Mahusiano

@doktatyphmahusiano


Channel hii ni maalum kwaajili ya kupostia picha, videos, audio na media nyingine tuu.

Mahusiano

03 Jul, 15:11


Badala ya kulalamika ni kwanini mpenzi wako bado anamfikiria ex wake, hebu jiulize iwapo unatosha kwenye maisha yake😑

Mahusiano

03 Jul, 12:24


Kamwe, asitokee kima yoyote yule akawafanya mjione kama vile mme-miss kitu fulani ili penzi lenu likamilike, trust me ikiwa mnao utulivu, mnayo maelewano na mnasikilizana basi penzi lenu linajitosheleza hundred percent😑

Mahusiano

03 Jul, 12:23


Brothers and Sisters, popote mlipo dhihirisheni upendo wenu waziwazi, sifianeni kwa maneno mazuri na yaliyo mema, hiyo ndio njia sahihi ya wanafiki kuogopa penzi lenu.

Mahusiano

03 Jul, 12:23


Kama kuna changamoto kubwa ambayo kimsingi imewafelisha wengi linapokuja suala la MAHUSIANO basi ni hii tabia ya kulinganisha mahusiano yenu na ya wengine.

Brothers and Sisters, kama wewe na mpenzi wako hamna desturi ya kutoana out mara kwa mara, basi msijione kama hampendani pale ambapo wengine wanatoana out.

Mahusiano

03 Jul, 12:23


Siri ya MAHUSIANO au NDOA yeyote ile yenye furaha na amani hutegemea tuu vile jinsi ambavyo kila mmoja anavyowajibika kikamilifu kudhihirisha wazi kwa maneno na matendo MAPENZI aliyonayo kwa mwenza wake.

Mahusiano

02 Jul, 11:58


Ni vile tuu namna utakavyom-treat BABY WAKO ndiko kutamfanya aidha aone alichelewa sana kuwa na wewe au ndiko kutampa sababu ya kuendelea kumfikiria Ex wake.

Mahusiano

02 Jul, 11:58


Mahusiano yoyote yale yaliyojengwa kwenye misingi madhubuti ya URAFIKI nd'o mahusiano bora kabisa kwasababu yanategemea maelewano zaidi.

Hivyo basi, tengeneza mazingira ya mwenza wako kuwa rafiki yako, maana itakuwa rahisi hata kukueleza wasiwasi wake, ila sasa iwapo utakuwa mkosoaji anayekuogopa, kamwe hatakushirikisha hisia zake.

Mahusiano

02 Jul, 11:57


Kwakawaida mafanikio kwenye MAHUSIANO au NDOA yoyote ile huwa hayaji tu kwa kumpata mtu sahihi, bali wewe mwenyewe kuwa mtu sahihi pia.

Mahusiano

02 Jul, 11:57


Ladies, Mwanaume akikupenda kwa kigezo cha uzuri, basi jua tuu hataacha kupenda wengine labda wazuri waache kuzaliwa lakini Mwanaume akikupenda kwa kigezo cha tabia njema, basi Mwanaume huyo atakupenda wewe pekee kwa maisha yake yote.

Mahusiano

02 Jul, 11:57


Tengeneza utayari wa kumsikiliza mwenza wako pindi anapokuwa na siku iliyojaa changamoto na madhila lukuki.

Mkumbushe namna unavyothamini yote anayoyafanya kwaajili yako na familia yenu kwa ujumla.

Kwa hatua hizo maridhawa zitamthibitishia kuwa yote anayoyafanya yanaonekana na kumpa hamasa ya kuendelea kufanya mambo mazuri na kujituma zaidi.

Mahusiano

01 Jul, 10:42


Siyo kila wakati MAPENZI ni hadithi tamu na yenye kusisimua, zipo nyakati MAPENZI hubadilika hadi kuwa hadithi mbaya tena inayochukiza na kutisha😑

Mahusiano

01 Jul, 09:23


Ifike wakati sasa kila mtu ajifunze namna ya kuya-expeirence na kuyatafsiri mapenzi kulingana na uwezo wenu, yaani wewe na huyo mwenzi wako.

