VIPEPERUSHI NA NUKUU ZA KIELIMU. @vipeperushivyakielimutz Channel on Telegram

VIPEPERUSHI NA NUKUU ZA KIELIMU.

@vipeperushivyakielimutz


HAPA UTAJIPATIA VIPEPERUSHI NA NUKUU ZA KIELIMU, KUTOKA KATIKA MANENO YA WANACHUONI WA KISALAFI NA MFANO WAKE AMBAZO ZIMETAFSIRIWA KATIKA LUGHA YA KISWAHILI.


•═JIUNGE NASI-JIFUNZE-TAWANYA KWA WENGINE═•

VIPEPERUSHI NA NUKUU ZA KIELIMU. (Swahili)

Je, unatafuta mahali pa kujifunza na kuelimika kwa maneno ya wanachuoni wa Kisalafi? Basi channel yetu ya Telegram 'vipeperushivyakielimutz' ni mahali sahihi kwako! Hapa utajipatia vipeperushi na nukuu za elimu, zilizotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili, kutoka kwa wanachuoni wa Kisalafi.nnChannel yetu inakuletea mafundisho muhimu ya kidini na kielimu, yaliyotolewa na wataalamu katika uwanja huo. Pamoja na vipeperushi na nukuu hizo, utapata ufahamu mpana kuhusu dini na maisha ya Kiislamu.nnTofauti na vyanzo vingine vya elimu, channel yetu inajitahidi kuleta tafsiri sahihi na fasaha kutoka kwa wanachuoni wenye ujuzi na taaluma katika dini ya Kiislamu. Hivyo, unaweza kuwa na uhakika kwamba mafundisho unayopata ni ya kuaminika na yanayokidhi viwango vya elimu.nnIli kujifunza zaidi, kujiunga na sisi ni rahisi sana! Bonyeza kitufe cha 'jiunge' na upate fursa ya kujifunza, kutafakari, na kushirikisha maarifa haya mazuri na wengine. Jiunge nasi leo na uwe sehemu ya jamii ya elimu na ufahamu wa dini yetu. Karibu kwa vipeperushi na nukuu za elimu ya Kisalafi!

VIPEPERUSHI NA NUKUU ZA KIELIMU.

20 Nov, 18:23


UMUHIMU WA SUBRA KATIKA KULINGANIA KATIKA NJIA YA ALLAH.


قال العلامة عبدلله بن صالح القصير رحمه الله تعالى :-

Amesema Mwanachuoni Shekh Abdullaah bin Swaaleh Al-Quswayr- Allah amrehemu:-



والداعي إلى الله يدعوا الناس غالبا إلى خلاف أهوائهم فلا بد أن يناله من سفهائهم والمستكبرين منهم من الأذى ما يحتاج مع٧ه إلى الصبر يبتغي به وجه الله تعالى ويستعين به على دعوته قال تعالى : ﴿ وَاسْتَعِينُوا بِالصَّبْرِ وَالصَّلاةِ إِنَّ اللَّهَ مَعَ الصَّابِرِينَ ﴾وفي الصحيح عن النبي ﷺ قال : ( واعلم أن النصر مع الصبر )..

"Na mwenye kulingania katika njia ya Allah mara nyingi anawalingania watu katika yale ambayo yako kinyume na matamanio yao. Basi hakuna budi kupata kutoka kwa wapumbavu wao na wenye kiburi miongoni mwao katika maudhi ambayo yatamuhitajia kusubiri huku akitafuta katika hilo uso wa Allah aliyekuwa juu, na atakemsaada kupitia hiyo -subra- juu ya ulinganizi wake amesema Allah:-

"Na takeni msaada kwa kusubiri na kuswali hakika ya Allah yuko pamoja na wenye kusubiri".
na katika swahihi kutoka kwa Mtume swala na salamu za Allah ziwe juu yake amesema "Na fahamu hakika ya nusra ipo pamoja na subra -kusubiri".


إفادة المسؤول عن ثلاثة الأصول ص :  (١٤)
.


Abuu Maysarah' Saalim

https://t.me/vipeperushivyakielimuTZ

VIPEPERUSHI NA NUKUU ZA KIELIMU.

17 Nov, 19:37


✍🏻✍🏻✍🏻KWA YALIYOJIRI KARIAKOO.

VIPEPERUSHI NA NUKUU ZA KIELIMU.

