UVUNJAJI NA UWIZI NDANI YA BOHARI SALAMA {SAFE DEPOSIT} YA HATTON GARDEN
Tumewahi kusikia, kuona au kusoma kuhusu uvunjaji na uwizi katika mabenki, mabohari salama au magari ya kubebea fedha katika sehemu mbalimbali duniani lakini wafanyaji matukio mara zote tumeshuhudia wakiwa ni vijana wanaotafuta pa kutokea katika maisha ila kwa makala yetu ya leo tunaenda kuona wazee ambao wengi wetu huwa tunawadharau na kuwaona wameshachoka kimwili na kiakili ila kwa wazee hawa al maarufu kwa jina la ‘THE GRANDPA GANG’ nafikiri wengi wetu watatubadilisha mtazamo wetu wa siku zote kwa wazee, kwani walichofanya ni zaidi ya kijana angefanya.
Mimi ningependa kuwaita wazee katika ubora wao kwa namna walivyochekecha akili zao na kuweza kustaajabisha dunia na kuweza kuweka rekodi ndani ya nchi ya uingereza katika jiji kubwa lenye ulinzi mkali la LONDON kwa kuweza kuiba katika bohari salama yenye ulinzi mkali vitu vyenye thamani kubwa katika historia ya nchi ya uingereza tangu dunia ianzishwe bila kutumia silaha yoyote zaidi ya akili kubwa na ueledi uliotukuka katika Nyanja za uwizi. Na hapa ndo msemo wa ‘uzee mwisho chalinze’ ndipo unapotimia kupitia wazee wetu hawa tutakaoenda kuwaona. Ni uwizi wa aina yake uliostaajabisha watu na sio kwasababu ya mali nyingi zilizoibiwa ila ni watu walioiba (wazee), njia iliyotumika kuiba na muda wa uwizi ulivyopangwa kwani ni moja ya uwizi uliotumia muda mrefu katika upangaji wake ambao ni miaka mitatu ambayo kiukweli inataka subira kwa wale wenye harakaharaka ila kwa hawa wazee walisimama na msemo "SUBIRA YAVUTA HERI". TUKIO ZIMA
Katika mpango wa tukio hili la uwizi lilijumuisha wazee wezi nane ambao walijikusanya na kuunda kundi lililoitwa ‘THE GRAND PA GANG’ likiwa na dhumuni kuu la kufanya uhalifu utakaocha historia nchini uingereza na kuongelewa duniani kote kutokana na ufundi utakaotumika kwenye uwizi wao.
Hawa wazee wanajulikana kwa majina ya KENNY COLLINS (75), DANIEL JONES (61), TERRY PERKINS (67), CARL WOOD (59), WILLIAM LINCOLN (60), HUGH DOYLE (50). BRIAN READER (76) na MR.BASIL [huyu nitakuja kumuelezea kwanini hajulikani jina lake halisi wala umri wake kama wenzake]. INAENDELEA...!!!