Ben Kukufarm @benkukufarm Channel on Telegram

Ben Kukufarm

@benkukufarm


Welcome

Ben Kukufarm (English)

Are you a fan of agriculture, sustainability, and eco-friendly practices? Look no further than Ben Kukufarm! This Telegram channel is dedicated to all things related to farming, gardening, and living a more sustainable lifestyle. Whether you're a seasoned farmer or just starting out with a small garden on your balcony, Ben Kukufarm has something for everyone. Join our community of like-minded individuals who are passionate about growing their own food, reducing waste, and caring for the environment

Who is Ben Kukufarm? Ben Kukufarm is a group of dedicated individuals who are committed to sharing knowledge, tips, and tricks for successful farming and gardening. From organic farming techniques to DIY projects for your garden, Ben Kukufarm offers a wealth of information to help you cultivate a green thumb

What is Ben Kukufarm? Ben Kukufarm is a Telegram channel where you can connect with fellow farmers, gardeners, and sustainability enthusiasts. We share informative articles, helpful resources, and engage in discussions about all things farming and gardening. Whether you have questions about composting, pest control, or seed starting, the Ben Kukufarm community is here to support you on your journey to a more sustainable lifestyle

Welcome to Ben Kukufarm! Join us today and start growing your knowledge and your garden with our friendly community of farmers and gardeners. Let's work together towards a greener, more sustainable future for all.

Ben Kukufarm

28 Jan, 05:02


VIDEO MPYA
Jifunze kupitia video hii ambayo ni muendelezo was vipindi vyetu kuhusu dawa za asili za kutibu kuku
Katika video hii utajifunza
1.nagonjwa ya kuku yanayotibika kwa kutumia kitunguu swaumu
2. Jinsi ya kuandaa kitunguu swaumu kuwa dawa ya asili ya kutibu kuku
3.jinsi ya kutumia dawa hii itokanayo na kunguu swaumu kutibu kuku

Subscribe katika YouTube channel hii na angalia video hii naamini utajifunza
LINK
๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡
https://youtu.be/Y3gVOyljHwM

Ben Kukufarm

20 Jan, 02:42


https://youtu.be/P645isnigsE

Ben Kukufarm

18 Jan, 05:43


MUONGOZO WA UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA (BROILER)
Katika video hii utajifunza jinsi ya kutunza kuku wa nyama ili ukiuza upate faida angalia video Hadi mwisho usisahau ku subscribe kwenye YouTube channel yenye video hii utajifunza zaidi
๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ๐Ÿ‘‡๐Ÿฝ
https://youtu.be/QFMAxdYtcz4?si=5Jvz_DOMV2x3972k

Ben Kukufarm

17 Jan, 02:31


VIDEO mpya jinsi ya kutibu MAGONJWA 5 hatari kwa kuku kwa kutumia majani ya mwarobaini na jinsi ya kuandaa dawa ingia hapa kutazama
๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

https://youtu.be/3UpEcbjtUfY

Ben Kukufarm

15 Jan, 17:59


๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“
๐Ÿ’ฆJE WAJUA...???๐Ÿ’ฆ
๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“

๐Ÿ—ฃ๏ธFahamu Kuhusu Aina Za Kuku Ili Utakapochukua Maamuzi Ya Kuanza Ufugaji Uwe Na Uwezo Wa Kujielezea Kuwa Nataka Aina Fulani Ya Vifaranga Kutokana Na Malengo Yako Tunajua Watu Wengi Sana Kujua Aina Za Kuku Ni Tatizo Kwao Ila Usijali Leo Tutakuekezea Vizuri Kabisa Ondoa Shaka Ayaah Twende...

๐Ÿง‘โ€๐ŸซNikukumbushe Kujiunga Na Page Yetu Kama Bado Haujajiunga Nasi Kwa Kubonyeza Hapa Chicken Notifications Kisha Tufollow Kama Tayari Ushajiunga Usisahau Kulike Na Kushare Asante Sana Kwa Support Yako...

๐Ÿฆป๐ŸฆปTunajua Mpaka Sasa Umeshasikia Majina Mengi Ya Kuku Sijui Kroiler Mara Kenbro Mara Malawi Mara Isa Brown Mara Hyline Brown Mara Saso Mara Broiler N.K Ila Ukiulizwa Kuku Fulani Ndio Kuku Wa Namna Gani Wengi Wetu Hatuna Majibu Utasikia Tu Mi Nafuga Tu Au Mimi Nauza Vifaranga Tu Ila Siwajui Kivileee Ila Ni Kuku Wazuri Sana Kwa Kutaga๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚...

๐Ÿ‹๏ธ๐Ÿ‹๏ธUnakwama Wapi Kujua Kuku Unaofuga Bhana Ayaah Tusichoshane Kuna Aina Kuu Mbili 2๏ธโƒฃ Za Kuku Ambazo Ni...๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

๐Ÿ“Kuku Wa Kienyeji...

๐Ÿ”Kuku Wa Kisasa...

1๏ธโƒฃ KUKU WA KIENYEJI ๐Ÿ“...

โœ๏ธHawa Ni Kuku Wa Asili Kabisa Ambao Mbegu Yao Ni Asili Hawajachanganywa Na Mbegu Yoyote Ya Kisasa Katika Kizazi Chao Kwahiyo Wanatabia Zote Za Kuku Wa Asili Kama Vile...๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

๐Ÿ‘‰Wanasifa Ya Kuatamia...

