Chakushangaza: Njia ya Elimu na Burudani

Chakushangaza ni channel ya kijamii iliyoanzishwa rasmi tarehe 11 Juni 2019. Imejikita katika kutoa elimu na burudani kwa njia ya kuvutia na inayoeleweka kwa urahisi. Channel hii inatambulika kwa kutoa maudhui yanayoweza kusaidia watu kutafakari na kuboresha maarifa yao katika masuala mbalimbali ya kijamii, kisayansi, na kiutamaduni. Kwa kutumia teknolojia ya kisasa, Chakushangaza inatoa masomo, maarifa, na habari zisizokwisha kwa watazamaji wake. Kwanza, channel hii ilianza kama jukwaa dogo la kuenezwa maarifa, lakini kwa haraka imekua kuwa moja ya vituo maarufu vya kujifunza nchini Tanzania na katika nchi nyingine za Kiafrika. Hii inatokana na uwezo wake wa kuchanganya burudani na maarifa, hivyo kuwafanya watu wawe na hamu ya kujifunza zaidi. Katika makala hii, tutachunguza zaidi kuhusu malengo na maudhui yanayotolewa na Chakushangaza, na jinsi inavyoweza kuboresha maisha ya watu.

Chakushangaza ina malengo gani?

Malengo makuu ya Chakushangaza ni kutoa elimu na maarifa kwa njia inayoweza kueleweka kwa urahisi. Channel hii inapenda kuhakikisha kuwa watu wanapata maudhui yanayowasaidia kukua kiakili na kiuchumi. Aidha, inachangia kuimarisha maarifa ya jamii kuhusu masuala mbalimbali, kutoka sayansi hadi sanaa.

Pamoja na hilo, Chakushangaza inataka kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa elimu na jinsi inavyoweza kubadilisha maisha ya mtu mmoja mmoja. Kwa kuanzisha majukwaa ya kujifunza, inawasaidia watu kujiendeleza kiakili na kujenga uwezo wa kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Je, Chakushangaza inatoa maudhui gani?

Chakushangaza inatoa maudhui mbalimbali ikiwemo elimu ya sayansi, teknolojia, utamaduni, na michezo. Ni channel inayotoa masomo, mihadhara, na mazungumzo kuhusu mada tofauti zinazowakabili watu wa kila rika. Kwa kutumia video, infographics, na maudhui mengine, inawapa watazamaji nafasi ya kujifunza kwa njia iliyo rahisi na ya kuvutia.

Aidha, inajihusisha na kutoa maarifa yanayohusiana na historia na tamaduni za Kiafrika, jambo ambalo linasaidia kuimarisha utambulisho wa kitamaduni na kuwaelezea watu kuhusu urithi wao. Hii ni muhimu katika dunia ya sasa ambayo inahitaji watu wajivunie na kuheshimu asili zao.

Ni vipi Chakushangaza inawasaidia watu katika maisha yao ya kila siku?

Chakushangaza inawasaidia watu katika maisha yao ya kila siku kwa kutoa maarifa na mawazo mapya yanayoweza kuboresha ufanisi wao. Kwa maudhui bora yanayotolewa, watazamaji wanaweza kujifunza mbinu za kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza, kama vile katika kazi zao au katika maisha ya kifamilia.

Pia, inawasaidia watu kujifunza kuhusu maendeleo ya kijamii na kiuchumi, hivyo kuwapa uwezo wa kufanya maamuzi bora. Kwa kufanya hivi, inaboresha uwezo wa watu kujiendesha katika jamii zao, na hivyo kuchangia katika maendeleo ya jumla ya taifa.

Je, ni njia gani zinazotumiwa na Chakushangaza kuwasilisha maudhui yake?

Chakushangaza inatumia njia mbalimbali kuwasilisha maudhui yake, ikiwa ni pamoja na video, podcast, na makala za maandiko. Hii inawapa watazamaji fursa ya kuchagua njia inayowafaa zaidi ya kupata maelezo. Video zinaweza kuwa na maudhui yaliyoandikwa isipokuwa pia mahojiano na wataalamu kwenye nyanja tofauti.

