Fahamu Mengi @fahamuzaidiii Channel on Telegram

Fahamu Mengi

@fahamuzaidiii


Pata stories mbalimbali humu
Buy ads on: https://telega.io/c/fahamuzaidii

Fahamu Mengi (Swahili)

Fahamu Mengi ni jukwaa la Telegram linalokuwezesha kupata stories mbalimbali za kusisimua. Kupitia jukwaa hili la fahamuzaidiii, utaweza kufurahia maudhui ya kusisimua kama vile visa vya kuvutia, hadithi za kusisimua, na mengi zaidi. Hapa utapata burudani ya hali ya juu na kuelimika kupitia makala mbalimbali zinazopatikana kwenye jukwaa hili. Fahamu Mengi inakuletea maudhui yanayokupa maarifa na kufanya muda wako uwe wa kuvutia na kuelimisha. nnKwa wapenda burudani na maarifa, jukwaa hili ni mahali pazuri kwako. Jisajili sasa na uanze kufurahia stories mbalimbali zilizo kwenye fahamuzaidiii. Kupitia jukwaa hili, utapata uzoefu wa kipekee wa kusoma na kujifunza mambo mbalimbali yanayoweza kuboresha maisha yako. Usikose nafasi ya kuungana na jamii iliyopo kwenye Fahamu Mengi na kujifunza kutoka kwa wengine. nnIkiwa unataka kuwafikia watumiaji wa jukwaa hili kwa kutangaza biashara yako au huduma zako, unaweza kununua matangazo kwa njia rahisi kupitia kiungo hiki: https://telega.io/c/fahamuzaidii. Hii ni fursa nzuri ya kukuza biashara yako na kuwafikia wateja wapya. Fahamu Mengi inakupa nafasi ya kipekee ya kushiriki na kufaidika na maudhui bora zinazopatikana kwenye Telegram. Jiunge leo na upate mengi zaidi!

Fahamu Mengi

18 Nov, 04:50


Ezo Momonga labda ndiye kiumbe mrembo zaidi kwenye sayari hii

Ezo Momonga ni squirrel mdogo na mzuri sana anayeruka, pia huitwa flycatcher ya Siberia. Mahali pekee kwenye sayari hii anapatikana ndani ya kisiwa cha Japan cha Hokkaido.

Fahamu Mengi

14 Nov, 06:39


Enjoy our content? Advertise on this channel and reach a highly engaged audience! 👉🏻

It's easy with Telega.io. As the leading platform for native ads and integrations on Telegram, it provides user-friendly and efficient tools for quick and automated ad launches.

⚡️ Place your ad here in three simple steps:

1 Sign up

2 Top up the balance in a convenient way

3 Create your advertising post

If your ad aligns with our content, we’ll gladly publish it.

Start your promotion journey now!

Fahamu Mengi

04 Nov, 11:36


Asali inaweza kudumu kwa zaidi ya miaka 300 bila kuharibika hii ni kitokana na asali kua na kiwango kidogo cha unyevunyevu na Ph yake kua ndogo ambayo ni kati ya 3-4.5 hii hufanya vijidudu vinavyosababisha kuharibika kwa vyakula kushindwa kuweka makazi kwenye asali. Utafiti unaonyesha kua wakati wa kipindi cha zamani huko misri ya kale asali ya zaiddi ya maiaka 3000 ilikutwa ikiwa bado nzuri na inalika bila kuleta madhara kwa binadamu.

Fahamu Mengi

21 Oct, 01:38


Joseph alisimulia kuwa wakati akilelewa katika kituo cha watoto yatima cha Joseph’s Orphanage huko Vermont US alikutana na tabia za kushangaza za watoto wa kiume kulazimishwa kuchezeana uume, na kama ukikataa basi unachanwa na viwembe katika sehemu hizo za siri ili uumie.

Joseph alisema kuwa ilikuwa inafika wakati watoto wanapelekwa kwenye mikutano na semina kabisa kufundishwa tabia hizo za kushangaza.