๐Ÿ‘‰Wanakua Taratibu Sana...

๐Ÿ‘‰Wanataga Mayai Machache Kwa Mwaka...

๐Ÿ‘‰Wanauwezo Wa Kujitafutia Chakula Wenyewe...

๐Ÿ‘‰ Wanastahimili Magonjwa Kuliko Kuku Wengine...

...Na Sifa Zingine Nyingi Tu Ila Kwa Leo Hizi Chache Zinakutosha...

2๏ธโƒฃKUKU WA KISASA๐Ÿ”...

โœ๏ธHawa Ni Kuku Walioboreshwa Wenye Sifa Tofauti Na Kuku Wa Kienyeji ๐Ÿ“ Yaani Kuku Hawa Kwenye Utagaji Na Ukuaji Ni Tofauti Kabisa Na Kuku Wa Asili Ila Kuku Wa Kisasa Wamegawanyika Katika Makundi Mawili 2๏ธโƒฃ Kama Ifuatavyo...

๐Ÿ”Chotara...

๐Ÿ”Pure Breed...

๐Ÿ™‡๐Ÿ™‡Mbona Kama Umechoka Kusoma Na Somo Ndio Kwanza Linaanza ๐Ÿ˜‚ Ayaah Tuendelee Sasa Tumesema KUKU WA KISASA Wapo Katika Makundi Mawili Na Tumeyataja Hapo Juu Eti Ameshasahau ๐Ÿ˜‚ Tumesema Wapo Chotara Na Pure Breed Ayaah Tunaposema Chotara Ndio Kuku Gani Na Tunaposema Pure Breed Ni Kuku Gani Pia...

๐Ÿ“๐Ÿ“KUKU CHOTARA...

โœ๏ธHawa Ni Kuku Wakisasa Waliochanganywa Na Kuku Wa Kienyeji Ili Kupata Mbegu Yenye Sifa Pande Zote Yaani Wanasifa Za Kisasa Na Pia Wanasifa Za Kuku Wa Asili Kama Vile...๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

๐Ÿ‘‰Wanauwezo Wa Kujitafutia Chakula Kama Kuku Wa Kienyeji...

๐Ÿ‘‰Wanauwezo Wa Kutaga Mayai Mengi Tofauti Na Kuku Wa Kienyeji...

๐Ÿ‘‰Licha Ya Kufanana Na Kuku Wa Kienyeji Ila Wamekosa Sifa Ya Kuatamia Yaani Hawawezi Kuatamia Mpaka Utumie Incubator Kutotolesha Mayai Yao...

๐Ÿ‘‰Wanakua Kwa Haraka Sana Na Pia Wanakua Na Uzito Mkubwa Kuliko Kuku Wa Kienyeji...

...Na Sifa Zingine Kedekede Kuhusu Hao Kuku Ila Kwa Leo Hizi Zinakutosha...

๐Ÿ“๐Ÿ“Kwa Kumalizia Kuku Hawa Ndio Wale Wanaoitwa KROILER ๐Ÿ‘‰ SASSO ๐Ÿ‘‰ TANBRO ๐Ÿ‘‰ KENBRO ๐Ÿ‘‰ Kwahiyo Ukiwa Na Hawa Kuku Jua Unafuga Kuku Chotara Na Sio Kuku Wa Kienyeji Kama Wengine Wanavyowaita...

๐Ÿ”๐Ÿ”PURE BREED...

โœ๏ธSasa Hawa Ndio Kuku Wa Kisasa Ambao Mbegu Zao Zimetengezwa Kisasa Zaidi Tukiwa Na Maana Hawa Ndio Kuku Wenye Sifa Za Utagaji Na Ukuaji Usio Wa Kawaida Na Kuku Wengine Yaani Chotara Atafanana Tabia Na Hawa Kuku Ila Hawezi Kuwa Nao Sawa Kabisa...

๐Ÿ”Pure Breed Hapa Ndio Unawakuta Kuku Wa Mayai (Layers) ๐Ÿฅš Na Pia Utakutana Na Broilers (Kuku Wa Nyama) Kwahiyo Hawa Wote Wanasifa Tofauti Mmoja Anakua Kwa Haraka Sana Na Kukupatia Nyama Na Mwingine Anakupatia Mayai Mengi Kwa Mwaka...

Leo jifunze kwanini kuku hula mayai au kutaga mayai yenye ganda laini na jinsi ya kumaliza tatizo hilo la kuku kula mayai au kuku kutaga mayai yenye ganda laini
Hi hapa video
๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡
https://youtu.be/UlA0Wuf7PYI

Ben Kukufarm

13 Jan, 03:23


https://youtu.be/Ds2_w2ABW5I

Ben Kukufarm

12 Jan, 03:35


https://youtu.be/-AHyar671KI

Ben Kukufarm

10 Jan, 03:35


ben:
Video
Jinsi ya kutumia majani ya mpera kutibu magonjwa ya kuku  ba yajue magonjwa ya kuku yanayotibika kwa majani ya mpera
๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡
https://youtu.be/o8Qt0GZiKOs

*MJUE KUKU AINA YA SASSO*

*BEN KUKUFARM*

*SASSO* ni kuku ambao mfugaji anaweza kuwafuga kwaajili ya mayai lakini pia kwaajili ya nyama. Pia ni kuku ambao wanakua katika mazingira ya aina yeyote kutokana na namna ya ufugaji utakao amua kuwafuga.

