ZIJUE HISTORIA @jifunzehistoria Channel on Telegram

ZIJUE HISTORIA

@jifunzehistoria


Jifunze na jikumbushe historia mbali mbali
Buy ads on:https://telega.io/c/jifunzehistoria

ZIJUE HISTORIA (Swahili)

Zijue Historia ni kituo cha Telegram kinachojikita katika kufunza na kukumbusha matukio mbalimbali ya kihistoria. Kupitia channel hii, utapata kujifunza kuhusu matukio muhimu yaliyotokea duniani na jinsi yalivyochangia katika mabadiliko ya jamii. Pia, utapata kufahamu historia ya tamaduni tofauti, vita vya zamani, watu maarufu, na mengi zaidi. Wote wanaopenda kuelimika kuhusu historia, kuanzia wanafunzi hadi wapenzi wa historia watapata manufaa katika channel hii. nnJifunze na Jikumbushe Historia inakuletea makala za kipekee zilizoandikwa kwa umakini mkubwa na wataalamu wa historia. Utapata kuona picha za kipekee, nyaraka za zamani, na video za kuvutia zinazohusiana na matukio ya kihistoria. Kupitia channel hii, utajifunza mambo mapya, kujenga uelewa wa historia, na kufahamu mizizi ya tamaduni zetu za leo. nnIkiwa unapenda kuelimika, kuelimisha wengine, au tu kupanua maarifa yako kuhusu historia, basi Zijue Historia ni mahali sahihi kwako. Jiunge nasi leo na uwe sehemu ya jamii yenye shauku ya historia. Pia, kwa wale wanaotaka kununua matangazo, fursa ya kufanya hivyo imefunguliwa kupitia kiungo: https://telega.io/c/jifunzehistoria

ZIJUE HISTORIA

07 Dec, 10:13


Hadi Mwaka 1989 Katika Nchi Nyingi Duniani Hasa Romania Kulikuwa na Sheria Mpya ya Ushuru Iliyoitwa Bachelor Tax. Ilikuwa Mwanaume Yeyote Aliyefikisha Umri wa Miaka 25 na Hajaoa Bado, Anaanza Kulipia Ushuru Serikalini Kila Baada ya Muda Fulani Mpaka Atakapooa.

Sheria hii ilianzia Roma tangu mwaka 1695, ikaanza kusambaa katika nchi nyingine kama Uingereza, Marekani, Poland na nchi nyingine nyingi ikiwemo South Africa pia. Mfano huko Poland waliita Bykowe kwamba mwanaume ukifika 25yrs hujaoa, unaanza kulipa kodi.

Nchi ya mwisho kuiondoa sheria hii ilikuwa ni Romania, na ni baada ya mapinduzi ya mwaka 1989 ndipo sheria hii ikafa baada ya kuanzishwa miaka mitatu nyuma, japo historia imeandika kuwa sheria hii ilikuwepo hadi mwaka 1999 huko Vastogirardi Italia.

ZIJUE HISTORIA

07 Dec, 10:10


Katika Kombe la Dunia la 1970, Mexico Anamfunga Ubelgiji na Kusonga Mbele Makundi. Akiwa Amelewa kwa Furaha Mlinzi wa Gereza la Chilpancing Mexico Akiwa na Bastola Akajikuta Anafungua Mageti na Kuwaachilia Wafungwa 142 Bila Kutarajia. Alisamehewa Kwakua Alikuwa Anashangilia Nchi Yake.

ZIJUE HISTORIA

05 Dec, 17:55


Mwaka 1960 Ufaransa (Mkoloni) Waliwafunga Wafungwa 150 Raia wa Algeria Kwenye Miti Waliyoisimika Katika Jangwa la Sahara Algeria, Kisha Wakalipua Bomu la Nyuklia Karibu kwa Majaribio ili Kujua ni Athari Kiasi Gani Zitapatikana Katika Miili Yao Kutokana na Mionzi Hatari ya Bomu Hilo. Watu 42,000 Walikufa kwa Mionzi Hiyo, Mabomu 17 ya Nyuklia Yalijaribiwa na Athari Zake Zinaendelea Mpaka Leo. Unaambiwa Hawa Wafungwa 150 Waligeuka Mishkaki.