Aidha, matumizi ya mitandao ya kijamii yana nguvu kubwa katika kuwasilisha maudhui ya Chakushangaza. Kwa kutumia majukwaa kama Instagram, Facebook, na YouTube, inashirikisha watazamaji wake na kuimarisha uhusiano wa karibu nao. Hii husaidia kuimarisha uelewa na kupanua mtindo wa mawasiliano.

Chakushangaza inaathiri vipi maendeleo ya kijamii?

Chakushangaza ina athari kubwa kwenye maendeleo ya kijamii kwa kuimarisha elimu na uelewa wa watu kuhusu masuala mbalimbali. Kwa kutoa maudhui yanayohusiana na maendeleo ya kijamii, inachochea watu kujiunga na mipango ya maendeleo katika jamii zao, na hivyo kuleta mabadiliko chanya.

Aidha, inaongeza uelewa wa umuhimu wa ushirikiano kati ya watu katika kutekeleza miradi ya maendeleo. Kwa kutoa maarifa yanayohusiana na biashara, afya, na mazingira, inawezesha jamii kujenga mazingira bora ya kuishi na kufanya kazi kwa ushirikiano.

Canal de Telegram Chakushangaza

Chakushangaza ni jukwaa la Telegram ambalo limeundwa kwa lengo la kuelimisha na kushangaza watumiaji wake. Kupitia channel hii, utapata habari za kusisimua, maelezo ya kuvutia, na mawaidha yenye manufaa. Jukwaa hili lina lengo la kuwaelimisha watumiaji wake kwa njia ya kipekee na ya kusisimua.

Ikiwa unatafuta kujifunza vitu vipya, kushangazwa na maarifa mapya, basi Chakushangaza ni mahali pazuri kwako. Tumia fursa hii ya kipekee ya kujifunza na kuboresha maarifa yako kupitia channel hii.

Chakushangaza imeanzishwa rasmi tarehe 11/06/2019 na inakualika kujiunga leo ili uweze kufurahia mawaidha, mijadala ya kuelimisha, na maarifa mapya. Usikose fursa hii adimu ya kuendeleza elimu yako na kuelimishwa kwa njia ya kuvutia na ya kusisimua.

Últimas Publicaciones de Chakushangaza

Post image

(SEHEMU YA TATU)

Baaada ya wiki moja MR. BASIL akakutana na wazee wenzake na kuanza kufanya mipango yao, amabacho cha kwanza kabisa ilikuwa ni kupata sehemu ya jumuiya [public] amabayo watakuwa wanashauriana namna ya kufanya tukio zima na ndipo MR BASIL akachagua pub moja hivi itwayo THE CASTLE ambayo yeye aliipendekeza kwasababu moja kuu ya kutokuwepo kwa CCCTV CAMERA kwani alishajua hatari yake huko mbeleni ambayo tutakuja kuiona baadae.

Kwahiyo THE CASTLE ikawa ndo kijiwe chao cha mipango ya tukio zima, MR. BASIL akawa amekuja na mwanzo wa mpango mzima wa tukio tukianza na chaguo la kijiwe cha kusukia mipango na sehemu ya kuvamia ambayo ni HATTON GARDEN, katika kikao chao cha kwanza alitaka idadi ya watu iongezeke kufikia nane na ndipo ikaja kazi ya kutafuta watu wa kuongezewa ambao walihitajika watu wa tano zaidi.

Kazi ya kutafuta hao watu alipewa DANIEL JONES kwasababu ya uzoefu na historia yake ya huko nyuma akiwa kijana kwani alishawahi kuvamia benki na kuiba vitu pamoja na fedha taslimu vyenye thamani ya paundi miliioni moja na kweli akaanza kazi ya kutafuta ila alipewa sharti moja kuwa ahakikishe hao watu wawe wazee akimaanisha wasiwe chini ya umri wa miaka 50. Yeye MR. BASIL aliamini kwenye msemo wa ‘UTU UZIMA DAWA’. Mtu wa kwanza kabisa kupatikana alikuwa rafiki yake JONES aitwaye PERKINS ambaye huyu ndo waliiba wote vile vitu vyenye thamani ya paundi million moja wakati huo wa ujana wao na bwana PERKINS alipoambiwa mpango wa tukio aliona neema imekuja kwani naye alikuwa na hali mbaya kifedha na alikubali kwa moyo mmoja kuingia mzigoni.