Unaweza kuwafuga ndani tu kama kuku wa nyama au mayai, pia unaweza kuwafuga kama kuku wa kienyeji kwa kuwaachia nnje (kujitafutia chakula na maji).


*SASSO* ni aina ya kuku ambao wana ladha ya kipekee kabisa kuliko aina yoyote ile ya kuku vilevile ni aina ya kuku wenye nguvu sana *(hard breeds or tough breeds)* ambao wana weza kuishi katika mazingira ya aina yeyote. Na kitu cha muhimu zaidi ni kwamba kuku hawa hawapati magonjwa kirahisi kulingaisha na kuku aina nyingine.

*SASSO* wana julikana kama kuku ambao wana rangirangi nyingi sana na kuku mmoja akitaga mayai yakitotolewa ni lazima vitoke vifaranga vyenye rangi nyingi yaani kila kifaranga kina kuwa na rangi yake.


*SASA KWANINI UFUGE SASSO*

Kuku aina ya *SASSO* ni wepesi kufugika, Hawaitaji uangalizi wa hali ya juu. Vilevile aina yake ya malisho au ulishaji ni sawa na kuku wa kienyeji.

Kuku hawa wana matokeo bora zaidi kuzidi kuku wa kienyeji kwakua wanakua haraka na pia kuku mmoja anauwezo wa kutaga *mayai 250* kwa muda wake wote tofauti na kuku wa kienyeji ambapo kuku mmoja hutaga mayai chini ya 100 kwa muda wake wote.

*SASSO* huanza kutaga kuanzia kati ya  wiki ya 18-20 na baada ya hapo hutaga mayai mpaka wiki 72.

*SASSO* anakua na uzito wa kuanzia 1.2kg baada ya siku 35 hivyo kumpa nafasi kubwa mkulima ya kuanza kujiingizia kipato mapema kupitia mayai na nyama kwa pamoja.

Kuku hawa wana matokeo mara tatu zaidi ya kuku wa kienyeji, hivyo basi kama mkulima na unapenda kukuza kipato chako na kufikia ndoto zako,

*SASSO* ni chaguo lililo bora zaidi  kwa kuyafikia malengo yako na kutimiza ndoto zako.

SOMO LA LEO
nimekuletea masomo mbalimbali kupitia Link za YouTube unaweza kuangalia video izi utajifunza kwa vitendo

*Somo la kwanza*
Umuhimu wa vitamini na jinsi ya kupunguza gharama za kununua vitamin za dukani kwa kutumia njia hii
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
https://youtu.be/FrfImQhA-6A

*Somo la pili*
Faida nane za kutumia mkaa katika chakula Cha mifugo kuzuia magonjwa yasitokee kwa mifugo wako
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
https://youtu.be/WF1FAgdXKDc

*Somo la tatu*
Njia rahisi ya kutibu Minyoo ya kuku bila kutumia gharama yoyote
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
https://youtu.be/XTMVVoEdXt8

*SOMO LA 4*
Sifa za Banda Bora la kuku na jinsi ya kulitengeneza
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
https://youtu.be/0u9a6eoXaw8

*SOMO LA 5*
Brooder kwaajiri ya kutunzia vifaranga wa kuku na jinsi ya kutengeneza
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
https://youtu.be/zK9yNbG3dts

*SOMO LA 6*
Sifa ya viota Bora vya kutagia kuku na jinsi ya kutengeneza
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
https://youtu.be/ARrxvYeQDew

*SOMO LA 7*
Fanya hivi kuzuia kuku kula mayai, kudonoana na kutaga mayai yenye Ganda laini au kuruka siku za kutaga
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
https://youtu.be/UlA0Wuf7PYI

Uchoyo wa elimu sio mzuri

*Share kwenye magroup mengine nao wajifunze*

Ben Kukufarm

08 Jan, 03:03


*SOMO MUHIMU KWA MFUGAJI KUKU*

*Na *BEN KUKUFARM*
*0746124684 au 0625728535*
Kipindi cha kifuku (kipindi cha joto kali) huongeza hatari ya magonjwa kwa kuku kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, unyevunyevu, na msongo (stress). Kuku wanaweza kupata magonjwa yanayotokana na joto kupita kiasi au mazingira machafu yanayotokana na jasho na unyevunyevu. Hapa ni magonjwa yanayojitokeza zaidi katika kipindi cha kifuku na jinsi ya kuyatambua na kuyadhibiti.

1. Heat Stress (Msongo wa Joto)

Sababu: Joto kali na uingizaji hewa duni kwenye banda.
Dalili:

Kuku kufungua midomo na kupumua kwa shida.

Kuku wanakaa mbali na wenzao (kutafuta sehemu ya baridi).

Kuku kushindwa kula vizuri na kupungua uzalishaji wa mayai.

Vifo ghafla.

Tiba na Kinga:

Hakikisha banda lina uingizaji hewa wa kutosha.

Weka maji safi na baridi kwa wingi.

Punguza msongamano wa kuku kwenye banda.

Weka kivuli au feni ndani ya banda.

2. Coccidiosis

Sababu: Unyevunyevu mwingi kwenye banda na kinyesi cha kuku.
Dalili:

Kuharisha damu
kinyesi chenye rangi ya kahawia.

Kuku kulegea na kupoteza hamu ya kula.

Manyoya kusimama na uzito kupungua.