ZIJUE HISTORIA

02 Dec, 11:18


Mwaka 2011 Kijana wa Miaka 17 Tyler Alred Raia wa Oklahoma US Alipata Ajali ya Gari Alilokuwa Anaendesha na Kuuwa Watu Wote Waliokuwamo Kasoro Yeye. Kwakuwa Hakuwa Amefikisha Miaka 21 Ili Kufungwa Jela, Jaji Mike Norman Alimhukumu Tyler Kuhudhulia Ibada Kanisani Kila Siku kwa Miaka 10.

ZIJUE HISTORIA

30 Nov, 17:17


Hii ni Sagada, nchini Phillipines, katika kijiji cha Igorot, kiliopo milima ya Province..Usichokijua ni kwamba katika kijiji hicho tokea karne ya 14, walikuwa na utamaduni, endapo mtu akifa hawaendi kumzika ardhini bali wana chukua Jeneza lake na kwenda , kulifungia katika milima hiyo ya province, likiwa lina bembea.

Katika imani watu wa kijiji hicho wana amini, kuwa kufunga jeneza hivyo juu, ni rahisi kwa marehemu/ wafu hao kuchukuliwa haraka na Mungu, kwasababu wana kuwa karibu nae.

Pia hawa amini, kuzika maiti ardhini, kwasababu wana amini chini ya ardhi kuna maji, hivyo kuwa weka wafu wao huko, nikuwafanya wateseke kutokana na maji huko ardhini.

Nakatika hiyo imani yao ya kuzifunga jeneza juu , hivyo endapo jeneza likadondoka chini, labda kwa kuoza au kamba kukatika, wao huamini mfu huyo tayari anakuwa amechukuliwa na Mungu.

ZIJUE HISTORIA

27 Nov, 17:21


Gazeti moja mnamo tarehe 18 mwezi wa 4 mwaka 1963 likiandika kua hapo baadae watu wataweza kubeba simu zao katika mifuko ya nguo zao aidha suriali ama sketi, ni takribani miaka 50+ sasa imetimia tangu andiko hilo liandikwe na sasa wote tunashuhudia kila mmoja anauwezo wa kubeba simu yake na kutembea nayo popote anapotaka.

ZIJUE HISTORIA

18 Nov, 04:55


Mwaka 2018 Polisi Mjini Piauí, Brazil Ilibidi Wamtie Mbaroni Kasuku Baada ya Kugundua Kuwa Alikuwa Amefundishwa na Mmiliki Wake Kuita "Mum, the Police" Kila Anapoona Police Wanakuja Karibu na Mtaa Waishio ili Kumshtua Mmiliki Huyo. Jamaa Huyo Alikuwa ni Mfanyabiashara wa Dawa za Kulevya.

ZIJUE HISTORIA

09 Nov, 12:07


Live stream started

ZIJUE HISTORIA

09 Nov, 10:22


Kijiji cha Mbati Wilaya ya Tunduru Ruvuma kimebarikiwa msitu wenye magogo yanayogeuka mawe, hii imesababisha kutembelewa na wageni kutoka ndani na nje ya Nchi.

Mratibu wa Utalii Kanda ya Kusini ambaye pia ni Afisa Msaidizi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Tunduru Debora Mwakanosya amesema miti inayogeuka mawe (Miti mawe) ni jamii ya miti ya mitetereka ambayo Duniani inapatikana nchi mbili ambazo ni Marekani na Tanzania na ina uwezo wa kudumu zaidi ya miaka 120.