Kupitia marafiki hawa wawili wakaweza kutafuta wengine wanne ili kukamilisha idadi ya watu watano wapya waliohitajika na ndipo wakapatikana wazee wengine wanne waliohusika katika tukio la zamani huko la kihistoria la kuteka treni ya kifalme iliyokuwa ikisafirisha fedha na kutokomea nazo [huu uwizi nao ulikuwa balaaa kwani akili kubwa ilitumika katika mpango mzima na ulinzi mkubwa wote wa kifalme ulisanda kwa hawa wezi kwani nafikiri ni uwizi namba mbili kwa ukubwa uingereza baada ya huu ninaouelezea leo, nisije nikamaliza uhondo bure nitaileta siku makala yake ya tukio zima]. INAENDELEA..!!

16 Feb, 05:22
353
Post image

(SEHEMU YA PILI)

Katika hao wezi nane kulikuwa na viongozi wakuu watatu waliokuwa wameanza na hili wazo la kuvamia HATTON GARDEN ambao ni BRIAN READER, DANIEL JONES na MR BASIL. Mnamo mwaka 2012 MR. BASIL ambaye huyu ndo mastermind wa tukio zima alikutana na wazee wenzake kama ilivyo kawaida kwa marafiki kukutana kupata unywaji na kubadilishana mawazo ya hapa na pale katika maongezi yao ya siku hiyo yalikuwa na utofauti kidogo na yale ya siku zote ni baada ya MR. BASIL kuwagusia wenzake wawili ambao ni BRIAN READER na DANIEL JONES kuwa amechoka na mambo ya kusubiri pensheni kila mwezi na bado alikuwa akilalamika kuwa haimtoshelezi mahitaji yake [huyu mzee alikuwa ni mtu wa totoz sana]. Baada ya malalamiko yale wenzake wakawa wanamcheka kwasababu wanamjua ugonjwa wake uko wapi ambao ni kupenda totoz sana ila MR BASIL hakuishia hapo aliendelea kuwaambia wenzake kuwa kwanini tusijiongeze kufanya chochote bila kujali umri wetu, ndipo bwana DANIEL JONES akamuuliza kwani wewe unatakaje...??? ndipo MR. BASIL akafunguka kuwa kwanini tusifanye uwizi wa akili ambao hatutatumia silaha wala kumjeruhi mtu.

Baada ya maelezo yale ya MR. BASIL akawa tayari ameshachukua attention ya wazee wenzake kwani nao wakaanza kumtolea macho wakisubiri kusikia kiendeleacho kuhusu maada yake aliyoileta kwani na wao kwa namna Fulani vyuma vilikuwa vimekaza na kuona kama fursa imejileta yenyewe.

MR.BASIL akaendele kuongea na kuwaambia kuwa mimi nina mpango kabambe na nimeamua kuwahusisha nyie marafiki zangu ili tufaidi wote kitakachopatikana katika mpango wetu wa tukio zima, ndipo akawaambia kuwa kesho yake wafanye hima waonane tena na atakuja na habari njema,

Kesho yake walikutana kama kawaida na akaanza kuwaelezea kuwa kwanini wasivamie bohari salama ya HATTON GARDEN....??? wenzake wakamwambia mbona umechagua sehemu yenye ulinzi mkali hivyo na ipo kati kati ya mji wa LONDON kwamba yeye haoni hatari ya kukamatwa , ndipo MR. BASIL akawaambia najua kabisa kuna ulinzi wa hatari ila nina maaana yangu kuchagua sehemu hiyo msiwe na wasiwasi nitawaelezea tukiwa kwenye mipango ya tukio.

