بسم الله الرحمن الرحيم
🔥https://t.me/ruduudilmiyyahssalafiyyahTZ
الحمد لله حمدا كثيرا طيبا مباركا فيه وأشهد أن لا إله إلا الله وأشهد أن محمد عبده ورسوله... أما بعد.
يقول الله في كتابه الكريم:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا (70) يُصْلِحْ لَكُمْ أَعْمَالَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَمَن يُطِعِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ فَازَ فَوْزًا عَظِيمًا (71). سورة الأحزاب
✍🏻ويقول الشاعر:
تكلَّمْ وسدَّدْ ما استطعْتَ ••• فإنَّما
كلامُكَ حَيُّ والسُّكوتُ جَمادُ.
وإن لم تجِدْ قولاً سديداً تقولُهُ ••• فصمْتُكَ مِن غِيرِ السَّدادِ سَدادُ.
Ama baada ya utangulizi huo mfupi enyi ndugu zangu wabora Allaah awahifadhi, kama mnakumbuka mnamo tarehe 28 Jumaadal Aakhirah 1446 H, sawa na tarehe 29 December 2024 M nilitawanya ubainifu kunako ufutwaji wa darasa katika channel yangu ya telegram niliyoianzisha ikiwa na lengo la kuhifadhi darasa za ndugu Abuu Usaamah Khamiys bnu Ame Allaah amuwafikishe na amuongoze katika haki na uadilifu, na ubainifu ule ulikuwa ni wenye kujitosheleza kwa kila yule ambaye aliusoma kwa jicho la uadilifu kinyume na yule ambaye jicho lake limejaa ukungu wa ta'aswub na kutokuwa na uadilifu wa kuzidurusu kadhiya vile inavyopaswa na alhamdulillaah wenye kuelewa walielewa kile nilichobainisha na kuainisha nukta za msingi zilizopelekea tukio lile kutokea.
Na nilielekeza umma wa kiislamu na masalafi khaaswa watakaohitajia darasa za ndugu Abuu Usaamah Khamiys bnu Ame watazipata katika channels zingine; Ambapo moja ipo chini yangu na nyingine ipo chini ya usimamizi wa ndugu yetu Abuu Muhsin Ja'afar حفظه الله ورعاه, ambaye huzikusanya darasa za walinganizi wote pindi wanapokuwa wamekamilisha vitabu basi hukusanya darasa hizo na mtu akihitajia atazipata kwa wepesi zaidi biidhnillaah na kuendelea kupata faaida.
Na miongoni mwa walinganizi ambao darasa zake zimekusanywa huko ni za ndugu Abuu Usaamah Khamiys bnu Ame Allaah amuongoze katika haki.
Lakini kwa masikitiko makubwa badala ya ndugu yetu huyu kuusoma ubainifu wangu ule kwa uadilifu na akafuatilia kwa makini zile nukta za msingi nilizoainisha kwa lengo la kujaribu kutengeneza yale aliyoharibu ambayo ndiyo yalikuwa chanzo cha mimi kufikia hatua ile, yeye akaendelea na yake na huku akinisemea uwongo mbele ya wanafunzi wake na umma mzima wa kiislamu wanaoifuatilia da'wah hii yenye baraka, kuwa mimi nimefuta darasa zake zote kwenye telegram channel yake (akikusudia hii channel yangu niliyoianzisha mimi), jambo ambalo siyo sahihi Allaahul mustaa'aanu.
Na sahihi ni kwamba sehemu kubwa ya darasa bado zipo, kama ambavyo nitabainisha hilo kupitia links nitakazozianisha hapo mbeleni na si kweli kwamba eti darasa zote zimefutwa na hakuna uwezekano wa kuzipata kabisa.
Na katika maneno yake mengine alipokuwa akizungumza na mmoja wa ndugu zetu akamwambia kwamba sisi tumefuta telegram yake yote, lakini wala hajadhurika na lolote na darasa zake zinaendelea, maneno ambayo yamejaa jeuri na kujiona ndani yake bila kujali mazungumzo azungumzayo yana athari kwake kiasi gani huku akidhania kwamba ananikomoa mimi au anatukomoa sisi kama alivyoyatamka kwa ujumla jumla Allaah amuongoze katika haki.
Sasa baada ya kunyamaza kwa muda kidogo, nimeanza kuona baadhi ya watu wenye kumfuata kiupofu huyu ndugu wakieneza huku na kule kuwa mimi nimefuta darasa na wakiwa wanaelekea kupotezea nukta kuu za msingi kwenye kadhiya hii na wakitaka kuulaghai umma wa kiislamu uone kuwa mimi nimefanya dhambi kubwa mno na kwamba ndugu Abuu Usaamah Khamiys bnu Ame hana kosa lolote katika kadhiya hii, jambo ambalo kwa mtu mwenye uadilifu na uelewa ulio safi hawezi kuitakidi itikadi hii mbovu na yenye uvundo ndani yake.
Kabla sijaelekea katika kiini cha ubainifu huu nilioudhamiria leo hii, napenda kumkumbusha ndugu Abuu Usaamah Khamiys bnu Ame Allaah amuongoze, pamoja na wale wenye kumtetea kwa baatwil kuwa wanapaswa wausome ubainifu wangu uliopita katika tarehe tajwa huko juu na kama hawataki kuusoma basi wamche Mola wao mlezi na waache