Vifo vya ghafla kwa vifaranga.

Tiba na Kinga:

Tumia dawa za Coccidiosis (kama Amprolium) kwenye maji ya kunywa.

Safisha na kuondoa kinyesi mara kwa mara.

Weka sakafu kavu na epuka unyevunyevu kwenye banda.

3. Ndui ya Kuku (Fowl Pox)

Sababu: Kuenea kwa virusi kupitia mbu au wadudu wengine.
Dalili:

Vidonda kwenye sehemu zisizo na manyoya (kama mdomo na macho).

Kukosa hamu ya kula.

Kupungua kwa uzalishaji wa mayai.

Tiba na Kinga:

Chanjo ya Ndui ya Kuku.

Dhibiti mbu na wadudu wengine kwa kupulizia dawa za wadudu (insecticides).

Tengeneza banda lenye hewa safi na epuka maji yaliyotuama karibu na banda.

4. Kideri (Newcastle Disease)

Sababu: Maambukizi ya virusi yanayoenezwa kupitia hewa, chakula, na maji.
Dalili:

Kupumua kwa shida na kukohoa.

Kuharisha kijani.

Kupinda shingo na kutembea kwa matatizo.

Vifo vingi kwa muda mfupi.


Tiba na Kinga:

Hakuna tiba ya moja kwa moja, lakini unaweza kutumia antibiotics za kuzuia maambukizi ya pili (secondary infections).

Chanjo ya Kideri mara kwa mara (kwa vifaranga na kuku wakubwa).

Osha na safisha vifaa vya kulishia na kunyweshea mara kwa mara.


5. Salmonella (Typhoid ya Kuku)

Sababu: Chakula na maji yaliyochafuliwa na kinyesi au maambukizi ya moja kwa moja kutoka kwa kuku wengine.
Dalili:

Kuharisha maji ya kijani au kahawia.

Kuku kulegea na kukosa nguvu.

Kupungua kwa uzito na kutaga mayai madogo.

Vifo visivyoeleweka.

Tiba na Kinga:

Tumia antibiotics (kama Amoxicillin au Tetracycline) baada ya kushauriana na daktari wa mifugo.

Safisha banda mara kwa mara na osha vifaa kwa maji ya moto.

Hakikisha maji na chakula ni safi kila wakati.

6. Gumboro Disease (Infectious Bursal Disease)

Sababu: Maambukizi ya virusi yanayoathiri vifaranga.
Dalili:

Vifaranga kulegea na kukaa chini kwa muda mrefu.

Kuharisha maji au kinyesi cha rangi isiyo ya kawaida.

Kuku kunyauka na vifo kwa wingi.

Tiba na Kinga:

Hakuna tiba, lakini chanjo ya Gumboro ni muhimu kwa vifaranga.

Osha na dawa banda kabla ya kuweka vifaranga wapya.

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Kipindi cha Kifuku:

1. Uingizaji Hewa: Hakikisha banda lina hewa ya kutosha na epuka msongamano.


2. Maji na Chakula: Kuku wapate maji safi na baridi kila wakati. Ongeza vitamini na electrolytes kwenye maji ya kunywa.


3. Chanjo: Fanya chanjo kwa wakati ili kuzuia magonjwa yanayoambukizwa kwa urahisi.


4. Usafi: Safisha banda na vifaa vya chakula na maji kila siku. Epuka unyevunyevu.


5. Kinga ya Wadudu: Dhibiti mbu, nzi na wadudu wengine wanaoeneza magonjwa.

Kipindi cha kifuku kinaweza kuwa na changamoto, lakini kwa kufuata hatua hizi, unaweza kupunguza vifo na kuongeza uzalishaji wa kuku wako.

SOMO LA LEO
nimekuletea masomo mbalimbali kupitia Link za YouTube unaweza kuangalia video izi utajifunza kwa vitendo

*HII HAPA FORMULA YA UTENGENEZAJI WA CHAKULA BORA CHA KUKU*

*itumie utakuja kunishukuru*
๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

https://youtu.be/MYQrRFCgONc

Ben Kukufarm

08 Jan, 03:03


*SOMO LA kwanza*
Fanya hivi kuzuia kuku kula mayai, kudonoana na kutaga mayai yenye Ganda laini au kuruka siku za kutaga
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
https://youtu.be/UlA0Wuf7PYI



*Somo la pili*
Faida nane za kutumia mkaa katika chakula Cha mifugo kuzuia magonjwa yasitokee kwa mifugo wako
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
https://youtu.be/WF1FAgdXKDc

*Somo la tatu*
Njia rahisi ya kutibu Minyoo ya kuku bila kutumia gharama yoyote
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
https://youtu.be/XTMVVoEdXt8

*SOMO LA 4*
Sifa za Banda Bora la kuku na jinsi ya kulitengeneza
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
https://youtu.be/0u9a6eoXaw8

*SOMO LA 5*
Brooder kwaajiri ya kutunzia vifaranga wa kuku na jinsi ya kutengeneza
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
https://youtu.be/zK9yNbG3dts

*SOMO LA 6*
Sifa ya viota Bora vya kutagia kuku na jinsi ya kutengeneza
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
https://youtu.be/ARrxvYeQDew

*Somo la saba*
Umuhimu wa vitamini na jinsi ya kupunguza gharama za kununua vitamin za dukani kwa kutumia njia hii
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
https://youtu.be/FrfImQhA-6A
Uchoyo wa elimu sio mzuri

