Katibu Mkuu wa CCM, Emmanuel Nchimbi amepiga marufuku tabia ya Viongozi kukamia kukata majina ya Wanachama wanaoshiriki kwenye Chaguzi mbalimbali huku akiwataka Viongozi wanaoshinda kuacha pia tabia ya kuwashughulikia ambao hawakuwapigia kura.Akiongea Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga leo October 10,2024, Nchimbi amesema “Tunapoelekea kwenye Chaguzi zetu, utekelezaji wa haki, acheni kupanga safu Viongozi bora ndio wapitishwe, ni kosa kubwa la kimaadili Kiongozi kumkamia Mwanachama kwamba safari hii tutahakikisha fulani anakatwa, kila Mwanachama ndani ya CCM ana haki sawa na mwingine”“Na tunao Watu wachache kwenye Chama chetu ambao akimaliza tu Uchaguzi wakati ameshachaguliwa kuwa Mwenyekiti au Katibu anaanza kupeleleza nani hakumuunga mkono na anaanza kuwashughulikia ambao hawakumuunga mkono hii ni tabia mbaya sana lazima tuikatae, Mtu akikupigia kura ni haki yake akikunyima ni haki yake, wewe unataka kila siku na kila Mtu akuunge mkono wewe ni Mungu!?, anayeungwa mkono na kila Mtu ni hela”#MillardAyoUPDATES