Amesema mti huo ukiuona juu unakuwa ni mti wa kawaida lakini unageuka jiwe kutokana na mfumo wa asili ambao Mungu ameuumba “hata hivyo ipo katika hatari kubwa ya kutoweka kutokana  na Watu wengi kuikata kwa matumizi mbalimbali"

ZIJUE HISTORIA

04 Nov, 13:56


Mekatilili wa Menza alikuwa kiongozi jasiri wa kabila la Wadigo, jamii ya Wagiriama, nchini Kenya. Anajulikana kwa kumcharaza makofi afisa wa Kiingereza aliyekuwa akijaribu kuingiza tamaduni za kigeni kwenye jamii yake. Aliongoza watu wake katika kupinga uvamizi wa Waingereza, ambao walikuwa wakipora ardhi na kutoza kodi kwa nguvu, pamoja na kupiga marufuku shughuli zao za jadi.

Mekatilili alitumia ngoma ya 'Kidufu' kukusanya watu na aliwaahidi kwamba watapigana hadi mwisho wa maisha yao dhidi ya ukandamizaji. Alikamatwa na kuwekwa kizuizini kwa miaka mitano, lakini alikomboa na kuendeleza harakati zake za mapinduzi. Alitembea kilomita 700 hadi Kilifi kuimarisha mapambano yake.

Akiwa na umri wa miaka 60, alianzisha harakati za waziwazi kupinga utawala wa Kiingereza. Alikamatwa tena mnamo Agosti 16, 1914, lakini alitoroka Kismayu, Somalia, na kuendelea na mapambano yake. Mekatilili anasimama kama mfano wa ujasiri na upinzani dhidi ya ukandamizaji.

ZIJUE HISTORIA

27 Oct, 11:10


King Mswati wa eSwatini.

Ni Mfalme aliyejipatia umaarufu Barani Afrika na duniani kwa ujumla hasa kutokana na utamaduni wake wa kuoa wake wengi.

Mfalme huyo wa taifa la zamani la Swaziland ambalo alilibadilisha jina kulibatiza jina jipya la Ufalme wa eSwatini. Alitoa tamko hilo mwaka 2018 wakati wa maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa alipokuwa akitimiza miaka 50 ya kuzaliwa.

eSwatini, lina maana ya ardhi ya Waswaz na lilitumiwa rasmi na Mfalme Mswati wa tatu kwa miaka mingi.

Mfalme huyu amejitwalia umaarufu kwa kuoa wake wake 15, ambapo wake zake wawili waliamua kumwacha na wawili wengine walifariki dunia, kwa sasa King Mswati III anadaiwa kuwa na watoto 34 na wajukuu 4.

Katika mila na desturi za Swaziland (eSwatini) Mfalme anahitajika kuchagua miongoni mwa halaiki ya wasichana ‘vipusa’ walio bikra kila mwaka katika ngoma maarufu ya ‘Reed Dance’ inayoitwa Umhlanga.

ZIJUE HISTORIA

22 Oct, 16:49


CHIPS ILIGUNDULIWA NA MTU MWEUSI.

UNAAMBIWA: Chips za viazi zilianza kutengenezwa rasmi Mwaka 1853 baada ya Mmarekani mweusi George Speck maarufu Crum (Mpishi) kupata hasira kisa Wateja wake kumlaumu kuwa anawawekea viazi vyenye mapande makubwamakubwa.

Alipoona Wateja wanamkera akaamua kuwakomoa kwa kukata vipande vidogovidogo sana lakini ndio kwanza Wateja wakavipenda, baadaye vikaanza kuchanganywa na mayai na kutengenezwa kiepe na sasa Crum ndio Legend na Baba wa Chips duniani.

ZIJUE HISTORIA

16 Oct, 17:11


Hili ndiyo jengo kubwa duniani la kupangisha,jengo hili lipo China huko Hangzhou.

Unaambiwa kwenye hili jengo kuna wapangaji elfu 30 pia kuna kituo cha polisi humo ndani, mkizinguana mnapelekana polisi humo humo ndani.

Sasa imagine kibongo bongo hapa mnakuwa wapangaji watano tu lakini maelewano hakuna kila siku ugomvi vipi ukija kukaa hapa.

ZIJUE HISTORIA

11 Oct, 09:59


Nchini Norway hakuna ambaye anaweza kuficha siri ya kipato chake kwasababu kila Raia kipato na pesa anayoingiza kwa mwaka huwekwa hadharani mtandaoni na kila Mtu anaweza kupita na kuona, Wafanyakazi wanaweza kuona kiwango cha pesa wanachoingiza Wafanyakazi wenzao na hata jirani yako anaweza kutazama akaona unachoingiza kwa mwaka.