*Share kwenye magroup mengine nao wajifunze*

Ben Kukufarm

02 Jan, 02:29


https://youtu.be/-AHyar671KI

Ben Kukufarm

01 Jan, 14:15


Heri ya mwaka mpya wafugaji wenzangu hakika tumevuka tuendelee kupeana elimu ili kukabiliana na changamoto mbalimbali katika tasnia hii ya ufugaji

Leo tupo na hili somo

*JINSI YA KUANDAA KISAMVU DAWA YA UTITILI, CHAWA NA VIROBOTO KWA KUKU*

*tazama video*
๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡
https://youtu.be/YbOQv6zUWrs

*Share*

Ben Kukufarm

29 Dec, 15:19


https://youtu.be/l4eir6SzKbY

Ben Kukufarm

28 Dec, 09:43


ONGEZA FAIDA KATIKA UFUGAJI WA KUKU
kwa kutumia chakula mbadala ili kupunguza gharama za chakula Cha kuku wako au mifugo mingine
jifunze jinsi ya kuotesha hydroponic fodder kwaajili ya malisho ya mifugo
๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

https://youtu.be/yxnYO85avgU

Ben Kukufarm

02 Dec, 20:05


Formula ya utengenezaji chakula Cha kuku ili kupunguza gharama za manunuzi ya chakula Cha dukani
๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡
https://youtu.be/MYQrRFCgONc

Ben Kukufarm

29 Nov, 18:47


https://youtu.be/yxnYO85avgU

Ben Kukufarm

28 Nov, 14:35


https://youtu.be/WF1FAgdXKDc

Ben Kukufarm

26 Nov, 12:29


https://youtu.be/QFMAxdYtcz4

Ben Kukufarm

26 Nov, 02:51


https://youtu.be/yxnYO85avgU

Ben Kukufarm

24 Nov, 13:37


Hii hapa dawa nzuri ya asili inayoweza tibu magonjwa mengi ya kuku
๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡
https://youtu.be/SMB96zE40gc

Ben Kukufarm

02 Nov, 13:31


Zimebaki siku chache Sana hivyo lipia tsh 10,000 namba ya malipo ni Voda 0746124684 jina benedicto mgata baada ya Apo niambie kuwa umeshร  lipia na unipe namba ya WhatsApp nikuunge kwenye group

Ben Kukufarm

30 Oct, 23:28


Zimebaki siku chache Sana hivyo lipia tsh 10,000 namba ya malipo ni Voda 0746124684 jina benedicto mgata baada ya Apo niambie kuwa umeshร  lipia na unipe namba ya WhatsApp nikuunge kwenye group

Ben Kukufarm

29 Oct, 04:05


*Unakumbushwa* Kama wewe ni mmoja ya wale wanao hitaji kujifunza kuhusu uundaji incubator,utunzaji wa vifaranga na jinsi ya kupunguza gharama za chakula katika ufugaji basi tambua zimebaki siku chache fanya malipo uungwe kwenye group la mafunzo tarehe 4 tunaanza mafunzo yetu

Ben Kukufarm

17 Oct, 10:37


*Madhara ya uchafu kwenye banda la kuku.*

Uchafu kwenye banda la kuku unaweza kusababisha magonjwa mbalimbali kwa kuku. Baadhi ya madhara na magonjwa yanayoweza kutokea ni pamoja na:

*Magonjwa ya ngozi: Uchafu unaweza kusababisha* magonjwa ya ngozi kwa kuku kama vile fangasi, vidonda, au michubuko inayoweza kusababishwa na bakteria au vimelea.

*Magonjwa ya mfumo wa kupumua* : Banda chafu kinaweza kusababisha ukuaji wa bakteria na virusi ambavyo vinaweza kusababisha magonjwa ya mfumo wa kupumua kwa kuku.

*Magonjwa ya matumbo:* Uchafu unaweza kusababisha maambukizi ya bakteria kwenye vyakula vya kuku na hivyo kusababisha magonjwa ya matumbo.

*Kuvutia wadudu na vimelea:* Uchafu unaweza kuwavutia wadudu kama nzi, chawa, au viroboto ambavyo vinaweza kusambaza magonjwa kwa kuku.

*Ni muhimu kusafisha mara kwa mara banda la kuku ili kuepuka magonjwa haya na kuhakikisha kuwa kuku wanapata mazingira safi na salama ya kuishi.*

baada ya kuona madhara ya uchafu kwenye banda la kuku basi tuangalie jinsi ya kutunza banda la kuku.

*Kutunza banda la kuku kuna hatua kadhaa muhimu.* Hapa kuna miongozo ya jinsi ya kutunza banda la kuku:

*Usafi* : Safisha mara kwa mara banda la kuku ili kuondoa uchafu, mabaki ya chakula, na takataka. Hii itazuia magonjwa na kuwapa kuku mazingira safi.

*Mipangilio Bora:* Hakikisha banda la kuku lina mifumo mizuri ya uingizaji hewa na mwanga. Pia, weka makasha ya kuku na viota vya kulelea mayai kwa kuzingatia idadi ya kuku unaowatunza.

*Lishe Bora:* Hakikisha kuku wanapata lishe bora na ya kutosha. Wape chakula cha kuku kinachofaa kulingana na umri wao na hakikisha maji safi yanapatikana kila wakati.