Kwa kusaidiana na mwanasheria wake Philip White, Joseph aliamua kufungua kesi mahakamani dhidi ya kanisa katoliki Dayosisi ya Vermont waliokuwa ndio waendeshaji wa kituo hicho akidai kuwa walikuwa wakihusika na uharibifu huo wa watoto kwa miaka yote.

Kesi hiyo namba 839 F. Supp. 275 (1993) ilisomwa kwa mara ya kwanza mahakamani November 10, 1993.

Katika mashitaka yake alisema alikuwa ameanza kujiuguza majeraha na kujiuguza kisaikolojia tangu mwaka 1992 kutokana na unyanyasaji kingono alikokuwa akiupata wakati akiwa mtoto akilelewa katika kituo hicho, alimshitaki moja kwa moja Sister Jane Doe kuwa ndiye mhusika mkuu.

Kituo hicho cha watoto yatima kilianza kuhudumu tangu miaka ya 1863 kikichukua watoto wa chini ya miaka 8, lakini kutokana na skendo hizo ikabidi kifungwe mwaka 1974, hakipo tena. Pichani ni sehemu ya majengo ya kituo hicho.

Fahamu Mengi

16 Oct, 17:05


Australia inasonga kwa kiwango cha cm 8.44 kwa mwaka.

Ndio bara linatembea Kwa Kasi zaidi kuliko mabara yote duniani.

Fahamu Mengi

06 Oct, 12:22


Hapo mwanzo tairi za magari zilikua na rangi nyeupe lakini ilipofika mwaka 1912 zilibadilishwa na kua nyeusi,hii ni baada ya carbon kuongezwa kwenye formula ya kutengeneza tairi.Iligundulika kua carbon inaweza kufanya tairi kua imara na kudumu kwa muda mrefu.

Fahamu Mengi

29 Sep, 13:20


Inaelezwa kuwa injiania Nigel alikua anapenda sana bata hadi kufikia treni mpya ya LNER Class A4 4468 Mallard iliyoanza safari zake nchini humo mwaka 1938 kupewa jina hilo la bata, treni hii ilianza safari katika reli aliyoisimamia yeye wakati wa ujenzi kama injinia.

Treni inaitwa LNER Class A4 4468 Mallard, sasa hiyo Mallard mwishoni maana yake bata, ni ndege wanaofanana kwa asilimia 100 na bata, kuna duck na mallad, wote ni bata, kwahiyo waliipa treni jina hilo la bata kwa heshima ya jamaa kupenda sana ndege hao.

Sasa mwaka 2016 ikiwa inatimia miaka 75 tangu mtaalamu afariki mwaka 1941, serikali ikazindua sanamu yake hiyo iliyopo katika stesheni ya treni ya King's Cross huko London kama heshima ya kumkumbuka kwa utaalamu wake mkubwa katika usafiri wa treni nchini humo.

Sanamu ilimuonyesha yeye akiwa amesimama (pichani) huku mguuni kukiwa na sanamu ya bata aliyeonekana amesimama naye kufuatia injinia huyo kua na mapenzi makubwa sana kwa bata enzi za uhai wake, kwani hata moja ya treni ilipewa jina la bata kwaajili yake.

Familia ya injinia ilikitafsiri kitendo hicho kama ni dhihaka kwa ndugu yao, walikasirika, hivyo siku chache tuu mbeleni watu walishangaa kuona sanamu ya bata pale mguuni imeng'olewa.

Fahamu Mengi

26 Sep, 18:48


Joseph Stalin alikuwa mtawala wa Soviet Union kuanzia mwaka 1922 hadi anafariki mwaka 1953 huko Moscow akiwa na umri wa miaka 74. Jamaa ana historia kubwa sana katika utawala wake, historia ambayo inaweza kufanana na watawala wengine kama akina Adolf Hitler.

Katika maisha yake alioa mara mbili, mke wa kwanza ni Kato Svanidze aliyeishi naye kwa mwaka mmoja pekee 1906–1907, waliachana baada ya mke huyu kufariki akiwa na miaka 22.