Mwezi wa kumi kila mwaka kiwango cha kodi ambacho Mtu hulipa kwa Mamlaka wa Mapato kuwekwa mtandaoni kikionesha na kipato anachoingiza, Unaambiwa kama utakuwa una maswali kwamba jirani yako ana pesa za kutosha kumiliki Gari kali anayotembelea?, haupati shida unaingia tu online na kupitia mkeka wa hesabu zake.

Kwa sasa ukichungulia jirani yako anatumiwa meseji kuwa ulipita kuchungulia hesabu zake, ila Waandishi wa habari wamepewa uhuru wa kuchungulia bila mwenye taarifa za pesa zake kuambiwa.

ZIJUE HISTORIA

07 Oct, 09:14


IJUE STORY YA BIBI SARA.

Wakati Sara Baartman mwenye umri wa miaka 20 alipopanda mashua ambayo ingemchukua kutoka Cape Town hadi London mnamo 1810,
Alijua kwamba hangeweza kuona tena nyumbani kwao.

Hata aliposimama pembeni mwa mashua na kuangalia nchi yake ikitoweka nyuma yake, Sara hakujua kuwa Hile ndio Ilikuwa picha ya mwisho ya kuiona ardhi ya baba zake.

Bibi Sara hakujua kuwa ULE ndio ulikuwa mwanzo wa yeye kufanyika onyesho la picha za utupu na uonyeshwaji wa jinsia ya wanawake weusi Kwa zaidi ya miaka mia moja mbeleni.

MAISHA NA NYAKATI ZA SARA BAARTMAN ni hadithi ya kusikitisha sana ya mwanamke huyu wa Khoi Khoi ambaye alichukuliwa kutoka Afrika Kusini, na kisha kuonyeshwa kama kituko kote Uingereza.

Picha zake zilipewa jina la "The Hottentot Venus" Neno Hottentot ni neno la Kiholanzi.

Hottentot Venus” ilikuwa jina lililo tolewa kwa msururu wa wanawake weusi walio onyeshwa katika maonyesho ya udadisi wa watu tofauti na wazungu yaliyochochea ngono nchini Uingereza na Ufaransa mwanzoni mwa karne ya kumi na tisa.

zamani neno Hilo lilitumika kuwadharau watu wa kale wa Khoe sun wa Afrika Kusini.

Mnamo 1814 Sara alipelekwa Ufaransa, na kuwa kitu cha utafiti wa kisayansi na matibabu ambao uliunda msingi wa maoni ya wazungu juu ya ujinsia wa wanawake weusi.

Alikufa mwaka uliofuata.

Lakini hata baada ya kifo chake, Sara Baartman alibaki kuwa kitu cha uchunguzi wa kisayansi wa wakoloni.

Kwa jina la Sayansi, walitengeneza plasta ya mwili wake kisha wakatoa SKELETON yake baada ya kukata UBONGO wake na UKE, wakaichuna ngozi yake na kuiweka kwenye chupa kwenye jumba la makumbusho la Musee de l’Homme huko Paris.

Sehemu zake za siri na sehemu nyingine za mwili zilionyeshwa hadharani kwa miaka 160 hadi hatimaye zilipoondolewa kwenye kuonekana mwaka wa 1974. 😭😭😭😭😭

Mnamo 1994, wakati huo Rais Nelson Mandela aliomba mabaki yake yaletwe nyumbani.

Mnamo Januari 2002, mabaki ya Baartman hatimaye yalirudishwa Cape Town ili kuzikwa Kwa heshima ipasavyo.