*Kinga na Afya:* Fanya chanjo za mara kwa mara kwa kuku na ukague kila mara afya zao. Ikiwa kuna dalili za magonjwa, wasiliana na mtaalamu wa wanyama au mtaalamu wa kuku ili kupata ushauri.

*Ulinzi* : Hakikisha banda la kuku lina kinga imara dhidi ya wanyama waharibifu kama vile mbwa, paka, au wanyama wengine wa porini.

kwakufuata miongozo hii ya msingi, utaweza kutunza banda la kuku kwa ufanisi na kuhakikisha kuku wako wanakuwa na afya njema na uzalishaji mzuri.

#BEN KUKUFARM
0746124684 au 0625728535

SOMO LA LEO
nimekuletea masomo mbalimbali kupitia Link za YouTube unaweza kuangalia video izi utajifunza kwa vitendo

[10/17, 10:05] Ben: Somo la ziada jinsi ya kuandaa majani ya mapera dawa nzuri ya kuku
๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡
https://youtu.be/o8Qt0GZiKOs


https://youtu.be/o8Qt0GZiKOs


*SOMO LA kwanza*
Fanya hivi kuzuia kuku kula mayai, kudonoana na kutaga mayai yenye Ganda laini au kuruka siku za kutaga
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
https://youtu.be/UlA0Wuf7PYI



*Somo la pili*
Faida nane za kutumia mkaa katika chakula Cha mifugo kuzuia magonjwa yasitokee kwa mifugo wako
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
https://youtu.be/WF1FAgdXKDc

*Somo la tatu*
Njia rahisi ya kutibu Minyoo ya kuku bila kutumia gharama yoyote
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
https://youtu.be/XTMVVoEdXt8

*SOMO LA 4*
Sifa za Banda Bora la kuku na jinsi ya kulitengeneza
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
https://youtu.be/0u9a6eoXaw8

*SOMO LA 5*
Brooder kwaajiri ya kutunzia vifaranga wa kuku na jinsi ya kutengeneza
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
https://youtu.be/zK9yNbG3dts

*SOMO LA 6*
Sifa ya viota Bora vya kutagia kuku na jinsi ya kutengeneza
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
https://youtu.be/ARrxvYeQDew

*Somo la saba*
Umuhimu wa vitamini na jinsi ya kupunguza gharama za kununua vitamin za dukani kwa kutumia njia hii
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
https://youtu.be/FrfImQhA-6A
Uchoyo wa elimu sio mzuri

*Share kwenye magroup mengine nao wajifunze*

Ben Kukufarm

16 Oct, 17:25


Kuku wangu wa kienyeji wanadonoana sana manyoya, shida itakuwa nini? Na nifanyaje?

Jibu

Kuku wako wa kienyeji wanapodonoana manyoya, inaweza kuwa ishara ya matatizo kadhaa:

1. *Msongamano*: Kuku wakiwa wengi sana kwenye eneo dogo, wanakuwa na nafasi ndogo ya kutembea na hii inaweza kusababisha stress na kudonoana. Hakikisha unawapa nafasi ya kutosha.

2. *Lishe Duni*: Upungufu wa madini kama vile protini, kalsiamu, na vitamini unaweza kuwafanya kuku waanze kudonoana. Hakikisha wanapata chakula bora kilicho na virutubisho vyote muhimu.

3. *Stress*: Stress inaweza kusababishwa na mabadiliko ya ghafla katika mazingira, kama vile uingizaji wa kuku wapya, joto kali, au kelele nyingi. Hakikisha mazingira yao ni tulivu na yenye utulivu.

4. *Magonjwa*: Magonjwa kama vile minyoo au wadudu kama utitiri wanaweza kusababisha kuku kujikuna na hatimaye kudonoana. Ni muhimu kuchunguza kama kuna dalili za magonjwa na kuwapa tiba ipasavyo.

*Suluhisho*:
- Punguza msongamano kwa kuhakikisha unatoa nafasi ya kutosha kwa kila kuku.
- Angalia chakula chao na uhakikishe wanapata lishe bora yenye protini ya kutosha.
- Angalia kama kuna dalili zozote za magonjwa na upate ushauri wa mtaalamu wa mifugo.
- Weka vitu vya kuwafanya kuku waburudike kama vile majani au pumba ili wasikae bure na kuanza kudonoana.

Kwa kufuata haya, unaweza kupunguza au kumaliza tatizo la kuku kudonoana manyoya.

SOMO LA LEO
nimekuletea masomo mbalimbali kupitia Link za YouTube unaweza kuangalia video izi utajifunza kwa vitendo

*SOMO LA kwanza*
Fanya hivi kuzuia kuku kula mayai, kudonoana na kutaga mayai yenye Ganda laini au kuruka siku za kutaga
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
https://youtu.be/UlA0Wuf7PYI



*Somo la pili*
Faida nane za kutumia mkaa katika chakula Cha mifugo kuzuia magonjwa yasitokee kwa mifugo wako
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
https://youtu.be/WF1FAgdXKDc

*Somo la tatu*
Njia rahisi ya kutibu Minyoo ya kuku bila kutumia gharama yoyote
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
https://youtu.be/XTMVVoEdXt8

*SOMO LA 4*
Sifa za Banda Bora la kuku na jinsi ya kulitengeneza
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
https://youtu.be/0u9a6eoXaw8