16 Nov, 04:32


🎞️NIKIWAZA UMAUTI AMANI INATOWEKA.🎞️


(Maandishi ya shairi kwa njia ya video)








https://t.me/duruuszakiswahiliTZ

⬇️⬇️⬇️⬇️⬇️⬇️

VIPEPERUSHI NA NUKUU ZA KIELIMU.

16 Nov, 04:32


🎙SAUTI YA SHAIRI


🌿NIKIWAZA UMAUTI, AMANI INATOWEKA.



LIMEANDIKWA NA NDUGU YETU:-

ABUU DARDAA IBN HASAN

🏔

VIPEPERUSHI NA NUKUU ZA KIELIMU.

16 Nov, 04:32


🌿SHAIRI;

NIKIWAZA UMAUTI, AMANI INATOWEKA.


MTUNZI;

ABUU DARDAA' IBN HASAN- ALLAH AMHIFADHI




بسم الله الرحمن الرحيم


1-Nikiwaza umauti, Amani inatoweka,

Mwili wakosa ribiti, Nabaki natetemeka,

Utapofika wakati, Wa uhai kunitoka,

Mapema akaripoti, Mtoaji malaika.






2-Hivi roho ikitoka, Nitahimili machungu!,

Shahada nitakumbuka, Iwe ni sahali kwangu,

Vipi nitasalimika, Akhera niwe na fungu!,

Giza nene la mashaka, Sioni ila ukungu.






3-Pale ikiletwa sanda, Nikafunikwa mwilini,

Na jeneza nikapanda, Kupelekwa kaburini,

Mama alivyonipenda, Atalia kwa huzuni,

Mwanangu ameshakwenda, Kakadiria Manani.






4-Hivi hizi nguo zangu, Nani atazichukua?,

Zitazidisha uchungu, Mama akizikagua,

Zilikua za mwanangu, Tena nilimfulia,

Imebaki kumbukumbu, Qadari imeshakua.






5-Wadogo wasofahamu, Uwezo wao mfupi,

Watauliza kwa hamu,Mama kaka yuko wapi?,

Embu mpigie simu, Mwambie aje na pipi,

Mama atatabasamu, Hajui ajibu vipi.






6-Watabaki kushangaa, Ndugu zangu kwenye dini,

Hapa jana tulikaa, Tukapitia mutuni,

Tukaswali na ishaa, Akalala kwa amani,

Kweli ikifika saa, Wakuzuia ni nani!.





7-Moyo wangu nakuasa, Tulizana ibadani,

Jiepushe na makosa, Yanapunguza imani,

Zisikughuri anasa, Pumbazo za duniani,

Akhera ukaitosa, Kwa vilivyokuwa duni.






8-Mola wangu nakuomba, Unifishe kwenye dini,

Kiama kikinikumba, Nami niwe kuliani,

Sina shida na majumba, Wala gari za thamani,

Kiburi na kujigamba, Mwisho wake duniani.




_______MWISHO_________

Channel yetu ya Darsa za Kiswahili kupitia Telegram
⬇️⬇️⬇️⬇️

https://t.me/duruuszakiswahiliTZ


جزاكم الله خيرا

VIPEPERUSHI NA NUKUU ZA KIELIMU.

15 Nov, 07:39


SHAIRI:-
TUMEMJUA KWA KHERI (ABUL FIDAAI)


بسم الله الرحمن الرحيم


01- Ugenini salafia, ndugu nilimsikia

Na kwa kheri maridhiya, si kwa shari za dunia,

Mzuri dini tabia, mpenzi wa salafia,

Tumemjua kwa kheri, Allah amlipe pepo.




02- Allah akawafikisha, wangu ndugu kumuona,

sio jambo la maisha, bali jambo la kusoma,

Elimu kuikitisha, Ibni bazi Dodoma,

Tumemjua kwa kheri, Allah amlipe pepo.




03- kwa Abu zaidi pengo, wa kuziba ajipange,

Kuyafikia malengo, kwa kituo cha Mwandege,

Mola alizibe pengo, Mwingine Mola mjenge,

Tumemjua kwa kheri, Allah amlipe pepo.




Abuu Zaynab' Qaasim- Lindi, Tanzania.
13 Jumaadal Uwlaa 1446, 15-11-2024.


https://t.me/vipeperushivyakielimuTZ

2,336

subscribers

3,388

photos

269

videos