ZIJUE HISTORIA

06 Oct, 07:28


*Wiki mbili(siku14)* HALOTEL
Gb7-8000
Gb8-9000
Gb10-10000
*Halotel mwezi*
Gb13-12000
Gb15-14000
Gb20-18,000
Gb22-20,000
Gb25-23,000
Gb30-27000
Gb38-35,000
Gb45-40,000
Gb50-45000
GB60-50,000

NB: HUDUMA NI UHAKIKA 100% MALIPO NI KABLA YA KAZI

Kwa mawasiliano MCHEKI hapa 👇👇👇
https://wa.me/255628314490

ZIJUE HISTORIA

02 Oct, 18:36


Nyaburebeka: Jiwe Linalocheza Kisiwa cha Ukerewe

Nyaburebeka ni jiwe kubwa linalopatikana Kaskazini Magharibi mwa Tanzania, katika kisiwa cha Ukerewe, tarafa ya Ukara. Jiwe hili lina uwezo wa kucheza, ambapo mtaalamu wa kulichezesha anahitaji kuligusa au kuliimbia. Ingawa lina uzito wa zaidi ya tani 20, Mzee Kakuru Makorokoro na familia yake wana uwezo wa kulisukuma.

Mzee Kakuru, kiongozi wa ukoo wa Makorokoro, anasema jiwe hili limekuwepo kwa karne nyingi na linahifadhi mila na tamaduni za familia yao. Wageni wanapaswa kuvua viatu wanapolitembelea kutokana na nyayo za binadamu zilizopo kwenye jiwe.

Kisiwa cha Ukara kina vivutio vingine vya ajabu, ikiwa ni pamoja na njia fupi ya kufika kwa jiwe hilo ambayo wanawake hawaruhusiwi kutumia, na sehemu ya maji ya ziwa ambayo hayachemki hata ikichemshwa. Pia kuna mti ambao jani lake likiangukia kwenye ziwa linakuwa mamba.

ZIJUE HISTORIA

29 Sep, 16:17


Msichana huyu anaitwa Nuntita Khampiranon, ni mwanamuziki maarufu raia wa Thailand, mwaka 2011 alishiriki katika mashindano ya kusaka vipaji ya Thailand's Got Talent, alionyesha uwezo mkubwa sana wa  kuimba kwa kufanya duet na yeye mwenyewe! Ana sauti ya kike pamoja na sauti ya kiume.

Kipaji chake kilikuwa cha kushangaza sana katika mashindano hayo hivi kwamba alishinda mashindano hayo kwa mwaka huo. Baadaye ilibainika kuwa Nuntita ni kijana wa kiume aliyebadili jinsia na kuwa wa kike.

Baada ya Nuntita mwenye umri wa miaka 38 sasa kushinda mashindano hayo makubwa nchini humo na kubainika kuwa ni transgender, ndipo nyota yake ikang'aa maradufu na moaka sasa ni mwanamuziki mkubwa nchini humo akitumia jina la usanii la Bell.

Nchini Thailand ni ruksa kisheria mtu kubadilisha jinsia aitakayo.

ZIJUE HISTORIA

29 Sep, 14:59


Anaitwa Mary Ann Bevan Kutoka London UK, Mwanamke Mbaya Zaidi Duniani. Baada ya Mumewe Thomas Kufariki Mwaka 1914 Ilibidi Mary Akubali Kudharirishwa na Kuchekwa Katika Matamasha Mbalimbali ili Apate Fedha Watoto Wake Wanne Wapate Mahitaji.
Alifariki Mwaka 1933 (59). Heshima Kwake.

ZIJUE HISTORIA

29 Sep, 13:31


Kabla ya Kupigwa Marufuku Mwaka 1920, Gereza la Urga Huko Mongolia Ndio Lilikuwa Gereza Hatari Zaidi Duniani. Mfungwa Alikuwa Anafungwa Kwanza Kwenye Box Mfano wa Jeneza Ndipo Anaingizwa Jela. Ukiingia Unakutana na Mabox Yenye Wafungwa Ndani. Liliitwa Box la Kifo.

ZIJUE HISTORIA

25 Sep, 09:04


December 21, 2018 mtandao wa The Sun wa Uingereza uliripoti taarifa ya mwanaume Khurum Shazada wa umri wa miaka 23 raia wa Birmingham nchini humo aliyekamatwa akifanya mapenzi na maiti saa chache baada ya kuzikwa.