*SOMO LA 5*
Brooder kwaajiri ya kutunzia vifaranga wa kuku na jinsi ya kutengeneza
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
https://youtu.be/zK9yNbG3dts

*SOMO LA 6*
Sifa ya viota Bora vya kutagia kuku na jinsi ya kutengeneza
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
https://youtu.be/ARrxvYeQDew

*Somo la saba*
Umuhimu wa vitamini na jinsi ya kupunguza gharama za kununua vitamin za dukani kwa kutumia njia hii
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
https://youtu.be/FrfImQhA-6A
Uchoyo wa elimu sio mzuri

*Share kwenye magroup mengine nao wajifunze*

Ben Kukufarm

14 Oct, 10:59


Je wajua Kuwa binzari ina msaada mkubwa katika kuboresha afya ya kuku? Kama hujui leo utajua nimekuletea video inayohusu faida za binzari kwa kuku, jinsi ya kuandaa binzari kwaajili ya kuku,na magonjwa unayoweza kumtibu kuku kwa binzari

*Tazama video kupitia link hii*
๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡
https://youtu.be/HHAuN-BhfUU

Ben Kukufarm

14 Oct, 05:12


https://youtu.be/o8Qt0GZiKOs

Ben Kukufarm

12 Oct, 21:21


*Brooder no Nini?*
Brooder ni sehemu masrumu inayotengenezwa ili itumike kutunza vifaranga
Lengo la kutengeneza brooder ili kutusaidia kuwapa vifaranga joto sahihi ili wasiathirike kwa baridi au joto lililo zidi maana huathili ukuaji wa vifaranga video hii inaonyesha hatua kwa hatua jinsi mtu anaweza tengeneza brooder kwa ajiri ya vifaranga wake wenye umli chini ya mwezi mmoja
*Itazame utakuja kuniehukuru*
๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

https://youtu.be/zK9yNbG3dts

Ben Kukufarm

09 Oct, 04:07


Kwa wale mliokosa mafunzo haya mwezi wa Tisa karibu mwezi wa kumi na moja ujifunze

Ben Kukufarm

07 Oct, 14:18


*NAWALISHA KUKU WANGU HAWAKUI NIFANYE NINI??*

JIBU!!..
KUKU KUKUA IMEGAWANYIKA
MAKUNDI MATATU,

# MBEGU YA KUKU!!
# CHAKULA UNACHOWALISHA,/ KIPIMO UNACHOWAPA,...

#MAGONJWA NA MAZINGIRA!!

1= MBEGU YA KUKU INAWEZA KUWA SABABU KUU YA KUKU WAKO KUKUA,

# WAPO KUKU MBEGU NDOGO UKUWAJI WAKE NI MDOGO HAWAWEZI KUKUA ZAIDI YA MAUMBO YAO

# HAKIKISHA CHAGUA LAKO NI SAHIHI KWENYE MBEGU,

2= HAKIKISHA CHAKULA WANACHOKULA KUKU NI LISHE YENYE UKAMILIFU, NA SIO BORA LISHE,

# HAKIKISHA WANAKULA KULINGANA NA UMRI WAO, KWANI MWILI HAUJENGWI KWA MATOFALI NI CHAKULA,

KILA KUKU ALE KULINGANA NA IMRI WAKE,,

JIZOWESHE HIVO ITAKUPUNGUZIA MALALAMIKO,,

# KUKU MKUBWA USIMPE CHA VIFARANGA,
.
# ZINGATIA HAYA ILI USILAUMU KILA KITU HATA WEWE MWENYEWE UTIJILAUMU,

#KINGA ZA MSINGI ZA KUKU,
# KUKU WAKINGWE UPESI MAGONJWA KUANZIA KINGA YA MAHEPE,
MDONDO,"
GOMBORO, "
NDUI, "
DAWA ZA MINYOO, "
NK!..


#KUKU WATIBIWE UPESI KABLA
HAWAJAONEWA NA MAGONJWA,

# ONDOA TATIZO HILI KWA.....

" KUKU WALE KWA WAKATI MDA UNAOFANANA SIKU ZOTE,

" KUKU WALE CHAKULA WASHIBE KULINGANA NA UMRI WAO,


" KUKU WAKIWA NA SIKU MOJA MPAKA YA 45 WASIPIMIWE CHAKULA,

". KUKU WAWEKEWE VYOMBO VYA CHAKULA KULINGANA NA IDADI YA KUKU,

" TUMIA MARA KWA MARA, LISHE YA MIMEA HIZI KAMA CHANZO CHA VITAMIN KWA KUKU WAKO,
KAMA ZA DUKANI ZIMEKOSEKANA AMA PESA HAUNA YA ESABU HII!!..