Mwaka 1918 akaoa mke wa pili aliyekuwa anaitwa Nadezhda Alliluyeva ambaye huyu alidumu naye hadi mwaka 1932, waliachana baada ya mke huyu wapili pia kufariki kwa kujiuwa akiwa na miaka 31.

Baada ya mkewe huyu kufariki Joseph alisema kuwa huyo ndiye alikuwa mwanadamu pekee duniani aliyekua anaulainisha moyo wake, na sasa amefariki hivyo moyo wake unageuka kuwa kama jiwe, hatakua na huruma wala upendo wowote kwa binadamu yeyote.

Fahamu Mengi

22 Sep, 02:41


Kanisa Hili Linaitwa Church of the Holy Sepulchre Lililoko Jerusalem. Humo Kuna Kaburi la Mfalme Baldwin II Aliyeitawala Israel Karne ya 12. Moja ya Vitu vya Kushangaza Kumhusu ni Kwamba Aliwahi Kwenda Kuomba Mkopo, Alipoulizwa Dhamana Yake Akasema ni Ndevu Zake, na Alipewa Mkopo.

Fahamu Mengi

15 Sep, 12:22


Mwaka 1919 Tank Kubwa Lililojazwa Gallon Milion 2.3 za Molasses Lilipasuka Katika Kiwanda cha Purity Distilling Company Huko Boston US na Kupelekea 'Mafuriko' Yaliyosababisha Vifo vya Watu 21 na Wengine 150 Kujeruhiwa. Molasses ni Sukari Iliyoyeyushwa na Kuwa Kama Asali.

Inaelezwa kwamba mafuriko hayo yaliyosababishwa na mpasuko wa tank hilo kubwa yalikwenda kwa kasi ya kilomita 56 kwa saa yakipita katikati ya mitaa ya watu na kusababisha vifo vya watu 21 na majeruhi 150.

Ujazo wa gallon milioni 2.3 ni sawa na ujazo wa karibia lita milioni 9 ambazo ni sawa na zaidi pipa 35,000. Sasa waza tuu kwa sauti kwamba ujazo wa pipa 35,000 uwe katika tank moja kubwa, kisha tank hilo lipasuke kwa pressure ya juu!, unasombwa kama kumbikumbi.

Molasses ni kama asali, lakini iliyotengenezwa kwa kutumia sukari ambayo hutumika kutengenezea pombe, madawa na hata baadhi ya vyakula vya bei ghali pia.

Fahamu Mengi

13 Sep, 13:46


Hello everybody, how are you? My Name is Ruslan and I teach finance education. If you want know how to take 1million dollar you can send me my channel

Fahamu Mengi

09 Sep, 13:13


Jamii ya Tidong, Indonesia hutaruhusiwa kuuona uso wa bi harusi wako hadi umuimbie nyimbo kadhaa za mapenzi zitakazompendeza wakati wa kufunga ndoa. Pia baada ya ndoa waliooana hawaruhusiwi kuingia bafuni na chooni kwa muda wa siku 03 kuepusha mikosi katika maisha yao.

Fahamu Mengi

04 Sep, 18:41


Maria Gomez Pereira raia wa Andalusia kusini mwa Hispania akiwa nyumbani kwake jikoni akiendelea kupika aligundua kuwa sakafuni palikuwa na madoa, akawaza kuchukua tambala afute madoa hayo lakini akagundua kua ni madoa yaliyojiunga na kuonekana kama sura ya mtu.

Hali hii ilimuogopesha sana Maria, akamwambia mumewe ambaye kwa kushirikiana na mwanae wakairarua sehemu ile ya sakafu na kuijenga upya, hali ikawa shwari kwa majuma machache lakini baadae yale madoa yanayojiunga na kutengeneza sura ya mtu yakajirudia tena.

Kuona hivyo kama familia wakatoa taarifa kwa uongozi wa eneo hilo, ikashauriwa sakafu ya jikoni hapo ivunjwe, walipochimba wakagundua kuwa kuna mabaki ya miili ya watu.