Hili ni tatizo la kiafya linaloitwa Necrophilia ambapo mtu anakua anatamani kushiriki tendo la ndoa na watu waliokufa ambapo hadi Shazada anashikiriwa alikuwa ameshafanya mapenzi na zaidi ya maiti 100.

"Ninalala juu yao na kisha kuvuta suruali yangu," aliiambua mahakama.

Mkewe alikiri kuwa ni kwa miezi mingi mumewe huyo alikuwa akirudi usiku nyumbani huku akinuka pombe pamoja na mnuko wa mtu aliyetoka kufanya mapenzi.

Tabia yake hiyo alisema alianza kuwa nayo tangu mwaka 2012 baada ya kuziingilia kingono maiti mbili za wanawake wajawazito huku akisema kuwa amewahi muingilia mwanamke aliyekuwa kapoteza fahamu akidhania alikuwa kafariki.

ZIJUE HISTORIA

24 Sep, 09:48


【EU_Exchange】AI-GPT company recruits HR managers

Only one mobile phone is needed, work from home

Age 25 and above

Monthly salary over $1,800

Main responsibilities:

1. Help the company recruit personnel

2. Promote the company's AI smart products

3. Successfully join the company and receive a $30+$20 reward

4. Online customer service:https://chatlink.wchatlink.com/widget/standalone.html?eid=f55ff528d770d699c2cc389645f3577a&language=en

ZIJUE HISTORIA

23 Sep, 12:16


Ningependa kuchukua fursa hii kuwashukuru nyote kwa kuunga mkono channel yetu ya "Zijue Historia" kwenye Telegram. Leo tumefikisha wanachama 8000! 🎉

Ni furaha kubwa kuona jamii yetu ikikua na watu wengi wenye hamu ya kujifunza na kubadilishana maarifa. Kila mmoja wenu ni muhimu sana katika safari hii, na bila nyinyi, mafanikio haya yangekuwa magumu kufikiwa.

Tunaahidi kuendelea kutoa maudhui bora na yenye thamani ili tuendelee kujifunza pamoja. Tafadhali endeleeni kushiriki na kuleta marafiki zaidi ili tuweze kufikia malengo makubwa zaidi!

Asanteni sana kwa kuwa sehemu ya familia ya "Zijue Historia"! 🙏❤️

#ZijueHistoria #Shukrani #TelegramFamily #Subscribers8000

ZIJUE HISTORIA

19 Sep, 17:39


Meli ya Octavius ilipatikana Oktoba 11, 1775 baharini huko Uingereza Ikiwa na wafanyikazi 28 waliokufa wakiwa wamegandishwa kwa barafu ndani humo, wote walikuwa wameganda kwa barafu.

Mwili wa nahodha ulikutwa bado uko kwenye meza huku kalamu ikiwa mkononi. Katika kabati la pembeni yake pia kulikuwa na miili ya mwanamke na mvulana aliyefunikwa na blanketi, wote wamekufa na wameganda.

Haya yote yalikuwa ni mshangao kwani kwa mara ya mwisho meli hiyo ilionekana Novemba 11, 1762 kabla ya baadaye kupotea kimaajabu majini, hii ilimaanisha kuwa meli ilikuwa imepotea kwa miaka 13.

Wachunguzi wa mambo walisema kuwa inawezekana meli ilipita katika eneo la bahari lenye barafu kali ndio maana watu wote 28 walionekana kuganda, lakini swali ni je, kwanini haikuonekana kwa miaka hiyo yote 13?.

ZIJUE HISTORIA

15 Sep, 05:04


Enjoy our content? Advertise on this channel and reach a highly engaged audience! 👉🏻

It's easy with Telega.io. As the leading platform for native ads and integrations on Telegram, it provides user-friendly and efficient tools for quick and automated ad launches.

⚡️ Place your ad here in three simple steps:

1 Sign up

2 Top up the balance in a convenient way

3 Create your advertising post

If your ad aligns with our content, we’ll gladly publish it.

Start your promotion journey now!