Kamwe msitake kufanya vitu vilivyo nje ya uwezo ili kuthibitisha kuwa mnapendana, kwasababu mnaweza mkapendana na msitoane out (japo ni muhimu kufanya hivyo) au mnaweza mkapendana na msipelekane photoshoot (na siyo lazima😑).

Mahusiano

01 Jul, 07:07


Kila Mwanaume anahitaji Mwanamke ambaye wakati wengine wanaangalia movie na kufuatilia udaku, yeye atapiga goti na kusemaπŸ‘‡

"Eeh Mungu Baba, nakuomba umbariki, umlinde na kumtunza MUME wangu kipenzi πŸ™".

Mahusiano

28 Jun, 08:17


Kwamujibu wa tafiti mbalimbali zilizofanywa na wataalam imebainika kuwa eti (eti lakini) Wanaume nd'o vinara wa ku-cheat kuliko Wanawake.

Jitetee kwamujibu wa experience na jinsia yako πŸ€”

Mahusiano

28 Jun, 07:45


Kimsingi ni kweli kabisa kwamba mavazi siyo tabia ila sasa nd'o yanayomtambulisha mtu kwa sauti na kwamsisitizo mkubwa hata kabla hajasema kuwa yeye ni nani.

Brothers and Sisters, vaeni vizuri(staha)

Mahusiano

28 Jun, 07:32


Dada, kama unatamani kumjua zaidi Mwanaume basi kuwa makini kwakuzingatia na ikiwezekana tilia mkazo zaidi kwenye maswali anayouliza kuliko majibu anayotoa, utanishukuru baadae πŸ™

Mahusiano

27 Jun, 15:53


Machozi mengi ya wadada niyakujitakia kwakutaka Wanaume wa mauzo ambao kimsingi hata huo uwezo tuu wa kujihudumia wao wenyewe hawana.

Hivyo basi ushauri wangu kwako wewe hapo mdada, tafuta MUME na si ilimradi tuu MWANAUME ili upunguze kuwaita watu MBWA😑

Najua kuna mtu anajiuliza, sasa kuna tofauti gani kati ya MUME na MWANAUME, well zipo nyingi ila mojawapo ni hii πŸ‘‡

MUME huwaza zaidi namna atakavyoyabeba majukumu yake kama MUME kwa MKE na kama BABA kwa familia.

MWANAUME ambaye unaweza pia kumuita MVULANA(shubaamiti😑) ni yule ambaye muda wote yeye huwaza zaidi KUDINYANA tuu.

Mahusiano

27 Jun, 14:04


Wengi wamepoteza watu wa thamani katika maisha yao kwasababu ya pupa za kimaamuzi, usiwe kama wao.

Amua kuwa tofauti, jaribu kuangalia kwa upana asili ya mabadiliko yake, pengine utagundua kitu au labda utagundua unapaswa kumsaidia na sio kumlalamikia wala kumtuhumu.

Mapenzi ni zaidi ya zile sweet moments, kuna wakati unatakiwa kumshika mkono mwenza wako na kumuonesha mwanga baada ya fikra zake kugubikwa na kiza.

Mahusiano

27 Jun, 10:18


Unapomuumiza mtu kisha ukamuona analia, kimsingi hapo usifikiri kuwa anakulilia wewe, lahasha bali kilio chake ni kwasababu anakuwa amepoteza muda wake wa thamani kwa jitu ambalo hata halikustahili kupewa huo muda, analia kwa kuchezewa hisia zake na namna alivyofanya mistake kujiwekeza kwako.

Mahusiano

27 Jun, 10:17


Abadani huwezi kufaidi pendo la mtu ikiwa bado unaangaza angaza kama yupo anayemzidi, hivyo ni vyema kama utaifundisha nafsi na akili yako kukinai na kuridhika, otherwise utakuwa mtumwa wa mwili mpaka kufa, hebu iongoze nafsi yako nayo ikakutii basi😑