Baaada ya wiki moja MR. BASIL akakutana na wazee wenzake na kuanza kufanya mipango yao. INAENDELEA...!!!


CHANNEL NAME @CHAKUSHANGAZA
CHANNEL LINK T.ME/CHAKUSHANGAZA

SAMBAZA MARA NYINGI UWEZAVYO

13 Feb, 02:36
530
Post image

(SEHEMU YA KWANZA)

UVUNJAJI NA UWIZI NDANI YA BOHARI SALAMA {SAFE DEPOSIT} YA HATTON GARDEN

Tumewahi kusikia, kuona au kusoma kuhusu uvunjaji na uwizi katika mabenki, mabohari salama au magari ya kubebea fedha katika sehemu mbalimbali duniani lakini wafanyaji matukio mara zote tumeshuhudia wakiwa ni vijana wanaotafuta pa kutokea katika maisha ila kwa makala yetu ya leo tunaenda kuona wazee ambao wengi wetu huwa tunawadharau na kuwaona wameshachoka kimwili na kiakili ila kwa wazee hawa al maarufu kwa jina la ‘THE GRANDPA GANG’ nafikiri wengi wetu watatubadilisha mtazamo wetu wa siku zote kwa wazee, kwani walichofanya ni zaidi ya kijana angefanya.
Mimi ningependa kuwaita wazee katika ubora wao kwa namna walivyochekecha akili zao na kuweza kustaajabisha dunia na kuweza kuweka rekodi ndani ya nchi ya uingereza katika jiji kubwa lenye ulinzi mkali la LONDON kwa kuweza kuiba katika bohari salama yenye ulinzi mkali vitu vyenye thamani kubwa katika historia ya nchi ya uingereza tangu dunia ianzishwe bila kutumia silaha yoyote zaidi ya akili kubwa na ueledi uliotukuka katika Nyanja za uwizi. Na hapa ndo msemo wa ‘uzee mwisho chalinze’ ndipo unapotimia kupitia wazee wetu hawa tutakaoenda kuwaona. Ni uwizi wa aina yake uliostaajabisha watu na sio kwasababu ya mali nyingi zilizoibiwa ila ni watu walioiba (wazee), njia iliyotumika kuiba na muda wa uwizi ulivyopangwa kwani ni moja ya uwizi uliotumia muda mrefu katika upangaji wake ambao ni miaka mitatu ambayo kiukweli inataka subira kwa wale wenye harakaharaka ila kwa hawa wazee walisimama na msemo "SUBIRA YAVUTA HERI". TUKIO ZIMA

Katika mpango wa tukio hili la uwizi lilijumuisha wazee wezi nane ambao walijikusanya na kuunda kundi lililoitwa ‘THE GRAND PA GANG’ likiwa na dhumuni kuu la kufanya uhalifu utakaocha historia nchini uingereza na kuongelewa duniani kote kutokana na ufundi utakaotumika kwenye uwizi wao.

Hawa wazee wanajulikana kwa majina ya KENNY COLLINS (75), DANIEL JONES (61), TERRY PERKINS (67), CARL WOOD (59), WILLIAM LINCOLN (60), HUGH DOYLE (50). BRIAN READER (76) na MR.BASIL [huyu nitakuja kumuelezea kwanini hajulikani jina lake halisi wala umri wake kama wenzake]. INAENDELEA...!!!

11 Feb, 11:07
524
Post image

#CHAKUSHANGAZA
ASILI YA JINA CHERAHANI YA KUSHONA NGUO.
Mwaka 1890 Charan Singh alikuwa mhindi wa kwanza kufika Kisumu nchini Kenya na kuanzia kutumia mashine hiyo ya kushona nguo, na Kwa kuwa jina lake aliitwa Charan, watu wakatumia jina lake hilo kuiita mashine hiyo kuwa ni CHERAHANI.
Ninaimani umeelimika.

03 Feb, 19:04
948