# MWALOVERA,
# MLONGE,
# MAJANI YA MPAPAI,
# MCHICHA ASILI ( BWASI)
# AZOLA,
# MAJANI YA MIPERA

*Jifunze zaidi kuhusu majani ya mlonge tazama video kupitia link hii chini huto jutia*
๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

https://youtu.be/-AHyar671KI?si=8qlcaWQ6Dsq1L_2U

Ben Kukufarm

03 Oct, 04:10


Je unakosea wap kipindi Cha utunzaji vifaranga?
Kama umekuwa ukipata vifo vya vifaranga na hujui nini kosa tazama video hii Hadi mwisho utajifunza
๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡
Subscribe channel hii ujifunze mengi zaidi kuhusu ufugaji

https://youtu.be/8WzrK3q0JxY

Ben Kukufarm

03 Oct, 04:09


https://youtube.com/shorts/032DlgoSx_4?feature=share

Ben Kukufarm

01 Oct, 14:52


*DAWA ZA ASILI* hizi hapa video mbalimbali zinazofundisha jinsi ya kuandaa dawa tofautitofauti za asili zenye uwezo wa kutibu magonjwa mbalimbali ya kuku jifunze sasa ili upunguze gharama ,zitokanazo na manunuzi ya dawa za dukani hapa utajifunza jinsi ya kuziandaa dawa hizo na kuzitumia kwa magonjwa mengi

*Tizama video hizi*
๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ๐Ÿ‘‡๐Ÿผ
https://www.youtube.com/playlist?list=PL-08tp9_pkhf_efkcs_l_vTwRN-Rbq4th

*Usiwe mchoyo tuma link hi na wengine wajifunze pamoja nasi Asante* ๐Ÿ™๐Ÿ™

Ben Kukufarm

26 Sep, 03:40


๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“๐Ÿ“
*SIKU 60 AMBAZO ZINAZOWEZA KUMUONDOA MFUGAJI BARABARANI*
................................๐Ÿ‡๐Ÿ‘‡
Katika safari ya ufugaji hasa ambayo inaanza na vifaranga kuna changamoto kadhaa ambazo zikiendelea zaidi ya siku 60 Tangu kupokea vifaranga ni rahisi kumuondoa mfugaji huyu kwenye tasinia ya ufugaji
๐Ÿ“ *MAGONJWA*... magonjwa yasiokoma bandani kwa vifaranga ni changamoto ambayo imetajwa kuwatoa wafugaji wengi kwenye Ramani na kujikuta wanawachukia vifaranga na kuwasusa. Wapo ambao hulazimika kuwauza hata kama wanaumwa ili muradi kurudisha pesa yake. 
Magonjwa ambayo yameshika hatamu katika vifaranga kwa wafugaji wengi ni
โœ”๏ธ  mafua
โœ”๏ธcoccidiosis
โœ”๏ธ typhoid na
โœ”๏ธprolium.
Haya ni magonjwa ambayo yamewafanya wafugaji wengi kukata tamaa na kuamini kuwa ufugaji ni zaidi ya kile wanacho ambiwa.
Hayo magonjwa yakikatalia bandani mara kwa mara ndani ya siku 60 garama zake ni zaidi ya 150,000/= mpaka 200,000/= kuyaondoa bandani.   Nasema hivyo kwa sababu dawa za kupambana na haya magonjwa huwa zinaanzia 15,000/= kwa moja ni garama kwa kiasi furani.
Jambo hili hupelekea wafugaji wengi kukata tamaa na kuona ameingia hasara hata kabla ya kufikia umri wa kutaga. 
๐Ÿ“ *BAJETI FINYU*....
Hapa mara nyingi huwa ni upande wa chakula,  maranda,  vitamin nk.  Kwa upande wa magonjwa huwa ni ngumu kuyawekea bajeti kwa sababu hatujui kifaranga ataumwa nini na kwa mara ngapi na atahitaji dawa ngapi. 
Kuna wafugaji huanza vyema lkn ikifika siku 60 mpaka 90 za ufugaji wao huanza kuyumba na kujikuta wanadhofisha kuku kwa kuwapa pumba na mwisho wa siku hujikuta wanauza kuku chini kiwango na hayakuwa malengo isipokuwa ameshindwa kuwaendesha.
๐Ÿ“ *MBEGU CHAFU* .... mbegu chafu ni chanzo cha kumfanya mfugaji apate hasara ndani ya siku 60 kwa kudumaa kwa vifaranga licha ya kwamba anawahudumia vizur na hawana magonjwa.  Wapo watu ambao huwabbikizia wafugaji vifaranga na kuambia ni kroila kumbe ni vifaranga wa kienyeji 
. Hapa mfugaji hutumia Sana rasilimali kuhudumia na kuchelewa Kuona matokeo Kisha anakata tamaa.
.....................................
Staki kuwa mchoyo Soma na hii utakuja kunishukuru Niko pale

Magonjwa 5 tishio kwa kuku ingia hapa
๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡
Elimu ya ufugaji kuku na magonjwa ya kuku: https://www.youtube.com/playlist?list=PL-08tp9_pkhf_efkcs_l_vTwRN-Rbq4th

Ben Kukufarm

23 Sep, 07:25


Tangazo nililotuma saa moja asubuhi lilikosewa namba ya simu waliopiga kapokea mdada imenibidi nifanye marekebisho ya namba ya simu pamoja na kuongeza kiwango Cha malipo hivyo kama ulichukua namba yenye 12 katikati hiyo sio yangu namba yangu ni hi 0746124684 na nimeiandika upya kwenye picha ya tangazo hakikisha unapofanya muamala jina linakuja BENEDICTO MGATA ili usije tuma pesa kwa mtu mwingine samahani kwa usumbufu

Ben Kukufarm

18 Sep, 13:45


Video
Jinsi ya kutumia majani ya mpera kutibu magonjwa ya kuku ba yajue magonjwa ya kuku yanayotibika kwa majani ya mpera
๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡
https://youtu.be/o8Qt0GZiKOs

Ben Kukufarm

18 Sep, 07:22


https://youtu.be/-AHyar671KI

1,322

subscribers

311

photos

24

videos