Baada ya kumaliza kutengeneza sakafu hiyo sasa zilianza kuonekana nyuso nyingi sakafuni ndani humo, watu wengi walidhani labda Maria alikuwa mchawi kwakua alikuwa hahami, lakini ajabu ni kuwa hadi anafariki mwaka 2004 bado nyuso hizo zilikuwa zinaendelea kuonekana katika sakafu ya nyumba yake.

Fahamu Mengi

04 Sep, 18:39


Hii ni Picha Iliyopigwa Mwaka 1943 Wakati wa Ukoloni Nchini Kenya Ikionyesha Jinsi Wanafunzi Walivyokuwa Wakifundishwa Namna ya Kuendesha Gari, Hayo Mawe Kichwani Waliwekewa Ili Wasiangalie Chini Wakati Wa Kuendesha.

Fahamu Mengi

03 Sep, 15:48


Visiwa vya Tiwi vinapatikana mbali kaskazini mwa Australia kilomita 80 kutoka katika mji wa Darwin wa nchini humo. inaelezwa kuwa katika visiwa hivi kuna radi kubwa huwa zinapiga kila siku mara moja kati ya mwezi September hadi mwezi March kila mwaka, ni kila siku.

Radi hizo kubwa walizozipa jina la Hector, zinatajwa kuwa ndio radi kubwa zaidi kumulika na kuunguruma duniani, zinasikika kila siku asubuhi au mchana, Katika visiwa hivi kuna watu wanaishi, na hadi mwaka 2017 idadi yao ilifika watu 2,500.

Mara kadhaa wataalamu huvifanya visiwa hivyo Kama sehemu ya majaribio ya kisayansi, lakini katu hakuna anayefahamu ni kwanini radi hizo kubwa zinaendelea kusikika kila siku ikifika september hadi march.

Fahamu Mengi

30 Aug, 01:07


Dokt. William Halsted Raia wa US, Anatajwa Kuwa ni 'Baba wa Upasuaji wa Kisasa.' Alikuwa Ananunua Mashati Yake ya Kazi Kutoka Paris Ufaransa, Akivaa Anarudisha Tena ili Yafuliwe na Kupigwa Pasi Kisha Wanayarudisha US. Alifariki Mwaka 1922, Hakua Anawaamini Madobi wa US.

Fahamu Mengi

28 Aug, 09:01


Sloths ni wanyama wa kipekee wanaoishi katika misitu ya mvua ya Amerika ya Kati na Kusini, wakitambulika kwa mtindo wao wa maisha wa polepole. Wana ngozi yenye rangi ya kijani ambayo inawasaidia kujificha kutokana na wanyama wanaowawinda, na mwendo wao wa polepole unawaruhusu kuhifadhi nishati. Sloths hutumia zaidi ya masaa 20 kwa siku kulala, na wanajulikana kwa kula majani na matunda, ambayo yanaweza kuchukua siku kadhaa kuweza kuyeyuka.

Aina mbili kuu za sloths ni sloth wa tatu na sloth wa mbili, na kila mmoja ana tabia na sifa za kipekee. Sloths wana mifumo ya umwa ya ajabu, ambayo inawaruhusu kukaa chini ya maji kwa muda mrefu bila kupumua, hivyo kuwasaidia kujilinda. Ingawa wanaonekana kuwa wazuri na wanyonge, sloths wana uwezo wa kuishi katika mazingira magumu na kuhimili mabadiliko ya hali ya hewa.

Fahamu Mengi

26 Aug, 00:31


Jamii ya Watu Wanaoishi Katika Mji wa Tamil Nadu Kusini mwa INDIA Wanayo Mila ya Ajabu Ambapo ni Ruksa Kuwauwa Wazazi Wako au Ndugu Zako Waliozeeka Kama tuu Utafikia Hatua ya Kushindwa Kuwatunza na Kuwahudumia. Mila Hii Bado Ipo Mpaka Sasa, Inaitwa Thalaikoothal.